Kilichotokea katika harambee ya kuchangia ujenzi wa nyumba yetu ya ibada

MWONA MBALI

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2016
Posts
460
Reaction score
611
Ama kweli hali ni tete, leo katika harambee ya kuchangia ujenzi wa nyumba yetu ya ibada hali imekuwa tete.

tumeanza na Kuku Jogoo mkubwa tukitegemea ushindani uwe mkubwa kama tulivyozoea tukaweka makisio ya pengine litafika hadi laki tatu na zaidi ila limeishia kuchukuliwa na mwanasiasa kwa tsh.50,000/= mara baada ya kulitoa jogoo ambalo hata mwanasiasa wetu hakulirusha linadiwe tena imebidi tuahirishe mnada hadi wakati mwengine.

mnada umehudhuriwa na watu wachache isivyo kawaida.

Dalali wetu ni yule yule, mahali na muda ni wakawaida siku zote, sijui waumini wamekasirika nini!!!

Mungu atawaona ndugu waumini.
 
Mlitegemea hela nyingi wakati hali yenyewe inafahamika ni tete,hata huyo mwanasiasa aliyetoa akifika kwake atajilaumu kwanini katoa hicho kiasi..
 
Mtoleeni Mungu, acheni ubahili. Mmpewa bure, toeni bure. Kwetu leo jogoo tu kanunuliwa kwa 120,000 na fungu la matembele kwa 35,000. Taabu WaKristo wa leo tunafikiri tunamtolea Pastor ama Askofu badala ya yule aliyetupa mali. Kumbuka mali na dhahabu vyote ni vyake.
 
Mlitegemea hela nyingi wakati hali yenyewe inafahamika ni tete,hata huyo mwanasiasa aliyetoa akifika kwake atajilaumu kwanini katoa hicho kiasi..

Hahaaaa halafu eti walitegemea mwanasiasa alirudishe liuzwe tena wakati mwenzao kashapigia bajeti ya kitoweo usiku. Na anakula haachi hata mifupa. Kwa uchungu

Chezea 50,000 ya mzee wetu....
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ama kweli hali ni tete, leo katika harambee ya kuchangia ujenzi wa nyumba yetu ya ibada hali imekuwa tete.

tumeanza na Kuku Jogoo mkubwa tukitegemea ushindani uwe mkubwa kama tulivyozoea tukaweka makisio ya pengine litafika hadi laki tatu na zaidi ila limeishia kuchukuliwa na mwanasiasa kwa tsh.50,000/= mara baada ya kulitoa jogoo ambalo hata mwanasiasa wetu hakulirusha linadiwe tena imebidi tuahirishe mnada hadi wakati mwengine.

mnada umehudhuriwa na watu wachache isivyo kawaida.

Dalali wetu ni yule yule, mahali na muda ni wakawaida siku zote, sijui waumini wamekasirika nini!!!

Mungu atawaona ndugu waumini.
Mmeligeuza pango la walanguzi
 
Back
Top Bottom