Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Mwananfunzi wa kidato cha nne Shule ya Sekondari Cyril Chami, Yasinta Mathew (17) amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kile kilichodaiwa kuwa na msongo wa mawazo
Kamanda Maigwa amesema tukio hilo lilitokea Agosti 16, 2021 maeneo ya Mweka kata ya Kibosho Mashariki ambapo mwanafunzi huyo alijinyonga kwa vitenge viwili alivyovifunga juu ya paa la nyumba aliyokuwa akiishi .
Ameeleza kuwa katika uchunguzi wa awali inadaiwa kuwa chanzo cha tukio hilo ni msongo wa mawazo baada ya kusimamishwa masomo na kwamba mwili wa marehemu tayari umefanyiwa uchunguzi na daktari na kukabidhiwa kwa ndugu zake kwa taratibu za mazishi.