Elections 2010 Kilichonishtua Juu Ya Dr Slaa Pale Mwembetogwa

  1. Chadema siku zote hawana siri wala kumsubili mtu aje kujitetea.
  2. Chadema huwa wawazi kwa kila jambo ndo maana tumekuwa na mafanikio
  3. chadema hatuna cha huyu mkubwa wala mdogo unapewa palepale makosa yako
  4. chadema huwa haiogopi mtu wa aina yoyote kama unabishaa muulize kikwete mwenyewe au Shimbo​
 
Omarilyas,
Hii ndio tunapigia kelele hapa. Kama unawafahamu watu hapa na una hakika si taja kwa majina? Huu ndio ujasiri wa hapa JF "dare to talk openly"Lakini naona unaturudisha kwa Maggid huko huko.
Just talk. Sema ni fulani na fulani!

I am sure u r not ready for that............its big and very disappointing in all aspects..connect the dots
 
OMG!
Maggid what have you done sasa?
kuna hoja nyingi hapa hutaki kuzijibu ilihali umeanzisha mjadala.
ntaomba nikutukane tena ohoooo!!!!!
 
Maggid yuko kimyaaaaaaaaa!!!!!!!!!! najua yupo hapa JF anasoma michango yenu Kimyaaaaaaaaaaa na anaweza asiseme kitu kabisaaaaaaaaaa maana anajua hila zake ziko nje

Ama anaanda makala nyingine moto zaidi..............
 
What if wapenzi wa Dr Slaa wangemvaa na kumrarua mtuhumiwa huyo.....bado tungeendelea ndoto za Utawala bora kutoka kwake???? ust thinking loudly........As a duty for critical citizenry..

Walau katika kupandisha kwangu kutoka Jangwani nikiwa peke yangu nimemsikia huyu aliyethubutu kufikiri kwa sauti katika umati unaoelekea Jangwani.
 
Ndugu Zangu,

Nimeona mada niliyoianzisha kwenye mjengwablog imeingizwa humu na wengi wameshiriki kuichangia, na mimi pia. Mada inasema " Nilichokiona Jana pale Mwembetogwa". Lakini ziada ya pale Mwembetogwa ni ukweli kuwa mwanzoni kabisa mwa hotuba yake, Dr Slaa alitoa kauli mbele ya umati ule. Kauli ambayo binafsi niliisikia na ilinishtua sana. Dr Slaa alisikika akitamka kuwa kuna kiongozi wa mkoa ( CHADEMA) ( Alimtaja jina) ambaye amehongwa na mgombea ubunge wa CCM jimbo lingine la Iringa ( naye alimtaja jina) ili asirudishe fomu zake. Dr Slaa akataka kiongozi huyo wa zamani wa CHADEMA apuuzwe na akitaka aende mahakamani.

Nadhani katika wakati huu kuna umuhimu wa kuwafahamu zaidi wagombea wetu. Na kumtakia mema Dr Slaa ni pamoja na kumwambia yale tunayoyaona ni mapungufu. Si kummwagia sifa tu. Maana, kwa kitendo kile, Dr Slaa kwa mtazamo wangu alimdhalilisha kiongozi yule wa CHADEMA mbele ya umati ule. Na bahati mbaya au nzuri kiongozi huyo wa CHADEMA alikuwapo. Kwa macho yangu nilimwona kiongozi huyo wa CHADEMA akishiriki kupiga makofi kuungana na umati uliokuwa ukishangilia kauli ya Dr Slaa. Masikini, kiongozi yule wa CHADEMA, bila shaka alipigwa na butwaa na hakuwa na la kufanya bali naye kupiga makofi!

Kwangu nilishtushwa na kusikitishwa sana. Bado naamini Dr Slaa hakumtendea haki kiongozi yule wa CHADEMA. Kama Dr Slaa alikuwa na ushahidi wa alichokisema, basi, hakuwa na haja ya kumtuhumu na kumtolea hukumu kiongozi yule pale hadharani. Kiongozi yule wa CHADEMA aliyehukumiwa hadharani ni mwanajamii hapa Iringa. Ameshapigwa mhuri mbaya bila hata kupewa fursa ya kujitetea. Kwa mzazi kama mimi naelewa jinsi kiongozi yule atakavyojisikia vibaya mbele ya familia yake, mke na watoto wake. Kwamba ametoka kwenye mkutano wa mgombea urais huku yeye akitajwa hadharani kuwa amehongwa asirudishe fomu.

