Elections 2010 Kilichonishtua Juu Ya Dr Slaa Pale Mwembetogwa

Elections 2010 Kilichonishtua Juu Ya Dr Slaa Pale Mwembetogwa

Kuna kosa gani kuwa biased?

Kuna wanaopenda Kikwete, wako Biased kwake! Kuna wanaopenda Slaa, wako biased kwake, kuna wanaopenda Lipumba, na wanasiasa wengine. Ka kutake side ni unafiki, basi nawe umo kwenye hilo kundi la wanafiki alilomo Maggid:argue:

Lets Behave as great thinkers Bana. This is not The correct argument on Bias.

Take These two Statements.
1.Makamba ni bias kwa CCM
2.NEC ni bias kwa CCM
Umeona utofauti wa hizo sentesi mbili?

Maggid anajipresent kama mwandishi ambaye hakutakiwa kegemea upande wowote. Hapo tunahaki ya kusema yeye ni Bias kwasababu anaegemea upande mmoja.
Angejiweka kama kina MS and Co no one could have term him as Bias, But a CCM supporter!! umeelewa lakini?
 
bw Majjid, Kwanini usianzishe mada yenye kichwa cha habari CCM ya Kikwete haijatutendea haki watanzania au "kilichoniogopesha ktk kipindi cha miaka mitano ya uongozi wa JK" wewe kama mzazi na mshabiki wa CCM hijisikii vibaya kuona jamii yako inaangamia kwa umaskini ilhali wachache ndo wanawekeza vijicent ndani na nje ya TZ? ... ndugu yangu kama umelogwa basi aliekuloga amesha kufa...
 
"Hili ningelisema kama nilivyolisema hata kama lingefanywa na Kikwete wa CCM, Lipumba wa CUF au mgombea ye yote yule."

Maggid, wewe ni MNAFIKI
Umeamua kumwandama Slaa kwa sababu zako mwenyewe na unataka kuwaaminisha watu kuwa una nia nzuri! Huo ni UNAFIKI. Nimechukizwa, siyo na wewe personally, bali na tabia yako ya kujifanya mkweli wakati siyo.

Acha hizo, Get REAL.
Hutakiwi kusema lolote la udhaifu kuhusu Slaa wewe ni Mnafiki....na hii ndiyo tathmini ya great thinker!
 
Dear Mjengwa, kwani unadeni gani mbona unatulazimisha? can you shut up cause some of us do not want to put up with whatever you think. Its not important to us, sawa? na hatuna muda wa kupoteza hayo mashairi yako kwa nini usiyatumie kwenye gazeti lako jipya la njombe jamii? not good enough for great thinkers
 
Dr Slaa ndio aina ya kiongozi tunayemtaka katika nchi kama Tanzania kwa sasa kwani ni nchi inayo-lack seriousness katika kila jambo, na kulindana kwa maslahi binafsi (mwenzetu-syndrome). Tunataka kiongozi anayeweza kuita spade kuwa ni spade na sio kijiko kikubwa. Go Slaa... go...
 
hapa ndio unaona ni kitu gani kiongozi sahihi na mwenye akili timamu gani anatakiwa kufanya baada ya kupata habari na kuzifanyia kazi, hakuna mambo ya siri sote tunastahili na tuna haki ya kufahamu kinachoendelea.
hiki ni kitu chema sana alichofanya Dr. Silaa, na anastahili pongezi, na akipata fursa ya kuwa Rais wa nchi hii na akaze mwendo huohuo, hatuitaji viongozi wala rushwa na watu kama hawa wanastahili sio tu kusemwa adharani badli kuchukuliwa hatua kali.
kwa namna hii, hii nchi itafika mahali fulani na maendeleao yataonekana kwa watanzania wote na sio watu wachache wenye maslahi binafsi.
 
