Kilichonivutia kwa uchunguzi wa polisi juu ya Hamza

Kilichonivutia kwa uchunguzi wa polisi juu ya Hamza

Kwa mara ya Kwanza polisi wetu wameweza kuchunguza kwa haraka zaidi na kwa mda mfupi mno na
kupataa majibu mengi juu ya gaidi Hamza.kuwa alijifunza Ugaidi mtandaoni,aliishi kwa Siri na kuwa alikua Ni gaidi wa kidini, Imani kali.

Polisi wetu wameweza kufanya uchunguzi huku gaidi Hamza akiwa amekwisha kufa.
Hicho kipengele ndio kilichonivutia zaidi.

Nadhani ni polisi hawa hawa walioshindwa kuchunguza tukio la watu waliopania na kukusudia kumuua Tundu Lissu.
Walishindwa kuchunguza kwa sababu walizozitoa wao kuwa Dereva wa Lisu hayupo iko kutoa ushirikiano wa kuhojiwa,wakati huo Lisu akiwa hospitali za Nairobi na belgium akiondolewa risasi na matibabu mengine.
Kama Hamza kafa na wameweza kupata taarifa zake za matendo yake ya Ugaidi,
Walishindwaje kupata taarifa za Waliotaka kumuua Lisu bila na Dereva na Lisu kuwepo? Lakini wakiwa hai?
Nachojua Mimi Serikali za Kenya na Ubelgiji zingeombwa na polisi wetu kwenda kuwahoji Lisu na Dereva zisingekataa.
Nawasifu polisi wetu kuchunguza kwa haraka na kupata majibu ya gaidi Hamza wakati akiwa amekwisha kufa.
Wamesahau kwamba ukiwa muongo basi usiwe msahaulifu! Wamesahau waliyoyakoroga mengi sana huko nyuma!
 
Mungu akiamua kumuumbua mtu ni sekunde tu,tunakoelekea ni kuzuri sana
 
Tukubali yaishe na tuendelee na mengine,hakuna umuhimu wa kulumbana.
Tunatakiwa kuwatwii walioko madarakani,mengine tumuachie aliye umba mbingu na nchi.
Tungewatii wakoloni wazungu leo tungekuwa mbali sana. Hawa wakoloni weusi, hata ukiwatii haitakusaidia.
 
Kwa mara ya Kwanza polisi wetu wameweza kuchunguza kwa haraka zaidi na kwa muda mfupi mno na kupataa majibu mengi juu ya gaidi Hamza. Kuwa alijifunza Ugaidi mtandaoni, aliishi kwa Siri na kuwa alikuwa ni gaidi wa kidini, Imani kali.

Polisi wetu wameweza kufanya uchunguzi huku gaidi Hamza akiwa amekwisha kufa. Hicho kipengele ndio kilichonivutia zaidi.

Nadhani ni polisi hawa hawa walioshindwa kuchunguza tukio la watu waliopania na kukusudia kumuua Tundu Lissu. Walishindwa kuchunguza kwa sababu walizozitoa wao kuwa Dereva wa Lissu hayupo iko kutoa ushirikiano wa kuhojiwa, wakati huo Lissu akiwa hospitali za Nairobi na Belgium akiondolewa risasi na matibabu mengine.

Kama Hamza kafa na wameweza kupata taarifa zake za matendo yake ya Ugaidi, Walishindwaje kupata taarifa za Waliotaka kumuua Lissu bila na Dereva na Lissu kuwepo? Lakini wakiwa hai?

Nachojua Mimi Serikali za Kenya na Ubelgiji zingeombwa na polisi wetu kwenda kuwahoji Lissu na Dereva zisingekataa. Nawasifu polisi wetu kuchunguza kwa haraka na kupata majibu ya gaidi Hamza wakati akiwa amekwisha kufa.
Mimi sina shaka hata kidogo na Uwezo wa kiuchunguzi wa Jeshi letu la POLISI kwenye maswala ya uchungu ni moja ya Majeshi bora sana duniani na inawataalamu na vifaa vya hali ya juu sana vya kiuchunguzi .Tatizo linakuja pale wanasiasa wanapoliingilia na kutaka wafanye vile wanavyotaka wao ndipo hapo watu wanaliona kama vile ni Jeshi la Hivyo .ila ni Jeshi zuri sana kama litapata wanasiasa wazuri.
 
Back
Top Bottom