Kilichonikuta Mlimani City: Nimekula chakula na kupewa bili kubwa nisiyotarajia

Kilichonikuta Mlimani City: Nimekula chakula na kupewa bili kubwa nisiyotarajia

Jana nilienda mlimani city, katika kufanya shopping, nilipomaliza wakati natoka nikaona kuna Restaurant, nikaagiza chakula wali kwa samaki "change"na juice ya ukwaju ila kosa nililofanya sikuulizia bei

Sasa nilipomaliza kula ikafikia wakati wakulipa hela nikamuuliza muhudumu nadaiwa sh. ngapi? yule muhudumu akaenda counter akarudi na bili inasoma 18,000/= na juice 4,000/= jumla 22,000/= kwakweli niliishiwa nguvu kabisa na nilijilaumu sana kwanini sikuuliza bei kabla hadi ninaondoka pale hadi muda huu bado akili haijakaa sawa

Yaani kama nimeibiwa mwenyewe nilishazoea uswahilini 3,000/= unapata msosi wamaana kabisa ila nimejifunza kitu kuulizia bei kabla yakuagiza kamajana ningekuwa sinahela sijui wangenifanya nini
Lawama ya kwanza kwanini hukwenda kufanya shopping Kariakoo badala yake ukaenda Mlimani City?

Status uliyokuwa unaitafuta ndio hiyo menu ya TZS 18,000 hata hivyo hii bei haijafika hata US$ 10 sijui kwa nini unalalama
 
Bahati yako hukuwa umepita hapo na mpenzi wako uliyetaka kumuimpress. Kama hiyo 22 thao inakuuma mpaka leo, ingekuja bill ya Tshs. 60,000/- labdacungeokotewa Muhimbili😀. Pole sana Kamanda.
 
Jana nilienda mlimani city, katika kufanya shopping, nilipomaliza wakati natoka nikaona kuna Restaurant, nikaagiza chakula wali kwa samaki "change"na juice ya ukwaju ila kosa nililofanya sikuulizia bei

Sasa nilipomaliza kula ikafikia wakati wakulipa hela nikamuuliza muhudumu nadaiwa sh. ngapi? yule muhudumu akaenda counter akarudi na bili inasoma 18,000/= na juice 4,000/= jumla 22,000/= kwakweli niliishiwa nguvu kabisa na nilijilaumu sana kwanini sikuuliza bei kabla hadi ninaondoka pale hadi muda huu bado akili haijakaa sawa

Yaani kama nimeibiwa mwenyewe nilishazoea uswahilini 3,000/= unapata msosi wamaana kabisa ila nimejifunza kitu kuulizia bei kabla yakuagiza kamajana ningekuwa sinahela sijui wangenifanya nini

Kama umezoea ushahilini unaagizaje bila kuangalia menu au kuuliza bei? mi nikiingia mahali sijapazoea, huwa nakuwa na 50.000 kama nipo mwenye au nauliza bei kwanza
 
Uwiiii pole mkuu mimi nilienda arusha kumfata hubby so jioni akaniambia twende impala sasa hubby yeye ni mzee wa konyagi always akaagiza konyagi yake na mie nikaagiza savana yangu +indian food ile kumaliza tunataka kuondoka tukaomba bill lohh kuangalia bei ya konyagi ni tsh 79000 nilishangaa sana na hela iliniuma sana kwa kwl duh.....siku ya pili gold crest tukaenda inauzwa 45 kitu kama hicho!! Nikasema shkamoooo arusha
Pole aise bora wangeandika tourists only
 
Kuna siku nilikutana na washkaji zangu 2 tukaenda maeneo fulani kule sinza tukaagiza kiti moto kg 2½ rost na ndizi, tukapiga na beer kadhaa nikajikuta nalipa 78000/=sitasahau [emoji16][emoji16]
 
Kununua kitu bila kuuliza bei, hususan katika mazingira mengi ya Tanzania ni kualika kulanguliwa.

Yani hata kama kuna discount unaweza usiambiwe, kwa sababu umejionesha hujali.
 
Pole sana...

Kama hukutarajia na hukujipanga kwa hilo, inashtusha sana...

Unaweza hisi kuna mkono wa mtu...

Cc: mahondaw
 
Wanaume wa Dar mnapenda sana kulalamika aiseeeee........
Mlisha zowea kula chips za 2000 na miguu ya kuku huko tandale ehhhh...[emoji12] [emoji12] [emoji12]
Wewe umezoea kula udaga na vile viwadudu vinaitwa senene kwa Sh 800...ugali wa rangi 500/na wadudu sh 300..maji bure kwenye jagi kwa mama muuza....tehe teheee.
 
Wewe umezoea kula udaga na vile viwadudu vinaitwa senene kwa Sh 800...ugali wa rangi 500/na wadudu sh 300..maji bure kwenye jagi kwa mama muuza....tehe teheee.
Huo mlo ndio unaleta heshima ndani sasa....... yaani baada ya hapo lazima shkamoo irudi kwao....[emoji12] [emoji12] [emoji12]
 
Vzuri uweunauliza vnginevyo uo ujasili uweunapesa zakutosha...
 
Mkuu ungeenda kule ndani ukamuone Mgr wao akueleze bei ya Kweli hao wahudumu siyo waaminifu wanachomekea watu bei ya Juu !
Mimi huwa nawatega mwishoni huwa nawazingua nawaambia Mimi nimezaliwa Muhumbili kwa hiyo kutaka kuniibia itabidi mfanye kazi ya ziada!
Wale wafanyakazi siyo waaminifu kabisa Yani nimeshawakata mara kadhaa!
 
Back
Top Bottom