CHADEMA wana vikao vyao, kwa kutanguliza busara wangeyamaliza ya kwao kwenye vikao vyao vya ndani, si hadharani. Na kama mgombea Urais, Dr Slaa anapaswa awe mfano wa kuheshimu utawala wa sheria. Hili ningelisema kama nilivyolisema hata kama lingefanywa na Kikwete wa CCM, Lipumba wa CUF au mgombea ye yote yule. Nisingelisikia nikalinyamazia. Kuandika ni kushauri pia. Tusingependa Dr Slaa apitishwe njia ya Mrema, ina miba na matope. Anayesoma na kuhusika na kilichoandikwa ana uhuru wa kupokea ushauri na kuufanyia kazi au kuachana nao. Nimechokoza mjadala....

Maggid,
Iringa.

Hapo kenye red....Hizo ndizo siasa za CCM zilizopitwa na wakati. Ndiyo maana watu wanakuwa recycled all the years, ikifanya kosa hapa anapelekwa kule ajilekebishe kisha kesho anapewa utamu zaidi!!!
 
Mara kwa mkuu wa wilaya....PANDA JUU YA JUKWAA!
Mara kwa mkuu wa majeshi...NAKUPA SIKU SABA UOMBE RADHI!
Sasa leo munampongeza kwa kumdhalilisha mtu hadharani baada ya kupora mke wa watu.

Huyu jamaa hafai kabisa na haambiliki.Mumemuandaa vyema lakini si chaguo jema. Kwa mtindo huu wangapi watachomwa moto kwa kudhaniwa ni wezi,wangapi wataozea gerezani kwa kudhaniwa magaidi!.
Eee! Mungu (Allah).Pitisha hukumu yako huyu mbakaji asiingize mguu wake pale ikulu.
 
ukamwambie na shehe yahaya aongeze sara zake pia!
 
Ndugu Zangu,

Nimeona mada niliyoianzisha kwenye mjengwablog imeingizwa humu na wengi wameshiriki kuichangia, na mimi pia. Mada inasema " Nilichokiona Jana pale Mwembetogwa". Lakini ziada ya pale Mwembetogwa ni ukweli kuwa mwanzoni kabisa mwa hotuba yake, Dr Slaa alitoa kauli mbele ya umati ule. Kauli ambayo binafsi niliisikia na ilinishtua sana. Dr Slaa alisikika akitamka kuwa kuna kiongozi wa mkoa ( CHADEMA) ( Alimtaja jina) ambaye amehongwa na mgombea ubunge wa CCM jimbo lingine la Iringa ( naye alimtaja jina) ili asirudishe fomu zake. Dr Slaa akataka kiongozi huyo wa zamani wa CHADEMA apuuzwe na akitaka aende mahakamani.

Nadhani katika wakati huu kuna umuhimu wa kuwafahamu zaidi wagombea wetu. Na kumtakia mema Dr Slaa ni pamoja na kumwambia yale tunayoyaona ni mapungufu. Si kummwagia sifa tu. Maana, kwa kitendo kile, Dr Slaa kwa mtazamo wangu alimdhalilisha kiongozi yule wa CHADEMA mbele ya umati ule. Na bahati mbaya au nzuri kiongozi huyo wa CHADEMA alikuwapo. Kwa macho yangu nilimwona kiongozi huyo wa CHADEMA akishiriki kupiga makofi kuungana na umati uliokuwa ukishangilia kauli ya Dr Slaa. Masikini, kiongozi yule wa CHADEMA, bila shaka alipigwa na butwaa na hakuwa na la kufanya bali naye kupiga makofi!

Kwangu nilishtushwa na kusikitishwa sana. Bado naamini Dr Slaa hakumtendea haki kiongozi yule wa CHADEMA. Kama Dr Slaa alikuwa na ushahidi wa alichokisema, basi, hakuwa na haja ya kumtuhumu na kumtolea hukumu kiongozi yule pale hadharani. Kiongozi yule wa CHADEMA aliyehukumiwa hadharani ni mwanajamii hapa Iringa. Ameshapigwa mhuri mbaya bila hata kupewa fursa ya kujitetea. Kwa mzazi kama mimi naelewa jinsi kiongozi yule atakavyojisikia vibaya mbele ya familia yake, mke na watoto wake. Kwamba ametoka kwenye mkutano wa mgombea urais huku yeye akitajwa hadharani kuwa amehongwa asirudishe fomu.

CHADEMA wana vikao vyao, kwa kutanguliza busara wangeyamaliza ya kwao kwenye vikao vyao vya ndani, si hadharani. Na kama mgombea Urais, Dr Slaa anapaswa awe mfano wa kuheshimu utawala wa sheria. Hili ningelisema kama nilivyolisema hata kama lingefanywa na Kikwete wa CCM, Lipumba wa CUF au mgombea ye yote yule. Nisingelisikia nikalinyamazia. Kuandika ni kushauri pia. Tusingependa Dr Slaa apitishwe njia ya Mrema, ina miba na matope. Anayesoma na kuhusika na kilichoandikwa ana uhuru wa kupokea ushauri na kuufanyia kazi au kuachana nao. Nimechokoza mjadala....

