Kilimanjaro: Jengo la shule lahatarisha usalama wa wanafunzi

Kilimanjaro: Jengo la shule lahatarisha usalama wa wanafunzi

Bushmamy

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2019
Posts
9,140
Reaction score
15,963
Serikali ya Kijiji cha Kikarara kilichopo Kata ya Old Moshi Mashariki kwa kushirikiana na uongozi wa Shule ya Msingi Matemboni imewalazimu kuwahamisha Wanafunzi kutoka katika vyumba vitatu vya madarasa kutokana na hali ya usalama wa majengo hayo.

Wanafunzi waliohamishwa wamechanganywa katika vyumba vingine vya madarasa kutokana na ubovu wa vyumba vya madarasa kuhatarisha uhai wa wanafunzi hao.

Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Auniel Temba amesema shule hiyo ya Msingi Matemboni ilijengwa kabla ya uhuru na hadi sasa haijawahi kufanyiwa marekebisho yoyote.


IMG-20230314-WA0010.jpg
IMG-20230314-WA0013.jpg
IMG-20230314-WA0015.jpg
IMG-20230314-WA0017.jpg

MWENYEKITI ATOA TAMKO
Mwenyekiti wa Kijiji cha Kikarara, Auniel Temba amekiri kuwa ni kweli hizo picha ni za madarasa ya Shule ya Msingi Matemboni

“Ni madarasa machakavu na tumeshaomba Serikali iyabomoe kwa kuwa ni hatarishi kwa watu wote. Wanafunzi wamehamishwa hawayatumii madarasa hayo kwa sasa.

“Tumezuia Wanafunzi na watu wengine wote kutosogea katika majengo hayo, tunaendelea kupiga kelele ili wahusika waje wafanye mabadiliko.

Unapotaka kubomoa jengo la Serikali lazima upate kibali cha Serikali, walishakuja wahandisi kwa ajili ya kufanya tathimini Mwaka 2022, tangu wameondoka hawajarudi.

“Hii ni shule kongwe na ina darasa la kwanza hadi la saba, hali hiyo imesababisha Wazazi kuanza kuhamisha watoto wao wakihofia usalama."
 
Kwa hali hii tukomeshe mara moja hizi biashara za magoli na misaada kwa wahanga nchi za nje.

Tukiendelea, kwa hakika tutakuwa hatujitambui.
 
Aiseeee! Hivi hizi tozo za miamala ya simu kwa ajili ujenzi wa madarasa na madawati kila mwezi bilioni 100 zinaenda wapi?

Halafu wanajenga vipi bila rinta
 
Wandugu wa old moshi jamani tukutane hapa. Chama na serikali wako bize kununua magoli tuje huku tuokoe maisha ya watoto wetu wasije dondokewa na kuta mashuleni.
 
Back
Top Bottom