Kilichonikuta Mlimani City: Nimekula chakula na kupewa bili kubwa nisiyotarajia

Kilichonikuta Mlimani City: Nimekula chakula na kupewa bili kubwa nisiyotarajia

Pole sana. Mie iliwahi kunikuta lakini tofauti na ya kwako. Niliwachukuwa warembo watatu kwenda Lunch mimi ndiye mlipaji kusherehekea Birthday ya mmoja wao. Kila mtu kaagiza atakacho tukala na kunywa kwa raha zetu. Sasa wakati wa kulipa umefika kumbe pochi nimesahau nyumbani. Dah! bahati nzuri hiyo sehemu nilikuwa naenda kula mara nyingi tu owners hata wale waiters wote walinifahamu mpaka jina. Nikawafahamisha tu kwamba nimesahau pochi home nitawapitisia haki yao kesho. Wakakubali bila usumbufu wowote. Sijui kama ingekuwa ni sememu ambayo hawanifahamu ingekuwaje sipendi kumbembesha mzigo mtu usiyemhusu ingawaje mmoja wa warembo alitaka kulipa nikamkatalia kata kata.

Jana nilienda mlimani city, katika kufanya shopping, nilipomaliza wakati natoka nikaona kuna Restaurant, nikaagiza chakula wali kwa samaki "change"na juice ya ukwaju ila kosa nililofanya sikuulizia bei

Sasa nilipomaliza kula ikafikia wakati wakulipa hela nikamuuliza muhudumu nadaiwa sh. ngapi? yule muhudumu akaenda counter akarudi na bili inasoma 18,000/= na juice 4,000/= jumla 22,000/= kwakweli niliishiwa nguvu kabisa na nilijilaumu sana kwanini sikuuliza bei kabla hadi ninaondoka pale hadi muda huu bado akili haijakaa sawa

Yaani kama nimeibiwa mwenyewe nilishazoea uswahilini 3,000/= unapata msosi wamaana kabisa ila nimejifunza kitu kuulizia bei kabla yakuagiza kamajana ningekuwa sinahela sijui wangenifanya nini
 
uje Arusha ukale lunch kibo palace, palace hotel...siku moja tulikuwa na mkutano nikala pale, sasa nilikuwa nakula na sign kwenye risiti mwisho wa siku watanipa bili nikagundua kumbe wali kuku au samaki ni sh 42,000. fresh juice 8,000, maji madogo sh 2,500. mchana tulikuwa tunakula kwenye mkutano usiku ndo kila mtu anajilipia bili ya chakula cha jioni. sasa nambie siku 5 nililipa sh ngapi hapo, nikagundua wageni walikuwa wanakunywa chai usiku hawakuwa wanakula nikagundua kwanini. sasa sema iyo bili yako badu kubwa au ni zaidi ya hii yakwangu au. hayo ndo maisha mbidada lazima ule na ulipe ili uhadisie kuwa siku moja...ila pesa hazikuwa zakwangu nilipewa tu nitumie basi
 
Ila kweli kama ameweza kufanya shopping mlimani city nadhan hawezi shangaa bei hiyo ya chakula maana vitu tu vya mliman vina bei mara tatu ya vitu vya sehemu nyingine sasa nadhan anazingua tu
Kipindi hicho mimi na mshikaji wangu fulani tulikuaga tunaenda kushangaa shangaa tuakingiaga duka fulani hivi pembeni ya game supermarket either maduka mawili au matatu baada ya Game kuna viatu vinauzwa mpaka laki 8 hio ilikua 2013 aisee tulikua tunacheka sana maana mshikaji wangu alikua anakiatu kama hicho cha laki nane sema cha mtumba na ni vya kawaida sana..
 
Bora wewe apo ni mlimani city mi niliendaga mbagara zakhemu kuna stationary moja niliingia nikakuta wadau wanapiga juice mule kutokana na khali ya uchovu na joto maana kazi yangu nilikuwa nasubiri hadi nusu saa ndo ikamilike nikaagiza juice na Mimi uku moyoni nikijua itakuwa mia tano ikizidi sana buku nikapiga glass ya kwanza ikaisha nikaagiza ya pili mwishoni nikamalizia mchanganyiko wa juice ya ukwaju matikiti sijui na matakataka gani Ile namaliza nikatoa 5000 nimkatie dada akanambia mbona pesa haitoshi nikashaangaa akanambia zile juice za parachichi ni 5000 na ule mchanganyiko 7000 nikampa 17000 yake nikasema poa tu
Mkuu nimecheka mpaka mbavu zinauma hahaha, Sio kwamba ulipark ndiga nje wakaona wewe wakishua ndo wakapandisha bei
 
Back
Top Bottom