Maggid,
Iringa.

Mjengwa, makosa na changamoto za kisiasa hutatuliwa kisiasa, tena hadharani. Vinginevyo itakuwa ni kuruhusu rumours kutawala, na huo ndio utakuwa mwisho wa political grouping yako.
Dr. Silaa alikuwa sahihi kutoa tamko lake hadharani.
 
Sasa bwana Maggid ulitaka huyo kiongozi asifiwe kama anavyofanya Kikwete kuwasifia mafisadi majukwaani huku raia wakibaki wanaulizana kulikoni?
Sikutaraji kama Kikwete angeweza kumsifia mtu kama Chenge au Lowassa! Huu ndiyo unafiki tusioutaka tunataka uongozi kama wa Slaa, tunakupa za uso papo hapo!
Maggid vipi bwana, kijana mdogo unaleta sera za kizamani za kufichana?
 
What if wapenzi wa Dr Slaa wangemvaa na kumrarua mtuhumiwa huyo.....bado tungeendelea ndoto za Utawala bora kutoka kwake???? ust thinking loudly........As a duty for critical citizenry..

Hatupo kwenye ulimwengu huo wa masumbwi mkuu, huku ni sera za ukweli na uwazi. Ndiyo maana pamoja na yote hayo sijasikia kama kuna mtu kamgusa au kumnyanyasa.
Hiyo ndiyo aina ya siasa tunayoihitaji Tanzania hii
 
What if wapenzi wa Dr Slaa wangemvaa na kumrarua mtuhumiwa huyo.....bado tungeendelea ndoto za Utawala bora kutoka kwake???? ust thinking loudly........As a duty for critical citizenry..

What if......!!! Didn't happen my bro...... What was he doing there anyway. If he was smart upstairs.................I think he shouldn't have been there!!!
 
Mara kwa mkuu wa wilaya....PANDA JUU YA JUKWAA!
Mara kwa mkuu wa majeshi...NAKUPA SIKU SABA UOMBE RADHI!
Sasa leo munampongeza kwa kumdhalilisha mtu hadharani baada ya kupora mke wa watu.

Huyu jamaa hafai kabisa na haambiliki.Mumemuandaa vyema lakini si chaguo jema. Kwa mtindo huu wangapi watachomwa moto kwa kudhaniwa ni wezi,wangapi wataozea gerezani kwa kudhaniwa magaidi!.
Eee! Mungu (Allah).Pitisha hukumu yako huyu mbakaji asiingize mguu wake pale ikulu.
Aaamin!.
 
What if......!!! Didn't happen my bro...... What was he doing there anyway. If he was smart upstairs.................I think he shouldn't have been there!!!

Isn't leaders' duty to be responsible and critically measure his or her public utterance ???
 
na maggid mjengwa,

iringa ni ngome ya ccm. Jana jioni dr slaa alitua iringa na kuvuta umati mkubwa wa watu. Nilikuwapo pale viwanja vya mwembetogwa. Nini aliongea na kina nini ndani yake, nitachambua hapa kwa ufupi;
nilifika viwanja vya mwembetogwa saa kumi na robo jioni. Tayari dr slaa alishatua. Watu walikuwa wengi sana. Pamoja na uzoefu wangu wote wa kujipenyeza kwenye kundi la watu nikiwa na kamera, bado kwangu safari hii ilishindikana. Niliishia kutafuta sehemu ya juu kidogo nyuma ili walau nipate picha ya dr slaa akihutubia. (picha ya kwanza hapo juu blogiini imepigwa na francis godwin.)

nimekaa iringa tangu mwaka 2004 na nimeudhuria mikutano yote ya kampeni za urais kuanzia jakaya kikwete, mbowe, lipumba hadi mrema, lakini niweke wazi. Mkutano wa jana pale viwanja vya mwembetogwa umevunja rekodi zote katika kujaza watu kwa mujibu wa kumbukumbu zangu za tangu 2004. Katika chaguzi ziliopita kuna watumishi wa serikali waliokuwa wakienda kwenye mikutano ya vyama vya upinzani kwa kunyata. Walikuwa na hofu ya kuonekana wanaunga mkono upinzani na kuonekana kwao kwenye mikutano ya akina mbowe, zitto na lipumba ingetafsiriwa kuwa hawaipigii kura ccm. Jana kulikuwa na watu wa aina zote, hata makada wa ccm walifika pia.

