ulaya12
JF-Expert Member
- Nov 16, 2017
- 834
- 907
Jana nilienda mlimani city, katika kufanya shopping, nilipomaliza wakati natoka nikaona kuna Restaurant, nikaagiza chakula wali kwa samaki "change"na juice ya ukwaju ila kosa nililofanya sikuulizia bei
Sasa nilipomaliza kula ikafikia wakati wakulipa hela nikamuuliza muhudumu nadaiwa sh. ngapi? yule muhudumu akaenda counter akarudi na bili inasoma 18,000/= na juice 4,000/= jumla 22,000/= kwakweli niliishiwa nguvu kabisa na nilijilaumu sana kwanini sikuuliza bei kabla hadi ninaondoka pale hadi muda huu bado akili haijakaa sawa
Yaani kama nimeibiwa mwenyewe nilishazoea uswahilini 3,000/= unapata msosi wamaana kabisa ila nimejifunza kitu kuulizia bei kabla yakuagiza kamajana ningekuwa sinahela sijui wangenifanya nini