BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,165
Pole sana. Mie iliwahi kunikuta lakini tofauti na ya kwako. Niliwachukuwa warembo watatu kwenda Lunch mimi ndiye mlipaji kusherehekea Birthday ya mmoja wao. Kila mtu kaagiza atakacho tukala na kunywa kwa raha zetu. Sasa wakati wa kulipa umefika kumbe pochi nimesahau nyumbani. Dah! bahati nzuri hiyo sehemu nilikuwa naenda kula mara nyingi tu owners hata wale waiters wote walinifahamu mpaka jina. Nikawafahamisha tu kwamba nimesahau pochi home nitawapitisia haki yao kesho. Wakakubali bila usumbufu wowote. Sijui kama ingekuwa ni sememu ambayo hawanifahamu ingekuwaje sipendi kumbembesha mzigo mtu usiyemhusu ingawaje mmoja wa warembo alitaka kulipa nikamkatalia kata kata.
Jana nilienda mlimani city, katika kufanya shopping, nilipomaliza wakati natoka nikaona kuna Restaurant, nikaagiza chakula wali kwa samaki "change"na juice ya ukwaju ila kosa nililofanya sikuulizia bei
Sasa nilipomaliza kula ikafikia wakati wakulipa hela nikamuuliza muhudumu nadaiwa sh. ngapi? yule muhudumu akaenda counter akarudi na bili inasoma 18,000/= na juice 4,000/= jumla 22,000/= kwakweli niliishiwa nguvu kabisa na nilijilaumu sana kwanini sikuuliza bei kabla hadi ninaondoka pale hadi muda huu bado akili haijakaa sawa
Yaani kama nimeibiwa mwenyewe nilishazoea uswahilini 3,000/= unapata msosi wamaana kabisa ila nimejifunza kitu kuulizia bei kabla yakuagiza kamajana ningekuwa sinahela sijui wangenifanya nini