Kilichotokea jana usiku kwa watumishi wa TRA ni matokeo ya serikali kushindwa kudhibiti rushwa na ufisadi kwenye utumishi wa umma

Kilichotokea jana usiku kwa watumishi wa TRA ni matokeo ya serikali kushindwa kudhibiti rushwa na ufisadi kwenye utumishi wa umma

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Watumishi wa TRA wengi (sio wote) kila mmoja kwa kitengo chake hutumia nafasi hiyo kujipatia pesa kinyume na taratibu. Serikali inakosa mapato kwasababu watumishi wa TRA na taasisi zingine wako busy kutafuta pesa.

Mmoja wa watumishi wa TRA ambaye kafariki ninafahamiana naye kiasi cha kuweza kupiga story mbili tatu, huwa ananisimulia issue zao nyingi tu za kupiga pesa

Hata usajili wa magari ya magumashi hufanywa na hao watumishi wa TRA kisha watumishi wengine wasiohusika na dili hilo hufuatilia na kumalizana kimyakimya.

Kama wangemkamata wangemalizana naye basi na wananchi kujua nini kinaendelea
Kila mmoja shahidi, Watanzania wengi leseni za vyombo vya moto tumepewa na watumishi wa TRA pasipo kuwa na sifa.

Kuna umuhimu wa serikali kuunda taasisi ya kufuatilia maadili , mienendo na utendaji wa taasisi za umma na watumishi wote nchini.

Hali ya rushwa na ufisadi ni kubwa sana kuliko watu wanavyodhani.
 
1733504614437.png



Amani Kamguna Simbayao anayesemekana ni dereva wa TRA walioshambuliwa jana imeripotiwa amepoteza maisha.

Kama Taifa kunahitajika hatua za makusudi kuiponya mbegu hii ya uhasama inayomea kwa kasi.

Tumepoteza nguvu kazi ya Taifa, kuna watoto wanaenda kuwa Yatima kutokana na Tamaa za Watawala wetu. Nawasihi Jeshi La Polisi, TISS na wengine, msiendelee kutukuza hili, wanaoteketea ni vijana wasio na hatia. Nani anajua anayefuata ni nani?
 
CCM ndio chanzo Cha yt,wameamua nchi iende ilimradii laiti wangeweka mipango haya yt yasingekuwepo ila kwakuwa wameamua iwe hv bac tutajionea mengii..

Ni huzunii
 
Mungu amrehemu huyu braza, alikua bado kijana naamini ana watoto wadogo na wazazi wake wanamtegemea😭😭
 
Watumishi wa TRA wengi (sio wote) kila mmoja kwa kitengo chake hutumia nafasi hiyo kujipatia pesa kinyume na taratibu. Serikali inakosa mapato kwasababu watumishi wa TRA na taasisi zingine wako busy kutafuta pesa..
Mkuu wa inchi siyo mkali linapokuja swala la kusimamia maadili ya watumishi, ripoti za ufisadi kaweka kabatini, hatujasikia mafisadi wanachukuliwa hatua, ndio mana sasa hivi kila secta ni upigaji unaendelea, haya mambo yanakera sana! Unajiuliza huyu kiongozi tumempa marungu yote ya kazi anakwama wapi?
 
Tra unakamata mtu bila kuwa na polisi

ndio maana Wananchi wanawapiga mawe maana wanajua ni wezi tu.

Mbeya napo wafanyakazi wa TRA walifariki gari nzima.. kisa kufukuza magendo tena bila msaada wa polisi

TRA wanapenda sana rushwa ndio zinawafanya wauwawe.
 
Back
Top Bottom