Wewe Maggid, usifikiri Watanzania ni Mabwege; Wewe endelea na ndoa yako na hao jamaa, hizo pesa wanazokupa utakuja Kujuta nazo
Well, hata matatizo huzidiana..tuanze na tatizo kuu..tusafishe kwanza Magogoni..PERIOD.Mpenda chongo, chongo huita kengeza. Kama Dr. Slaa alifanya anayoshutumiwa basi hakumtendea haki kiongozi MWENZIE!
Amandla........
Ama kweli kipendacho moyo! chongo huliita kengeza.
Yaani nyote mumeshindwa kumwelewa Maggid.
Utawala wa kihuni na kupayuka payuka anaoukusudia Dkt Slaa si kwamba hatuutaki tu bali haufai popote duniani. Hata Mrema alijaribu akashindwa.
Lakini huyu jamaa hashindwi na wala haoni vibaya na hilo.Ikiwa ameweza kupora mke wa mtu na kumshika mkono mbele ya umati akimdhalilisha mumewe,atashindwa na hilo?.
Na huyu anapigania demokrasia.....and so was Kagame, Hitler, Museveni etc...damn even Fodey Sankoh was..sijamuongelea Meles na mwenzie Aferweki
Maggid,Ndugu Zangu,
Nimeona mada niliyoianzisha kwenye mjengwablog imeingizwa humu na wengi wameshiriki kuichangia, na mimi pia. Mada inasema " Nilichokiona Jana pale Mwembetogwa". Lakini ziada ya pale Mwembetogwa ni ukweli kuwa mwanzoni kabisa mwa hotuba yake, Dr Slaa alitoa kauli mbele ya umati ule. Kauli ambayo binafsi niliisikia na ilinishtua sana. Dr Slaa alisikika akitamka kuwa kuna kiongozi wa mkoa ( CHADEMA) ( Alimtaja jina) ambaye amehongwa na mgombea ubunge wa CCM jimbo lingine la Iringa ( naye alimtaja jina) ili asirudishe fomu zake. Dr Slaa akataka kiongozi huyo wa zamani wa CHADEMA apuuzwe na akitaka aende mahakamani.
Nadhani katika wakati huu kuna umuhimu wa kuwafahamu zaidi wagombea wetu. Na kumtakia mema Dr Slaa ni pamoja na kumwambia yale tunayoyaona ni mapungufu. Si kummwagia sifa tu. Maana, kwa kitendo kile, Dr Slaa kwa mtazamo wangu alimdhalilisha kiongozi yule wa CHADEMA mbele ya umati ule. Na bahati mbaya au nzuri kiongozi huyo wa CHADEMA alikuwapo. Kwa macho yangu nilimwona kiongozi huyo wa CHADEMA akishiriki kupiga makofi kuungana na umati uliokuwa ukishangilia kauli ya Dr Slaa. Masikini, kiongozi yule wa CHADEMA, bila shaka alipigwa na butwaa na hakuwa na la kufanya bali naye kupiga makofi!
Kwangu nilishtushwa na kusikitishwa sana. Bado naamini Dr Slaa hakumtendea haki kiongozi yule wa CHADEMA. Kama Dr Slaa alikuwa na ushahidi wa alichokisema, basi, hakuwa na haja ya kumtuhumu na kumtolea hukumu kiongozi yule pale hadharani. Kiongozi yule wa CHADEMA aliyehukumiwa hadharani ni mwanajamii hapa Iringa. Ameshapigwa mhuri mbaya bila hata kupewa fursa ya kujitetea. Kwa mzazi kama mimi naelewa jinsi kiongozi yule atakavyojisikia vibaya mbele ya familia yake, mke na watoto wake. Kwamba ametoka kwenye mkutano wa mgombea urais huku yeye akitajwa hadharani kuwa amehongwa asirudishe fomu.
