Emma Lukosi
JF-Expert Member
- Jul 22, 2009
- 929
- 147
Ni bora ukafanye maisha yako mengine kuliko kujikombakomba, Kwa taarifa yako nilikua field Pale DailyNews Nafasi za kupachikwa kwa sasa zimejaa. kama ulikua unategemea ka promo imekula kwako.Kama una frustrations zako nyingine ziwezi kukusaidia. Maswali nimeyaona na aliyeuliza hakunilazimisha niyajibu. Kuna maelezo ya jumla nimeyatoa kutokana na maswali hayo. Mengine nitajibu nitakapotaka na kama nitaweza kuyajibu yote siwezi kusema sasa. Mimi ni mtu huru na najivunia uhuru wangu. Nina maisha yangu mengine. Yanahitaji muda wangu pia.
Kama una frustrations zako nyingine ziwezi kukusaidia. Maswali nimeyaona na aliyeuliza hakunilazimisha niyajibu. Kuna maelezo ya jumla nimeyatoa kutokana na maswali hayo. Mengine nitajibu nitakapotaka na kama nitaweza kuyajibu yote siwezi kusema sasa. Mimi ni mtu huru na najivunia uhuru wangu. Nina maisha yangu mengine. Yanahitaji muda wangu pia.
Jibu hoja kwa hoja acha vioja bwana MAJID MJENGWA aka MAGGID.
JMushi,
Kuna mwandishi wa habari alikamatwa na kufikishwa kwa Idi Amin. Aliamini kuwa ungekuwa ni mwisho wake. Idi Amin alitamka na kumwuliza mwandishi yule swali moja tu; " Nyinyi waandishi wa habari mnaandika mambo mengi mbaya kuhusu mimi. Sasa nikuulize kijana, hivi katika yote ninayoongea na ninayoyafanya hakuna hata moja lililo zuri?" Mwandishi yule akajibu; " Yapo mengi Mkuu".
Idi Amin akatamka; " Basi, nenda kaandike moja tu lililo zuri kuhusu mimi!" Tafakari.
Sasa wewe ni mwandishi wa habari? mwandishi wa makala? au chambio la mafisadi?.
JMushi,
Kuna mwandishi wa habari alikamatwa na kufikishwa kwa Idi Amin. Aliamini kuwa ungekuwa ni mwisho wake. Idi Amin alitamka na kumwuliza mwandishi yule swali moja tu; " Nyinyi waandishi wa habari mnaandika mambo mengi mbaya kuhusu mimi. Sasa nikuulize kijana, hivi katika yote ninayoongea na ninayoyafanya hakuna hata moja lililo zuri?" Mwandishi yule akajibu; " Yapo mengi Mkuu".
Idi Amin akatamka; " Basi, nenda kaandike moja tu lililo zuri kuhusu mimi!" Tafakari.
Ningependelea ujibu hoja kutokana na yale niliyoyajibu kwenye makala yako,nimezungumzia zile ulizoziita "Dhaifu" na nikakuelezea ni kwanini si dhaifu...So unijibu ni kivipi sababu zangu nilizozitoa hazimake sense dhidi ya hizo dhaifu ulizozimention,nime analyze moja baada ya nyingine,na kama bado unaamini kuwa dhaifu zako bado zina make sense,then weka wazi why,sidhani kama ni tatizo kubwa kwa mtu ambaye ni mwandishi.
Mjengwa mbona hukutuambia ulichokiona uwanja wa Sanora alipotembelea JK na pia kutoa uchambuzi wa strengths na weaknesses zake. Bado inaonekana unaogelea kwenye dimbwi la kutaka kutuaminisha CCM na JK are perfect na wengine ni wakulinganishwa.
Maggid kama unaona unachoandika ni fikra zako shida ya nini kujibu mmoja baada ya mwingine endelea kuandika fikra zako. Acheni kuipotosha jamii kwa kujifanya mnaandika kisomi. Mbona viongozi wengine wa upinzani hutoi tathmini zao umeona Chadema tu.. Kweli you are finishing and firing yourself out. Wewe endelea kutuandikia habari za chai na chapati haya mengine waachie wenyewe.
Mushi mdogo wangu,
Ndio maana ya demokrasia hiyo. Na wewe umesomea mambo hayo mpaka Ulaya . Hatuwezi kukubaliana kwa kila kitu. Katika uliyoyaandika kuna nayokubaliana nawe, mengine hapana. Katika maisha, hata ya kisiasa kuna kutokubaliana. Wakati mwingine tuwaachie wengine wasome na waamue. Hayo unayosema wewe kuwa hayana maana, kuna watu wa CHADEMA wamenipigia simu kunishukuru. Hao nao wanatofautiana na wewe hata kama mko chama kimoja. Na katika diplomasia husemwa; "tumekubaliana kutokubaliana". Naomba mdogo wangu tukubaliane kwa hilo.
