Elections 2010 Kilichonishtua Juu Ya Dr Slaa Pale Mwembetogwa


Mchukia ufisadi, huyu si mwandishi hivyo hata zile A, B, C za uandishi hazifahamu. Alikurupuka tu kuandika bila hata ya kutafakari mantiki ya anachoandika. Ni bora tu akaendelea kuandika kuhusu Chai na Chapati nyumbani kwa michuzi badala ya kudandia field ambayo haijui hata kidogo.
 
Huyo mtu ambaye Majjid anasema hakutendewa haki ni kiongozi wa Chadema(Mkoa) na alikuwa anataka kugombea ubunge kwa hiyo tunajua kwamba anauwezo mkubwa kiakili. Kama anaona hajatendewa haki anajua njia ipi achukuwe.
 
Maggid,
Duh, labda nikuulize wewe, Hivi Hitler alipewa nafasi ya kujitetea na mbona anatuhukumiwa kwa yote aloyafanya..au tumseme mtu mdogo sana kama Osama naye vipi hutuwezi kuzungumza mabaya yake hadi afikishwe mahakamani? mbona viongozi wote duniani wanamzungumzia huyu mtu mdogo ktk majukwaa na sijakusikia hata siku moja ukiandika kusikitishwa na viongozi hao. Kama wewe unayo habari tofauti na Dr.Slaa alozungumza yasema wazi nasi tutapima makosa ya Dr.Slaa.

Mkuu wangu umechemsha hata kama unatafuta ligi basi haiendi hivi.. jaribu sana kutafuta mada yenye mvuto zaidi toka hotuba za Dr.Slaa kisha hapo weka staha kiasi kwamba hata mimi naweza fikiria kweli mpira umeahirishwa kuliko kuwaona vibaka wa kiboko msheri wakirudi, nitajua fika wahuni hao hawana uwezo wa kulipa kiingilio wanatafuta mnyonge.
 

Kuchokoza mjadala au kuuthibitishia umma kuhusu ubabaishaji wako?Mjadala gani uko one-sided?

Wewe hutochoka au njaa yako ndio inakufanya usichoke?

Sio siri,Dkt Slaa akiingia Ikulu kilio hakitakuwa kwa akina Rostam na mafisadi wenzie pekee bali hata wababaishaji kama Mjengwa.Sijui ataandika nini tena!
 
Maggid hiki siyo kipindi cha kuoneana aibu wala nini!!!

huyo mwenyekiti hakufanya vibaya na hiyo iwe fundisho kwako na kwa jamii nyingine kuwa hiki siyo kipindi wala hakuna tena kipindi kitakuja wewe au mtu mwingine aonewe aibu kwa ujinga anaofanya..

huyo mwenyekiti ndiyo ameisha kisiasa na kamwe hakuwa mtu tena mwaminifu na wakutumainiwa katika jamii inayomzunguka....

ukiwa mwana mageuzi simama katika haki na tetea hoja hako..

People Power!!!!!!
 
Hivi huyu kijana alipomaliza shule yake tambaza alikwenda wapi...........alisomea chuo gani...........inaku/tupa picha gani...........if y'all know what i mean............
 
Mr Mjengwa, in the past you were attention-seeker activist blogger openly supporting CUF. I don't know what has happened to your relationship with CUF. I see you are indirectly trying to infiltrate CCM by bashing Dr Slaa. No way!
CCM supporters do not like your dumb tricks and we condone your low class behavior.
You better stick with what you write and believe in your nonesense and useless blog. All you write and post in your cheap blog is telling people "ooh I was in Sweden, ooh This morning I was in Moro, Oooh I was in KLM flight etc"...who cares or give a sh-it!
Unlike your cheap blog, this is JF where everybody is allowed to express his/her thoughts.
My advice to you: Do keep taking those funny street photos about things or events that make no sense and continue to write those dumb poems of yours.
This is not a blog for small minded and dumb folks like you or your stupid followers. JF is open for everybody.
Please do not come here. Don't even come to Dar. Stay with your dumb issues in Iringa. Stay with CUF or TLP!
Vote CCM
 
na wewe unafanya nini hapa?
 

Kadhalilishwa au kajidhalilisha mwenyewe? Mbali na hivyo yeye kadhalilisha watanzania wote wenye mapenzi mema,...., ila kweli watu huwa tuna fikra na upeo tofauti, vinginevyo hiyo statement hata mtu ambaye hajasoma kabisa hawezi kuitaja katika mazingira kama haya. Mshauri aende mahakamani!
 