Ama,
Nadhani hujanielewa hoja yangu kuhusu Maggid. Anajifanya kuwa mkweli kuhusu Dr Slaa, na anataka watu waamini hivyo, wakati siyo mkweli. Hiyo ni hypocrisy. Anajifanya kumpa Dr ushauri kama kwa nia njema, wakati siyo kweli.
Mimi sina tatizo na mtu kuchagua upande, iwe ccm, chadema, cuf, au chama kingine chochote. Tatizo langu ni pale mtu anapoamua kuwa MNAFIKI.
Unaweza kuamua kuniita mi mnafiki, kwa kuwa umeamua hivyo, lakini mimi siyo mnafiki kwa hali yoyote. Kama nina upande niliochagua, kama wewe unavyodhani, sijiviki manyoya ya kondoo na kutaka kuwaaminisha wale wa upande mwingine (ambao sikuuchagua) kwamba ninawatakia mema. Unafiki wangu uko wapi hapo? Unless hujui maana ya neno unafiki.
 
Dk. Slaa amepata kufichua hadharani makubwa zaidi, yaliyowahusu wakubwa zaidi pale Mwembe Yanga mwaka wa 2007. WanaJF watakumbuka kwamba Dk. Slaa aliwataka wale aliowataja waende mahakamani, ambapo angeleta ushahidi kuthibitisha matamshi yake. Hakuna hata mmoja aliyethubutu kufanya hivyo. Wengi wao wanapeta mitaani, na bila aibu baadhi yao wanataka sasa Watanzania wawachague kuendelea na uongozi! Shame on us Tanzanians if we give in to these mafisadi!!!

Tunataka viongozi jasiri kama Dk. Slaa ambao wako tayari kutoa facts and figures kuthibitisha maovu yanayotendwa Serikalini na katika mashirika ya umma. Juzi tu, amemkemea Jenerali Abdulrahmani Shimbo kwa kutishia wananchi eti JWTZ wako tayari kuhakikisha wananchi wanakubali "matokeo" ya Uchaguzi wa Oktoba 31. JWTZ wamepanga "matokeo" gani?

Tamko kama hili lingetolewa na Jaji Lewis Makame, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (NEC). Jaji Makame angesema kwamba Tume yake itahakikisha kila mwananchi aliyejiandikisha atakuwa huru kupiga kura, bila kuhongwa au kutishwa, na kwamba uhesabuji utaendeshwa bila interference toka chama chochote: Kwa hiyo wananchi wakubali matokeo, tungeweza kuona hilo ni tamko stahiki. Lakini JWTZ au Polisi hawana jukumu hilo.

Kuhusu Dk. Slaa na tamko lake kuhusu huyu MwanaChadema aliyehongwa, sisi wanaChadema tumejijengea utamaduni wa kusema kwa uwazi. Hata huko Bungeni waBunge wetu, wakiongozwa na Dk. Slaa hawakusita kufichua maovu yanayotendwa na viongozi. Tukitaka Bunge lidhibiti mwenendo wa Serikali, kama Katiba inavyotaka, ni lazima tuwe wawazi. Tufichue yale yote yanayokwamisha maendeleo yetu, hasa ubadhirifu na wizi wa fedha za umma. Tufichue ufisadi unaodhoofisha miradi ya maendeleo.

Tumefaidika kutokana na juhudi za Dk. Slaa, Mhe. Zitto Kabwe na Wabunge wengine wa Chadema, na tunataka mtindo huu uendelee. Uchaguzi huu utupe fursa ya kupata Rais na wabunge wazalendo wa kweli, waadilifu, wasiosita kudhibiti viongozi mafisadi ua wabadhirifu, wenye huruma na wanyonge.

Hao ndio Dk. Slaa na timu yake.
 
Ndugu Zangu,

Nimeona mada niliyoianzisha kwenye mjengwablog imeingizwa humu na wengi wameshiriki kuichangia, na mimi pia. Mada inasema " Nilichokiona Jana pale Mwembetogwa". Lakini ziada ya pale Mwembetogwa ni ukweli kuwa mwanzoni kabisa mwa hotuba yake, Dr Slaa alitoa kauli mbele ya umati ule. Kauli ambayo binafsi niliisikia na ilinishtua sana. Dr Slaa alisikika akitamka kuwa kuna kiongozi wa mkoa ( CHADEMA) ( Alimtaja jina) ambaye amehongwa na mgombea ubunge wa CCM jimbo lingine la Iringa ( naye alimtaja jina) ili asirudishe fomu zake. Dr Slaa akataka kiongozi huyo wa zamani wa CHADEMA apuuzwe na akitaka aende mahakamani.

