Ah,kujiunga leo na leo na kushikia bango la utetezi?Mapacha wa Mjengwa au Mjengwa mwenyewe?
Haihitaji jambo baya la pili kuthibitisha ubaya wa la kwanza.Haihitaji makala "za akili" ili kutambua mapungufu ya za Mjengwa.Kwani,kwa mfano,ni lazima kuwe na ugonjwa mwingine ili jamii iweze kufahamu ubaya wa ukimwi?
Wewe mwenye akili nyepesi unaweza kumtaka kila anayemkosoa Mjengwa nae aandike ili nae aweze kuchambuliwa.Unachosahau hapa ni ukweli kuwa si kila mtu ana kimbelembele kama cha Mjengwa.Ndio.Kuna chambuzi za kutumwa (kama huko Daily News) na hizi za kujipendekeza kwa mafisadi zinazoandikwa na akina Mjengwa.
Kabla hujakurupuka kusifia uchambuzi huu ni vema ukarejea chambuzi zilizopita ili uweze kufahamu ubabaishaji na unafiki wa Mjengwa.Kwa mfano,kwanini uchambuzi wake hapa ni sifa na mapungufu ya Dkt Slaa na Chadema lakini ikija ishu ya Kikwete na CCM inakuwa sifa zaidi ya sifa kaa Kikwete,mkewe na mtoto wao Riziwani,no mapungufu then kwa kujikosha mapungufu yatakayozungumziwa na Mjengwa ni ya CCM na sio Kikwete.
TAFUTA MAHALA POPOTE PALE AMBAPO MJENGWA AMEWAHI KUMKOSOA KIKWETE kisha tuwekee hapa (na simaanishi "expert analyses zake za uchaguzi " pekee BALI MAKALA YOYOTE ILIYOWAHI KUANDIKWA NA MJENGWA.