Maggid,unaposema mtu mdogo sana una maana gani. Huyu bwana alitarajia kuwa mbunge,na uwezekano wa kuwa waziri kama mbunge ungekuwepo. La sivyo huyu bwana angeingia katika kamati za bunge. Kama amerubuniwa kwa vijisenti na kuwasaliti Chadema,usaliti huo ungeendelea kwa wakati akiwa kiongozi. Mbunge ni mtunga sheria,ndio wanaojadili masuala ya kiuchumi,kijamii na kiusalama, unaposema ni mtu mdogo sijui ni kwa misingi gani. Hebu tufahamishe yaweza kuwa una hoja muungwana.
Mimi ni msomaji wa makala zako ndani ya raia mwema,ni mtembeleaji mzuri wa blog yako ambayo imejikita kuonyesha uhalisia wa maisha ya mtanzania kule kijijini,hili nakupongeza sana. Kinachonishangaza ni wewe unayeyajua maisha ya kule nyeregete yanavyowakamaua wananchi,bado unadiriki kumtetea kiongozi ambaye ameonyesha wazi kujali kula na si masilahi ya taifa, kwa maana kuwa mbunge bila kujali anatoka chama gani ni kiongozi wa taifa tayari. Nasema kumtetea kwasababu hujatuthibitishia kuwa Dr Slaa hana taarifa za uhakika za huyu bwana,kana kwamba amehukumiwa bila kusikilizwa. Umetoa hukumu bila kumhoji Dr Slaa au kutueleza mahojiano na huyo bwana. Dr amempa uhuru aende mahakamani kama alivyowahi kuwaambia mafisadi wa mwembe yanga waende mahakamani, kielelezo cha uhakika wa yale anayoyasema.
Maggid, sisi ni masikini sana,lakini umasikini wetu si wa rasilimali, ni uzembe wa kulindana na kuoneana haya. Leo waliofuja mabilioni ya walala hoi wakiwemo wa Nyeregete eti wanapigiwa debe ni watu safi,ni mapanga ya zamani yenye makali. Vikao vya Chama vitajadili nini zaidi kama mwenyekiti amesema ni watu safi. Hatuwezi kuendelea na utaratibu huu wa kijinga wa kulindana, tuwataje wasaliti wote wa maendeleo yetu hadharani ili ifike wakati mtu akiwa na tuhuma anajinyonga kama kule Japan wanavyofanya ili kuepuka fedheha ya taifa. Ndio maana japan wapo hapo walipo.
Kule China kiongozi aliyesababisha uzembe wa maziwa alitajwa hadharani, akahukumiwa TV zikionyeshwa,hakuna vikao vya ndani wakati wa kupigania maendeleo. Labda nikuulize vikao vya ndani vya Chadema vingebaini kuwa ni msaliti 'So what''! yaishie uvunguni eti tumsitiri ana mke ana watoto,kama anajua hivyo asingefanya alichokifanya.
Naomba kutoa hoja
 
Majid alitaka Slaa aunde tume ya kumchunguza huyo jamaa. No chance for that in CHADEMA. I have been dreaming for a president like Slaa for long time. Mungu tusaidie tumpate huyu mtu atuongoze... Amen.
 
Kama ni kweli hakuhongwa, si arudishe hiyo fomu? Vikao hivyo vya siri wanavyoendekeza CCM ndivyo vinavyotumaliza kwa kufukia maovu! Muovu awekwe hadharani, na kama si muovu basi adhibitishe....!
 
ahahahaaahhahahhahha
maaaagid!!

jamaa anataka kuwa mwamndishi wa habari wa ikuru!!!
 
Me nadhani ni sawa tu, its calling a spade a spade and not a big spoon, Slaa ana data na mara nyingi haropoki ovyo vinginevyo angesha shitakiwa!
 
Bado napata shida kidogo kuelewa, huyu jamaa alihongwa asirudishe fomu je alirudisha au haukurudisha? na je Slaa alitaka kiongozi yupi apuuzwe? nahisi labda Maggid kwa makusudi kabisa anataka kupotosha ukweli au la hakuelewa. Maana haiingii akilini huyu jamaa alihongwa na CCM asirudishe fomu halafu ( na hakurudisha??) iweje hadi sasa bado awe kiongozi wa Chadema na hata baada ya kuwasaliti?. Nahisi huyu kiongozi yeye mwenyewe ndio alimwambia Slaa kuhusu kutakwa kuhongwa ( maana nijuavyo Chadema wamesimamisha mgombea Iringa mjini), so Slaa alitaka Kiongozi wa CCM aliyetaka kuhongwa ndio apuuzwe, na ndio sababu hata huyo Kiongozi "aliyedhalilishwa" alikuwa akipiga makofi. Sio kuwa alipiga makofi eti sababu hakuwa na jinsi, no alipiga makofi sababu Slaa alikuwa anampa makavu Monica Mbega. Tafadhali walioko Iringa na waliofanikiwa kuhudhulia mkutano huo hebu mtujuze zaidi, mimi sina imani na habari hii ya Mjengwa!
 
What if wapenzi wa Dr Slaa wangemvaa na kumrarua mtuhumiwa huyo.....bado tungeendelea ndoto za Utawala bora kutoka kwake???? ust thinking loudly........As a duty for critical citizenry..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…