Kwenye hotuba yake ya takribani dakika 43 dr slaa alijikita katika maeneo makubwa matatu;
uchaguzi wenyewe; alianza kwa shambulizi dhidi ya mnadhimu mkuu wa majeshi ( jwtz) na polisi kwa tamko lao juu ya uchaguzi. Dr slaa naye akasema ametoa tamko lake akiwa njombe kushutumu hatua hiyo ya jeshi na polisi akisema kuwa ni kuwatisha wapiga kura.

Dr slaa akagusia pia masuala ya elimu akisisitiza azma ya chadema kutoka elimu bure kuanzia chekechea. Katika eneo hili dr slaa alifanikiwa pia ( kisiasa) kukwepa kutoa ufafanuzi wa ni kwa namna gani. Kuna mahali alifanikiwa sana alipojaribu kulinganisha na wakati wake alipokuwa shuleni na hali ilivyo sasa.

” ndugu zangu, leo mtoto anakwenda shule anaambiwa abebe na ndoo!” alisema dr slaa. Niliwasikia wasikilizaji wakimalizia na ” mafagio, makwanja…”

hapo dr slaa aliweza kupenya kwenye kero na matatizo ya kila siku ya wapiga kura. Na ni mambo haya ambayo wapiga kura wanayaelewa zaidi kuliko kashfa za epa, iptl, deep green na nyinginezo ambazo akina dr slaa na wanasiasa wengine wameshindwa kuziweka katika lugha nyepesi ikamfanya mpiga kura wa kihesa awaelewe. Mpiga kura ambaye bado anaumiza kichwa kila siku kutafuta senti za kununulia mafuta ya taa na michango ya madawati ya watoto wake.

Dr slaa aligusia kwa kirefu pia suala la uchumi na namna serikali yake itakavyohakikisha tanzania inanufaika na rasilimali zake. Kuna wakati kwenye hotuba yake alijichanganya kido aliposema wachagueni wabunge wa chadema ili kwenye kikao cha bajeti cha julai mwakani wapige mapanga bajeti tupate fedha za elimu na mengineyo. Dr slaa alisahau kuwa yeye ndiye atakayeunda serikali na lazima aonyeshe kwa wapiga kura kuwa ndivyo itakavyokuwa.

Staili ya dr slaa
ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kumsikiliza dr slaa akihutubia ‘ live’.

Nguvu zake:
- dr slaa ana mvuto. Anavuta wasikilizaji. Anaongea kwa staili inayomfanya mtu aamini kuwa dakika ijayo ana kitu cha muhimu zaidi atakitamka. Watu wanavutika, wanabaki kumsikiliza.
- anaongea kwa staili ya kimahubiri. Ana uzoefu katika hilo. Kuna wakati anayaacha matokeo ya anachoongea kwa mungu na watu.
- ametokea ndani ya ccm. Anafahamu kuwa walio wengi anaowahutubia kwa kawaida ni wapiga kura wa ccm. Dr slaa anafahamu, wanachokitafuta wanaomsikiliza walikuwa nacho, wamekipoteza, kwa uzembe. Hata baba wa taifa angefufuka pale mwembe togwa angetamka; ” eh, hivi dr slaa naye amerudi ccm!”. Ndio, jana pale mwembetogwa dr slaa alikuwa anazungumzia ccm ya mwalimu.
- dr slaa mara kwa mara anatumia nafsi ya tatu; ” wanasema dr slaa….” anayesema hayo ni dr slaa.
- hasimami mahala pamoja jukwaani. Anatembea tembea huku akigeukia hadhira yake.
- anachangamka jukwaani. Aliweza hata kurukaruka kidogo. Inawavutia wanaomsikiliza.