CHADEMA wana vikao vyao, kwa kutanguliza busara wangeyamaliza ya kwao kwenye vikao vyao vya ndani, si hadharani. Na kama mgombea Urais, Dr Slaa anapaswa awe mfano wa kuheshimu utawala wa sheria. Hili ningelisema kama nilivyolisema hata kama lingefanywa na Kikwete wa CCM, Lipumba wa CUF au mgombea ye yote yule. Nisingelisikia nikalinyamazia. Kuandika ni kushauri pia. Tusingependa Dr Slaa apitishwe njia ya Mrema, ina miba na matope. Anayesoma na kuhusika na kilichoandikwa ana uhuru wa kupokea ushauri na kuufanyia kazi au kuachana nao. Nimechokoza mjadala....
Maggid,
Iringa.
Mkuu naona unatumia alama za freemassonary. Slaa akiingia madarakani, masuala ya wanajimu na ulinzi wa majini hautakuwa na nafasi tena. Jiandae tu na kimbembe cha kukosa ajira.Ama kweli kipendacho moyo! chongo huliita kengeza.
Yaani nyote mumeshindwa kumwelewa Maggid.
Utawala wa kihuni na kupayuka payuka anaoukusudia Dkt Slaa si kwamba hatuutaki tu bali haufai popote duniani. Hata Mrema alijaribu akashindwa.
Lakini huyu jamaa hashindwi na wala haoni vibaya na hilo.Ikiwa ameweza kupora mke wa mtu na kumshika mkono mbele ya umati akimdhalilisha mumewe,atashindwa na hilo?.
Uko hapa tangu 2006 hujui lugha za jf? ohhhhhhhhhhh ni kwa sababu unaingia hapa kwa msimu wa miaka mitano mitano?Great thinkers na lugha zao!
Ndugu zangu
So far,malengo ya Mjengwa yanaelekea kutimia: KU-DIVERT ATTENTION YETU.Hivi hakuna anayejiuliza kwamba kwanini ghafla huyu jamaa kahamisha nguvu zake kutoka kwenye kiblogu chake cha picha na kijarida mfu cha Kwanza Jamii (kilichozaliwa baada ya kifo cha asili cha Gozi Spoti) na kuja kwa KASI ZAIDI,ARI ZAIDI na NGUVU ZAIDI hapa JF huku mada zake zikilenga TUMJADILI YEYE BADALA YA KIKWETE NA MAFISADI WENZIE WA CCM?
Sidhani kama Mjengwa ni msahaulifu as such bali anajua sana anachofanya i.e ku-earn kihalali ujira wake.This is the same person ambaye jana "alitoa hukumu" kwa Chadema,CUF na CCM huku akijipa majukumu ya Jaji Lewis Makame kutangaza matokeo ya uchaguzi huo kabla hata ya siku ya kupiga kura.Leo anajifanya kasahau na kumtaka Dokta Slaa asimhukumu mgombea fisadi.Hili sio la kushangaza kwa "mwandishi" ambaye hajawahi kuona mapungufu,udhaifu au ubovu wa Jakaya Kikwete kwa muda wote ambao amekuwa madarakani.Kutarajia Mjengwa azungumzie list of shame,EPA,Richmond,Kagoda,Meremeta,etc ni sawa na kutarajia Kikwete aite independent health specialists wa kumpima afya yake na kuiweka hadharani.Au ni sawa na kutarajia Makamba aitishe press conference na kutueleza kwanini alifikuzwa ualimu zamani hizo.
Najua ni vigumu kuwapuuza watu wa aina ya Mjengwa lakini kwa vile tupo katika mapambano muhimu kwa future yetu na vizazi vijavyo basi yatupasa tuelekeze zaidi focus na nguvu zetu kwenye mapamabano hayo na kuwapuuza the Mjengwas.Tunapaswa kukumbuka kuwa wenzetu hawa wapo kazini,na ujira wao unategemea sana impact ya wanavyotekeleza maagizo ya waliowatuma.
