Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepata ushindi mkubwa katika Kata ya Mbokomu, baada ya kushinda vitongoji vitano kati ya saba. Ushindi huu unathibitisha umaarufu wa CHADEMA katika kata hiyo, huku wananchi wakionyesha imani kubwa kwa chama hicho katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa.