Kilimanjaro ipo nyuma sana katika Soka

Kilimanjaro ipo nyuma sana katika Soka

Ab5

Senior Member
Joined
Dec 3, 2017
Posts
151
Reaction score
99
Oya wadau kuna swala linanikera ni mkoa wa KILIMANJARO kukosa timu ligi kuu Tanzania bara.

Hivi tatizo ni nini kwa viongozi wetu tunakwama wapi hadi tukose timu ligi kuu?

Mimi tangu niijue ligi kuu bara sijawahi kusikia kuna timu ya same, mwanga, Moshi mjini, Moshi vijijini, Hai au Rombo inashiriki ligi kuu Tanzania Bara au mnashiriki ya ligi ya Kenya?

Lakini nimetembea maeneo kama Makanya, Hedaru, Gonja, Same, Kisiwani, Himo, Rombo & Machame kana vipaji kwelikweli Kwa vijana wa shuleni na mtaani.

Vipaji hivi nimevuona kweny michuano kama copacocala. Hivi hamjui Kupitia soka tunaweza tukatangaza zaidi vivutio vya utalii kama mbuga ya Mkomazi, maporomoko ya shengena, mlima KILIMANJARO N.K

My take hakikisheni mwakani tunatoa timu ligi kuu. Tunashindwa hadi na mikoa ya kusini shubamitiii
 
Soka bongo hailipi na wala haina faida endelevu, ndio maana haishobokewi pande zile.
 
Soka bongo hailipi na wala haina faida endelevu, ndio maana haishobokewi pande zile.
Hailipi?
Haina faida?

Chukuwa mfano wa singida utd wana wadhamini kedekede zaidi ya 7 ,

Tena saizi ndio kuna lipa balaa sports pesa ,Azam,vodacom etc etc

Hakuna sehemu yenye ulaji kwasasa kama mpira hapa bongo
 
For sure sisi wa kilimanjaro tumefeli hapa
 
Huwezi ukawa bora kwenye kila kitu, sisi kazi yetu ni kufanya biashara na kuimarisha uchumi wa nchi. Mpira watafanya wengine...
 
Mkoa wenyewe hauna historia ya kutoa wachezaji wakubwa.Ushauri:Hapo kwenye MY TAKE unatakiwa utuambie soka lisipoendelezwa au likiendelezwa mkoani Kilimanjaro kutakuwa na madhara/faida A,B,C
 
Mkoa wenyewe hauna historia ya kutoa wachezaji wakubwa.Ushauri:Hapo kwenye MY TAKE unatakiwa utuambie soka lisipoendelezwa au likiendelezwa mkoani Kilimanjaro kutakuwa na madhara/faida A,B,C
Nimetoa faida ikiwemo kutnagaza zaidi vivutio vya kitalii vya mkoa wetu ni vingi mno
.Kufungua fursa za biashara mbali kutokana na muingiliano wa watu
.kupunguza tatizo la uhaba wa ajira kwani vijana wengi watapata nafasi kweny timu hiyo au hizo
.vilevile kutoa fursa kwa wawekezaji kuwekeza kweny mpira mkoani kwetu kwani siku hizi mpira pesa. Club ikifika ligi kudu ni rahisi sana kupata wazamini wa kueleweka
Vilevile burudani kwa watu wa mkoa wetu kushuhudia pindi timu yao ikicheza
Bila kusahau kukuza soka la bongo general kwa kupata vipaji kutoka Kilimanjaro
 
Waache kilimanjaro aisee kipaji walicho nacho madem wake watam kwelikweli
 
Back
Top Bottom