Lakini kwa upande mwingine angalau kadri Mjengwa anavyojibidiisha kama attention seeker (i.e. attention ya mafisadi na yetu pia) ndivyo anavyowasaidia wale waliokuwa hawamjui vizuri "mwanafilosofia" huyu.Sie wengine tulishamfahamu mapema tangu alipoanza "kuteleza" kabla ya uchaguzi wa mwaka 2005,na jinsi alivyokuwa akihangaika kusaka attention kwa kuanzisha vijarida vilivyoishia kufa vifo vya asili (Gozi Spoti na sasa hilo Kwanza Jamii).Alidhani vijarida hivyo vingeweza kutumika kama forums nzuri ya kutughilibu lakini Inshallah Mungu hafichi mnafiki.
Pengine anatarajia japo u-DC baada ya kusahauliwa na JK mwaka 2005-2010....but my advice is to just ignore him.Best way to deal with attention seekers is to ignore them.Kama hatujihangaishi kubishana na Malaria Sugu au TandaleOne (in which case either of them might actually be Mjengwa) kwanini basi tupoteze muda wetu kumfanikishia Mjengwa mission yake ya ku-divert attention yetu?
Kinachomsumbua Mjengwa ni njaa tu.......Ukiwa na njaa huna mawazo huru!
Kama kazi ya kuandika balanced news umeshindwa muombe Muhingo uingie kwenye Team ya Campaign!
Ndugu Zangu,
Nimeona mada niliyoianzisha kwenye mjengwablog imeingizwa humu na wengi wameshiriki kuichangia, na mimi pia. Mada inasema " Nilichokiona Jana pale Mwembetogwa". Lakini ziada ya pale Mwembetogwa ni ukweli kuwa mwanzoni kabisa mwa hotuba yake, Dr Slaa alitoa kauli mbele ya umati ule. Kauli ambayo binafsi niliisikia na ilinishtua sana. Dr Slaa alisikika akitamka kuwa kuna kiongozi wa mkoa ( CHADEMA) ( Alimtaja jina) ambaye amehongwa na mgombea ubunge wa CCM jimbo lingine la Iringa ( naye alimtaja jina) ili asirudishe fomu zake. Dr Slaa akataka kiongozi huyo wa zamani wa CHADEMA apuuzwe na akitaka aende mahakamani.
Nadhani katika wakati huu kuna umuhimu wa kuwafahamu zaidi wagombea wetu. Na kumtakia mema Dr Slaa ni pamoja na kumwambia yale tunayoyaona ni mapungufu. Si kummwagia sifa tu. Maana, kwa kitendo kile, Dr Slaa kwa mtazamo wangu alimdhalilisha kiongozi yule wa CHADEMA mbele ya umati ule. Na bahati mbaya au nzuri kiongozi huyo wa CHADEMA alikuwapo. Kwa macho yangu nilimwona kiongozi huyo wa CHADEMA akishiriki kupiga makofi kuungana na umati uliokuwa ukishangilia kauli ya Dr Slaa. Masikini, kiongozi yule wa CHADEMA, bila shaka alipigwa na butwaa na hakuwa na la kufanya bali naye kupiga makofi!
Kwangu nilishtushwa na kusikitishwa sana. Bado naamini Dr Slaa hakumtendea haki kiongozi yule wa CHADEMA. Kama Dr Slaa alikuwa na ushahidi wa alichokisema, basi, hakuwa na haja ya kumtuhumu na kumtolea hukumu kiongozi yule pale hadharani. Kiongozi yule wa CHADEMA aliyehukumiwa hadharani ni mwanajamii hapa Iringa. Ameshapigwa mhuri mbaya bila hata kupewa fursa ya kujitetea. Kwa mzazi kama mimi naelewa jinsi kiongozi yule atakavyojisikia vibaya mbele ya familia yake, mke na watoto wake. Kwamba ametoka kwenye mkutano wa mgombea urais huku yeye akitajwa hadharani kuwa amehongwa asirudishe fomu.
