Kilimanjaro: Mwanafunzi Ajinyonga kwa msongo wa Mawazo

Kilimanjaro: Mwanafunzi Ajinyonga kwa msongo wa Mawazo

Mbona Grace wa ifm mamaye alimuwahi Yuko kitaa anadunda. Na Tena atapata mme na familia fresh tu maisha yataenda. Ni Nani asiyefanya zinaa anyooshe mkono

unadhani mpuuzi huwa na majuto!!!

wenye majuto ni wale wanaokosea kwa bahati mbaya,huyu anayekandwa huku anajirekodi ni kahaba tu hana excuse.
 
Hatari za kuwa nje ya Kristo ni nyingi.


Kristo ndiye atufarijiye, ndiye tumaini letu; Na ndiye Mwokozi wetu.



JESUS IS SAVIOR
 
Mwananfunzi wa kidato cha nne Shule ya Sekondari Cyril Chami, Yasinta Mathew (17) amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kile kilichodaiwa kuwa na msongo wa mawazo

Kamanda Maigwa amesema tukio hilo lilitokea Agosti 16, 2021 maeneo ya Mweka kata ya Kibosho Mashariki ambapo mwanafunzi huyo alijinyonga kwa vitenge viwili alivyovifunga juu ya paa la nyumba aliyokuwa akiishi .

Ameeleza kuwa katika uchunguzi wa awali inadaiwa kuwa chanzo cha tukio hilo ni msongo wa mawazo baada ya kusimamishwa masomo na kwamba mwili wa marehemu tayari umefanyiwa uchunguzi na daktari na kukabidhiwa kwa ndugu zake kwa taratibu za mazishi.
Japan ni nchi ambayo vijana wa shule hasa secondary hadi chuo wanajiua sana kutokana na stress za shule zisizo na future.
Mzazi anamlazimisha kijana aende shule huku uhakika na future ya mtoto haieleweki, poleni wazazi wenzangu tuna watoto pia wapo mashuleni huko
 
Mtoto anapozaliwa is empty he knows A and B from parents, anakoalekea ni matokeo ya malezi ya Baba na Mama, this include every decisions they make!
Hapo kwenye kubarehe hua pabaya sana. Mimi nlivofika form two siku moja nlijitafakari nkaona nmebadlika sana na nkiendelea huko nnakoelekea ntaishia pabaya, nashkuru mungu nlifanikiwa kujirudsha kwenye mstari.

Nlikua shule ya boarding. Utukutu mwingi, nlikua na kesi karibia na kila mwalimu, nlianza kujiamini sana, prepo usiku mi natoroka na wa4m4 (wazoefu) naingia mtaani knunua soft drinks na chips + kuzurura (atleast mara tatu kwa wiki) + vitabia vingine vingi vya ujingaujinga.

Hapo tayari nlikua na kesi pia ambazo kama zingefuatiliwa vizuri ningefukuzwa shule bila kujitetea.

Kitu kilchonpa alarm nkaona nnakoelekea napotea ni siku ambayo nlifanya mtihani wa terminal. Tangu nmeanza darasa la kwnza skuwahkua nje ya top5 katka matokeo, ila ile pepa nlikua ktka nafas 6 za mwisho out of 42 (private), na katika somo langu pendwa la b/math nligundua nmekua kilaza sana sababu skujib chochote cha maana na tayar nlikua nmeamua kulko aibu ya kupata F, bora niache kukusanya niztafte answersheet japo msimamiz aliniwah kabla sjaanza kutekeleza uamzi wangu.

In short nlikua nshakua mjinga sana na nakiri nlikua nafanya vitu vya kijinga na vyaovyoovyo sana.

Nafikiri mama yangu alikua ananiombea sana, na sala zake ndizo zilinisaidia kubadlika mpaka kufikia mwisho wa mwaka kpind tunafanya mtihan wa taifa nlikunmerudia form yangu ya sku zote.

Wito kwa wazazi, jitahidi kufanya followup kwa mtoto hasa pale anapoanza kuingia adolesence, apo hua kuna uharibifu mwingi uspokaa makini,
 
Jamani ndugu kaka dada shangazi wajomba wamama wadogo wababa wakubwa wabibi na wababu jaribu kufundisha watoto wakiwa wadogo ama mkiwa nao nyumbani emotional Intelligence
 
Ni vigumu kumtia moyo haraka kiivyo,binti yako karudishwa nyumbani,unaamua kufuatilia unaambiwa kakamatwa akiwa bweni la wanaume ametoka kulala au kakamatwa uwanjani anafanya mapenzi,au alitoroka kaenda disco,hivi huyo unaanzaje kumfariji kwanza?
Mmh...
 
Ni vigumu kumtia moyo haraka kiivyo,binti yako karudishwa nyumbani,unaamua kufuatilia unaambiwa kakamatwa akiwa bweni la wanaume ametoka kulala au kakamatwa uwanjani anafanya mapenzi,au alitoroka kaenda disco,hivi huyo unaanzaje kumfariji kwanza?
Chukulia ni madhaifu yake,

pia angalia kama ulishawahi kumuelimisha juu ya kukabiliana na vishawishi/mihemko ya mwili

mimi nina watoto wawili wa kwanza wa kiume ana 4 yrs na wa pili wa kike ana 2yrs, siku zote huwa naumiza kichwa namna ya kuwalea katika misingi imara ili waweze kukabiliana na hali ya maisha watakayokutana nayo

Hata ikitokea binti yangu akipata ujauzito kabla ya wakati mimi nitakua tayari kuwajibishwa
 
Chukulia ni madhaifu yake,

pia angalia kama ulishawahi kumuelimisha juu ya kukabiliana na vishawishi/mihemko ya mwili

mimi nina watoto wawili wa kwanza wa kiume ana 4 yrs na wa pili wa kike ana 2yrs, siku zote huwa naumiza kichwa namna ya kuwalea katika misingi imara ili waweze kukabiliana na hali ya maisha watakayokutana nayo

Hata ikitokea binti yangu akipata ujauzito kabla ya wakati mimi nitakua tayari kuwajibishwa
Uko sahihi pia
 
Umenikumbusha story moja iliwahi kutokea huku zenj. Kuna msichana wa form four picha zake za uchi zilirushwa kwenye mitandao. Yule mtt inaonekana alipata ushauri wa kisaikolojia. Baada ya siku chache alirudi tena kwenye mtandao kuomba radhi kwa wazazi wake, kwa Serikali pamoja na jamii yote. Wako waliombeza lkn inaonekana wazazi wake walimsameh na kuwa upande wake kwa kujua binaadam anakosea wakati wowote. Hakuna mkamilifu.

Sisi mpaka kufika tulipofika hapa tushafanya maovu mengi tu. Tushaumiza wengi tu. Tumesamehewa na maisha yameendelea na sasa ni watu tunaoheshimika katika jamii zetu.
Baada ya siku chache alirudi tena kwenye mtandao kuomba radhi kwa wazazi wake, kwa Serikali pamoja na jamii yote. Wako waliombeza lkn inaonekana wazazi wake walimsameh na kuwa upande wake kwa kujua binaadam anakosea wakati wowote. Hakuna mkamilifu.[emoji1548][emoji1752][emoji1752][emoji1752]
 
Back
Top Bottom