Wewe tushakuzoea pro-CCM? Analysis zako hazina mashiko
Makala za Maggid hazina mvuto kama vile za Bagenda, tatizo lake anaandika vitu vilivyo nje ya uwezo wake. Hajui uchambuzi wa kisayansi na kisomi nadhani yeye angefaa zaidi kuwa mpiga picha au angalau ripota lakini sio mchambuzi. Uwezo wake wa kuchanganua mambo sio mkubwa. Hata ukiangalia milinganisho (analogy) yake zake katika makala zake kunakuwa hakuna mlingano. (makala zake huunza na kisa kisha hujaribu kujenga hoja juu ya hicho kisa) lakini ajabu kunakuwa hakuna ulinganifu kabisa.
Jikombe sana kwa CCM , unaweza kuambulia kuziba nafasi ya Nape pale Lumumba
Yah,tatizo lake ni elimu.Kuna tofauti kati ya analysis ya Simba na Yanga na analysis ya ishu nzito kama hii ya namna Dkt Slaa anavyojiandaa kuingia Ikulu.Mjengwa,unajitahidi kuficha u-Kikwete wako kwa kujidai eti kuongelea "mazuri" ya Dkt Slaa!Mbona hujawahi kufanya analysis kumhusu Kikwete na kujumuisha weaknesses zake?Mjengwa na rafiki yake Michuzi ni waganga njaa wa CCM ; huku kujidai anafanya analysisi ya Slaa ni kujibaraguza tu!! Level ya education yake haimruhusu kuweza kuelewa Dr. Slaa anafafanua nini!! He is just a bogus blogger.
zakwako zenye mvuto na zilizo ndani ya uwezo wako ziko wapi tuzisome? uchambuzi wako wa kisayansi na kisomi uko wapi ndugu nikazisome? labda mwenzetu unauwezo wa kuchanganua mambo na labda makala zako ni more analogy!!! tafadhali naomba nisome makala zako ili niweze kuzilinganisha na za Majjid kwani unaonesha wewe ni mahiri zaidi ili tunufaike na uchambuzi wako!! usiandike kwa mate na hali wino upo!!!
Ah,kujiunga leo na leo na kushikia bango la utetezi?Mapacha wa Mjengwa au Mjengwa mwenyewe?
Haihitaji jambo baya la pili kuthibitisha ubaya wa la kwanza.Haihitaji makala "za akili" ili kutambua mapungufu ya za Mjengwa.Kwani,kwa mfano,ni lazima kuwe na ugonjwa mwingine ili jamii iweze kufahamu ubaya wa ukimwi?
Wewe mwenye akili nyepesi unaweza kumtaka kila anayemkosoa Mjengwa nae aandike ili nae aweze kuchambuliwa.Unachosahau hapa ni ukweli kuwa si kila mtu ana kimbelembele kama cha Mjengwa.Ndio.Kuna chambuzi za kutumwa (kama huko Daily News) na hizi za kujipendekeza kwa mafisadi zinazoandikwa na akina Mjengwa.
Kabla hujakurupuka kusifia uchambuzi huu ni vema ukarejea chambuzi zilizopita ili uweze kufahamu ubabaishaji na unafiki wa Mjengwa.Kwa mfano,kwanini uchambuzi wake hapa ni sifa na mapungufu ya Dkt Slaa na Chadema lakini ikija ishu ya Kikwete na CCM inakuwa sifa zaidi ya sifa kaa Kikwete,mkewe na mtoto wao Riziwani,no mapungufu then kwa kujikosha mapungufu yatakayozungumziwa na Mjengwa ni ya CCM na sio Kikwete.
TAFUTA MAHALA POPOTE PALE AMBAPO MJENGWA AMEWAHI KUMKOSOA KIKWETE kisha tuwekee hapa (na simaanishi "expert analyses zake za uchaguzi " pekee BALI MAKALA YOYOTE ILIYOWAHI KUANDIKWA NA MJENGWA.
TAFUTA MAHALA POPOTE PALE AMBAPO MJENGWA AMEWAHI KUMKOSOA KIKWETE kisha tuwekee hapa (na simaanishi "expert analyses zake za uchaguzi " pekee BALI MAKALA YOYOTE ILIYOWAHI KUANDIKWA NA MJENGWA.