Jeshi la polisi mkoani Kilamanjaro linamshikilia mwanamke mmoja maarufu kama mama Baraka pamoja na mwanae wa kiume aitwae Baraka mwenye umri wa miaka 20 kwa kosa la mauji ya mumewe ajulikanae kwa jina la Fasil Herman mwenye umri wa miaka 57.
Mauaji hayo yametokea katika maeneo ya Forest, kata ya Ngarenairobi, wilaya ya Siha,
Mdogo wa marehemu anasema kuwa kwa mujibu wa mashuhuda waliowahi eneo la tukio ni kuwa mke na mume walikuwa wakipigana na ndipo kijana nae kuingilia ugomvi na hatimae mume kudondoka chini na kufariki dunia.