Kilimanjaro: Baba akamatwa akitaka kumuozesha bintiye

Kilimanjaro: Baba akamatwa akitaka kumuozesha bintiye

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Mkazi wa kijiji cha Emuguri, kata ya Njoro Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro(jina lake linahifadhiwa) anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani hapa kwa madai ya kutaka kumuozesha binti yake wa miaka 11 kwa mahari ya ng'ombe watatu.

Tukio hilo lilitokea Agosti 7, mwaka huu katika kijiji hicho ambapo baba huyo aliandaa sherehe ya kimila ya kumuaga binti huyo aliyekuwa aozeshwe kwa kijana wa Kata jirani ya Ruvu.

Kamanda wa Polisi Mkoani Kilimanjaro, Simon Maigwa amethibitisha kukamatwa kwa mzee huyo baada ya kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema.

Kamanda Maigwa amesema wanamshikilia mzee huyo mwenye umri wa miaka 68 kwa uchunguzi wa tukio hilo na upelelezi utakapokamilika atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo zinazomkabili.

"Tunamshikilia mzee mmoja ambaye jina lake tunalihifadhi baada ya kumfanyia sherehe ya kimila binti yake kwaajili ya kumepeleka kwa mwanaume huko Ruvu ,bahati nzuri tulipata taarifa kutoka kwa wasamaria wema ndipo tulipomkamata,"amesema Kamanda Maigwa

Kutokana na tukio hilo, Kamanda Maigwa ametoa onyo kwa watu wenye tabia kama hizo za kuwaozesha watoto wadogo akisema hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mzee huyo ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hizo.

Mwananchi digital ilipoitafuta familia ya binti huyo kujua ni kwanini binti huyo hakupelekwa shule na kutaka kuozeshwa walikataa kutoa ushirikiano na kusema hawawezi kuzungumza chochote kwa sasa.

Chanzo: Mwananchi
 
Duuuh miaka 11, hivi mtoto kama huyo anaenda kufanya majukumu gani ndoani na akili yake ya kitoto hiyo.
Kwe wenzetu hilo ni jambo la kawaida tu.
Walishaoaga hadi Binti wa Miaka 6.
Na kushiriki tendo akiwa na Miaka 9.

Kwao ni jambo la kawaida tu.
Sembuse huyo wa miaka 11
 
Tatizo ni Umasikini ulioletwa na CCM
 
Corona ipo Moshi na Arusha kwa sababu ya laana ya kushangilia kifo cha Magufuli
 
mpaka mtu kanogewa anataka kuoa kabisa maana yake ameshamfanya kila kitu huyo binti wa miaka kumi na moja dah!
 
Kwe wenzetu hilo ni jambo la kawaida tu.
Walishaoaga hadi Binti wa Miaka 6.
Na kushiriki tendo akiwa na Miaka 9.

Kwao ni jambo la kawaida tu.
Sembuse huyo wa miaka 11
Daah ni hatari iyo mkuu mtoto wa miaka 6 hata hisia hana ni kumtesa tu aisee.
 
CCM oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee, Tozo oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee midala tena kwao
 
Back
Top Bottom