Nadhani katika wakati huu kuna umuhimu wa kuwafahamu zaidi wagombea wetu. Na kumtakia mema Dr Slaa ni pamoja na kumwambia yale tunayoyaona ni mapungufu. Si kummwagia sifa tu. Maana, kwa kitendo kile, Dr Slaa kwa mtazamo wangu alimdhalilisha kiongozi yule wa CHADEMA mbele ya umati ule. Na bahati mbaya au nzuri kiongozi huyo wa CHADEMA alikuwapo. Kwa macho yangu nilimwona kiongozi huyo wa CHADEMA akishiriki kupiga makofi kuungana na umati uliokuwa ukishangilia kauli ya Dr Slaa. Masikini, kiongozi yule wa CHADEMA, bila shaka alipigwa na butwaa na hakuwa na la kufanya bali naye kupiga makofi!

Kwangu nilishtushwa na kusikitishwa sana. Bado naamini Dr Slaa hakumtendea haki kiongozi yule wa CHADEMA. Kama Dr Slaa alikuwa na ushahidi wa alichokisema, basi, hakuwa na haja ya kumtuhumu na kumtolea hukumu kiongozi yule pale hadharani. Kiongozi yule wa CHADEMA aliyehukumiwa hadharani ni mwanajamii hapa Iringa. Ameshapigwa mhuri mbaya bila hata kupewa fursa ya kujitetea. Kwa mzazi kama mimi naelewa jinsi kiongozi yule atakavyojisikia vibaya mbele ya familia yake, mke na watoto wake. Kwamba ametoka kwenye mkutano wa mgombea urais huku yeye akitajwa hadharani kuwa amehongwa asirudishe fomu.

CHADEMA wana vikao vyao, kwa kutanguliza busara wangeyamaliza ya kwao kwenye vikao vyao vya ndani, si hadharani. Na kama mgombea Urais, Dr Slaa anapaswa awe mfano wa kuheshimu utawala wa sheria. Hili ningelisema kama nilivyolisema hata kama lingefanywa na Kikwete wa CCM, Lipumba wa CUF au mgombea ye yote yule. Nisingelisikia nikalinyamazia. Kuandika ni kushauri pia. Tusingependa Dr Slaa apitishwe njia ya Mrema, ina miba na matope. Anayesoma na kuhusika na kilichoandikwa ana uhuru wa kupokea ushauri na kuufanyia kazi au kuachana nao. Nimechokoza mjadala....

Maggid,
Iringa.
Shekhe wangu MAggid,
Kumtaja MHALIFU siyo kumhukumu.
Hakuna mahala kwenye sheria panaposema kwamba kumtaja mhalifu unakuwa umetenda kosa. Ila kama umemepeleka mbele ya sheria na ikajuulikana si mhalifu hapo anaruhusiwa kusafisha jina lake dhidi yako uliyemshtaki.

Amini nakuambia kwamba Dr. Slaa hakurupuki. Ni mgombea mwerevu kuliko wa kwako.
 
CHADEMA Inachora mstari kati ya Ukweli na Uongo, Uadilifu na Ubadhirifu, Mtu Msaliti nivyema Jamii ikamtambua ili kipindi kingine asipewe Dhamana

After all huyo Jamaa alishasimamishwa Uongozi kwa Hiyo kuendelea kumuita Kiongozi unaonesha aina nyingine ya Ubabaishaji na kukosa umakini
 
Maggid ungepaswa kushtushwa na Taarifa kwamba kuna Graduate wa Mlimani Baba yake ni Rais anamiliki Magorofa Matatu, hizo ndizo habari ulizopaswa kushtushwa nazo
 
Maggid ungepaswa kushtushwa na Taarifa kwamba kuna Graduate wa Mlimani Baba yake ni Rais anamiliki Magorofa Matatu, hizo ndizo habari ulizopaswa kushtushwa nazo
Hivi kuna watu bado wanazichukulia seriously makala za huyu 'Mjenga'?
 