CHADEMA wana vikao vyao, kwa kutanguliza busara wangeyamaliza ya kwao kwenye vikao vyao vya ndani, si hadharani. Na kama mgombea Urais, Dr Slaa anapaswa awe mfano wa kuheshimu utawala wa sheria. Hili ningelisema kama nilivyolisema hata kama lingefanywa na Kikwete wa CCM, Lipumba wa CUF au mgombea ye yote yule. Nisingelisikia nikalinyamazia. Kuandika ni kushauri pia. Tusingependa Dr Slaa apitishwe njia ya Mrema, ina miba na matope. Anayesoma na kuhusika na kilichoandikwa ana uhuru wa kupokea ushauri na kuufanyia kazi au kuachana nao. Nimechokoza mjadala....
Maggid,
Iringa.
ndugu zangu,
nimeona mada niliyoianzisha kwenye mjengwablog imeingizwa humu na wengi wameshiriki kuichangia, na mimi pia. Mada inasema " nilichokiona jana pale mwembetogwa". Lakini ziada ya pale mwembetogwa ni ukweli kuwa mwanzoni kabisa mwa hotuba yake, dr slaa alitoa kauli mbele ya umati ule. Kauli ambayo binafsi niliisikia na ilinishtua sana. Dr slaa alisikika akitamka kuwa kuna kiongozi wa mkoa ( chadema) ( alimtaja jina) ambaye amehongwa na mgombea ubunge wa ccm jimbo lingine la iringa ( naye alimtaja jina) ili asirudishe fomu zake. Dr slaa akataka kiongozi huyo wa zamani wa chadema apuuzwe na akitaka aende mahakamani.
Nadhani katika wakati huu kuna umuhimu wa kuwafahamu zaidi wagombea wetu. Na kumtakia mema dr slaa ni pamoja na kumwambia yale tunayoyaona ni mapungufu. Si kummwagia sifa tu. Maana, kwa kitendo kile, dr slaa kwa mtazamo wangu alimdhalilisha kiongozi yule wa chadema mbele ya umati ule. Na bahati mbaya au nzuri kiongozi huyo wa chadema alikuwapo. Kwa macho yangu nilimwona kiongozi huyo wa chadema akishiriki kupiga makofi kuungana na umati uliokuwa ukishangilia kauli ya dr slaa. Masikini, kiongozi yule wa chadema, bila shaka alipigwa na butwaa na hakuwa na la kufanya bali naye kupiga makofi!
Kwangu nilishtushwa na kusikitishwa sana. Bado naamini dr slaa hakumtendea haki kiongozi yule wa chadema. Kama dr slaa alikuwa na ushahidi wa alichokisema, basi, hakuwa na haja ya kumtuhumu na kumtolea hukumu kiongozi yule pale hadharani. Kiongozi yule wa chadema aliyehukumiwa hadharani ni mwanajamii hapa iringa. Ameshapigwa mhuri mbaya bila hata kupewa fursa ya kujitetea. Kwa mzazi kama mimi naelewa jinsi kiongozi yule atakavyojisikia vibaya mbele ya familia yake, mke na watoto wake. Kwamba ametoka kwenye mkutano wa mgombea urais huku yeye akitajwa hadharani kuwa amehongwa asirudishe fomu.
Chadema wana vikao vyao, kwa kutanguliza busara wangeyamaliza ya kwao kwenye vikao vyao vya ndani, si hadharani. Na kama mgombea urais, dr slaa anapaswa awe mfano wa kuheshimu utawala wa sheria. Hili ningelisema kama nilivyolisema hata kama lingefanywa na kikwete wa ccm, lipumba wa cuf au mgombea ye yote yule. Nisingelisikia nikalinyamazia. Kuandika ni kushauri pia. Tusingependa dr slaa apitishwe njia ya mrema, ina miba na matope. Anayesoma na kuhusika na kilichoandikwa ana uhuru wa kupokea ushauri na kuufanyia kazi au kuachana nao. Nimechokoza mjadala....
Maggid,
iringa.