Udhaifu wake:
- anaanza hotuba yake kwa kuonyesha ana haraka kidogo. Wanaomsikiza nao wanapata ‘ stress’ ya namna fulani. Watu wanaanza kuangalia saa zao pia. Details hizo zinaweza kumtoa nje msikilizaji.
- wakati mwingine anaonyesha jazba kidogo. Maneno kama ; ” kama kikwete mwanamme…” anatakiwa ayaepuke. Yanaweza kutafsiriwa vibaya na katika nchi nyingine wanaharakati wa jinsia wanaweza kumjia juu.
- anatoa maagizo, anatoa siku saba.. Hata kabla hajaingia ikulu. Labda angetamka zaidi ” chadema tunataka’. Kuna wapigakura wanaohofia kumwingiza madarakani mwenye silika za udikteta.
- dr slaa hakuzungumzia katiba na umuhimu wa kuanzishwa kwa mchakato wa kuandika katiba mpya kwa nchi yetu. Wapiga kura wengi leo wameanza kuelewa kuwa katiba yetu ni chanzo cha matatizo yetu mengi. Haitoshi tu kubadilisha marais na vyama. Huko ni sawa na kuyatoa maji kwenye ndoo ya bati na kuyaingiza kwenye ndoo ya plastiki. Na kubadili ni kuyatoa maji kutoka kwenye ndoo ya plastiki kuarudisha kwenye ndoo ya bati! Maji ni yale yale. Ndio maana , zawadi kubwa kwa sasa kwa watanzania katika kusherehekea miaka 50 ya uhuru ni kuanzisha mchakato wa kuandika katiba mpya shirikishi itakayoirudisha nchi yetu kwenye reli. Na hakika imeanza kuwa kiu kubwa ya watanzania.
- huenda dr slaa hapati muda mwingi wa kutafuta taarifa zenye kuwagusa watu walio mbele yake kumsikiliza. Kuwa watu wengi walijazana pale mwembetogwa jana kwa mtazamo wangu kunachangiwa pia na namna ccm ilivyoboronga katika kumpata mgombea ubunge jimbo la iringa mjini. Miongoni mwa waliomsikiliza dr slaa jana pale mwembetogwa ni wanachama na wapenzi wengi wa ccm. Na ajabu kubwa kabisa; dr slaa tangu mwanzo hadi mwisho wa hotuba yake hakutamka jina la ” mama monica mbega”. Mgombea ubunge wa ccm, iringa mjini. Hata mgombea wa chadema mchungaji msigwa alipopewa dakika tatu na slaa aongee, naye hakutamka jina la ” monica mbega” na kwanini wana iringa mjini wasimchague monica mbega.

Mengineyo;
tatizo la chadema na vyama vingi vingine vya upinzani linabaki pale pale; oganaizesheni. Wengi katika umati ule uliokusanyika pale mwembetogwa hawajui zilipo ofisi za chadema mjini. Hawawajui makada wa chadema. Mkutano kama ule ilikuwa ni fura kwa chadema kuwatambulisha makada wa chadema na wapi wapenzi wa chadema waende kupata taarifa za chama chao.

Badala yake, wengi wa waliokwenda pale mwembetogwa kumsikiliza dr slaa wamerudi majumbani kwao. Na atakayewatembelea tena kuzungumzia uchaguzi ni balozi wao wa nyumba kumi.

Naam. Demokrasia yetu bado changa. Na ishara za jamii inayotaka mabadiliko inaonekana. Tuwe na ujasiri wa kutoa maoni yetu kwa kutanguliza maslahi ya tanzania kwanza. Hata roma haikujengwa kwa siku moja.

Maggid
iringa.

nakubaliana na mengi uliyoyasema katika makala yako. Kazi kubwa iliyofanyika mapaka sasa ni kuwatoa uoga watanzania, baada ya woga kutoka sasa chama kinaweza kujiimarisha nchi nzima. Kumbuka pia kuwa sheria zetu na katiba viko very unfriendly. Inawezekana kwa muda mchache aliokuwa hapa mwembetongwa hakuzungumzia katiba lakini ameshazungumza suala hilo sana na wananchi sasa wanaelewa kuwa endapo dr slaa atafanikiwa kuwa rais mchakato wa kurekebisha katiba utaanzishwa ndani ya siku 100.
 
Mr Mjengwa, in the past you were attention-seeker activist blogger openly supporting CUF. I don't know what has happened to your relationship with CUF. I see you are indirectly trying to infiltrate CCM by bashing Dr Slaa. No way!
CCM supporters do not like your dumb tricks and we condone your low class behavior.
You better stick with what you write and believe in your nonesense and useless blog. All you write and post in your cheap blog is telling people "ooh I was in Sweden, ooh This morning I was in Moro, Oooh I was in KLM flight etc"...who cares or give a sh-it!
Unlike your cheap blog, this is JF where everybody is allowed to express his/her thoughts.
My advice to you: Do keep taking those funny street photos about things or events that make no sense and continue to write those dumb poems of yours.
This is not a blog for small minded and dumb folks like you or your stupid followers. JF is open for everybody.
Please do not come here. Don't even come to Dar. Stay with your dumb issues in Iringa. Stay with CUF or TLP!
Vote CCM
Kwani wewe gaba...li una tofauti na huyu unayeita followers wake stupid?
Kwa taarifa yako maandishi yako na hoja zako hapa JF hazina tofauti kabisa na za Maggid.
 
Back
Top Bottom