Japo yaonekana hili ni jambo jema nadhani uchaguzi tuliochiwa ni kuyakubali maneno yanayodaiwa kusemwa na Dr. Slaa kama yanavyoripotiwa na Maggid. Hata hivyo, ndugu yetu Maggid hatupi hasa maneno aliyoyasema Dr. Slaa yalikuwa yapi hasa kwani alichotupatia ni kile ambacho yeye anaweza kuwa amekitafsiri kuwa kimesemwa. Kwa mwalimu makini kama yeye nina uhakika ana uwezo kabisa wa kuwa ameyarekodi maneno yale ya Dr. Slaa na angetusaidia kuyaweka hapa ili kila mtu asikilize ni nini HASA KILISEMWA hadi kumfanya mtu anayedaiwa kutajwa naye kupiga makofi!

Vinginevyo sijaona msingi wowote wa kusema mtu kadhalilishwa au Dr. Slaa hakutenda haki. Maana kumbukumbu zangu zinanionesha kuwna viongozi kadhaa ndani ya chama tawala ambao wamewatimua watu na kuwatia viboko hadharani na wengine kuwachapa vibao!
 
Japo yaonekana hili ni jambo jema nadhani uchaguzi tuliochiwa ni kuyakubali maneno yanayodaiwa kusemwa na Dr. Slaa kama yanavyoripotiwa na Maggid. Hata hivyo, ndugu yetu Maggid hatupi hasa maneno aliyoyasema Dr. Slaa yalikuwa yapi hasa kwani alichotupatia ni kile ambacho yeye anaweza kuwa amekitafsiri kuwa kimesemwa. Kwa mwalimu makini kama yeye nina uhakika ana uwezo kabisa wa kuwa ameyarekodi maneno yale ya Dr. Slaa na angetusaidia kuyaweka hapa ili kila mtu asikilize ni nini HASA KILISEMWA hadi kumfanya mtu anayedaiwa kutajwa naye kupiga makofi! !

I wish na haya yangeulizwa kwa wale wanaoripoti ama kutoa maoni kuhusu yanayodaiwa kusemwa na wengine pia......
 
Let us have a commercial Break Bana ya kilichojiri huko Mbeya, na hapo ni Uyole nasikia

Photo0051.jpg
 
Mpenda chongo, chongo huita kengeza. Kama Dr. Slaa alifanya anayoshutumiwa basi hakumtendea haki kiongozi MWENZIE!

Amandla........
 
Wewe Maggid, usifikiri Watanzania ni Mabwege; Wewe endelea na ndoa yako na hao jamaa, hizo pesa wanazokupa utakuja Kujuta nazo
 
Dk. Slaa amepata kufichua hadharani makubwa zaidi, yaliyowahusu wakubwa zaidi pale Mwembe Yanga mwaka wa 2007. WanaJF watakumbuka kwamba Dk. Slaa aliwataka wale aliowataja waende mahakamani, ambapo angeleta ushahidi kuthibitisha matamshi yake. Hakuna hata mmoja aliyethubutu kufanya hivyo. Wengi wao wanapeta mitaani, na bila aibu baadhi yao wanataka sasa Watanzania wawachague kuendelea na uongozi! Shame on us Tanzanians if we give in to these mafisadi!!!

Tunataka viongozi jasiri kama Dk. Slaa ambao wako tayari kutoa facts and figures kuthibitisha maovu yanayotendwa Serikalini na katika mashirika ya umma. Juzi tu, amemkemea Jenerali Abdulrahmani Shimbo kwa kutishia wananchi eti JWTZ wako tayari kuhakikisha wananchi wanakubali "matokeo" ya Uchaguzi wa Oktoba 31. JWTZ wamepanga "matokeo" gani? .

Angalia upotoshaji huu....nilidhani alisema kuwa hawataruhusu na hakuna atakayemwaga damu....Hivi aliongelea kitu chochote kuhusiana na kuhakikisha kuwa wanakubali matokeo?????
 
Back
Top Bottom