Sir John Roberts
JF-Expert Member
- Mar 1, 2017
- 12,835
- 23,584
Hii dunia hii Mungu ataumiza watu sana huko tuendako.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu inawezekana alibaka au alitengenezewa kesi...Ila sheria hizi, mtu anaweza akacheza na vifungu ukaonekana hujaua ata kama ulionekana na watu
Yote yanawezekana mkuuMkuu inawezekana alibaka au alitengenezewa kesi...
kuna kitu humo ndani parokiani kimejificha...
Hizi kesi za kubaka nimesha shuhudia zaidi ya nne zilizotengenezwa na mtoto amefundishwa kuongea... Bahati Mbaya mbele ya mahakama anajisahau anasema nimeambiwa niseme hivi tofauti na maelezo polisi
Huyo Padre atafutiwe Kigango kingine, hapo alipo hatakuwa salamaAkielezea hukumu hiyo, wakili wa upande wa utetezi, Edwin Silayo alieleza kuwa baada ya mahakama kufuatilia mwenendo wa kesi pamoja na kusikiliza mashahidi wa pande zote upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha tuhuma zilizokuwa zikimkabili padri huyo.
Wakili wa serikali kauza mechi!Hafai tena kuwa mtumishi wa Mungu, ameshinda kesi kwasababu ya makosa ya hati ya mashataka na sio kwamba hakubaka.
Mbakwaji na maandalizi ya hati ya mashitaka iliyomfanya Padri ashinde kesi anausikaje hapo!? Muaandaji wa hati ya mashitaka ni wakili wa serikali (DPP) sasa mapungufu ya DPP yanaamuhusi vipi Muathirika!? Mahakama iaache visingizio,isimamie haki,na isiruhusu kabisa mapungufu madogo ya kisheria kuchukua nafasi ya Haki!!!Naona watu.wengi humu wanapenda wenzao yawafike mabaya. Yani Padre kushinda kesi watu hawataki kabisa yani tayari wana hukumu zao kuwa padre lazima atakuwa amebakq tu. Jamani !
Mno mnoTaarifa mbaya sana hii kwa FaizaFoxy na genge lake.
Ameweka panapowekwa na mheshimiwa?Kisa ni dem mmoja hivi hawara wa mheshimiwa ...jamaa akaamua mchafua
Mkuu, umepiga kwenye mshono.1. Ni keli hakubaka? au legal technicalities zimemtoa?
UKWELI ANAUJUA MUNGU NA NAFSI YAKE PADRE
Sheria ina shida gani?.Binadamu ndio wanafiki sio sheria.Sheria iko vile ilivyotengenezwa na binadamu.shida iko kwa watumiaji.Ndiomaana siipendi sheria, ni unafiki wa kiwango cha lami
Ila kweli inawezekana kosa amelitenda haiwezekani asingiziwe... sema ndo hivo hapo atahamishwa atupwe sabattical roma baada ya miaka 7 arudishwe bongo atupwe huko ruvuma au lindiAskofu wake ukweli anaujua unaweza ushinde mahakamani lakini bado kanisani ukapigwa ban…ngoja arudi apelekwe roma sabattical leave
NdioAmeweka panapowekwa na mheshimiwa?
Kama alifanya kanisa linajua hata rudi …Ila kweli inawezekana kosa amelitenda haiwezekani asingiziwe... sema ndo hivo hapo atahamishwa atupwe sabattical roma baada ya miaka 7 arudishwe bongo atupwe huko ruvuma au lindi
Hapa kuna jambo.Wizara ya ustawi wa Jamii na Watetezi wa watoto lazima waingilie kati na wakate rufaa . Huyu Padri atahamishwa na kwenda sehemu nyingine mpya na kuboresha mbinu zake za kuhadaa watoto wenye umri mdogo. Kesi hii ni nyeti na ilitakiwa ipewe uzito wake. Hapa kuna heshima ya Kanisa Katoliki ambayo inawezwa kulindwa kwa nguvu yoyote ile na kuwanyima haki waathirika.Padri Sosthenes Soka (42) wa Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi, sasa yuko huru, baada ya kupangua kesi zote tatu za ubakaji zilizokuwa zikimkabili mbele ya mahakimu watatu tofauti katika Mahakama ya Hakimu Mkazi na Wilaya ya Moshi.
Hii ni baada ya kuachiwa huru leo Septemba 29, 2023 katika kesi ya jinai namba 349 ya mwaka 2022 kati ya kesi tatu za ubakaji zilizokuwa zikimkabili ambapo alikuwa akishtakiwa kwa kosa la ubakaji wa mtoto mwenye umri wa miaka 13, katika kanisa alilokuwa akihudumu.
Padri Soka ambaye alikuwa akitoa huduma katika Parokia teule ya Mtakatifu Dionis Aropagita ya Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi, alifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza, Septemba 26, 2022 na kufunguliwa kesi tatu tofauti za kubaka watoto watatu zilizosomwa kwa mahakimu watatu tofauti.
Katika kesi ya kwanza ya jinai namba 44 ya mwaka 2022 iliyokuwa ikisikilizwa na hakimu mkazi Jenipha Edward, Mahakama ilimuachia huru Septemba 22, mwaka huu baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha shtaka la ubakaji na ulawiti wa mtoto wa miaka 12 lililokuwa likimkabili.
Septemba 25, mahakama hiyo pia ilimuachia huru Padri Soka katika kesi ya jinai namba 45 ya mwaka 2022 ya ubakaji wa mtoto mwenye umri wa miaka 12, ambayo ilikuwa ikisikilizwa na Hakimu mkazi mwandamizi wa Mahakama hiyo, Herieth Mhenga.
Kama ilivyokuwa katika kesi namba 44 na 45 za mwaka 2022, ndivyo imekuwa katika kesi namba 349 ambapo Padri Soka ameachiwa huru leo Septemba 29 baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha shtaka kwa viwango ambavyo sheria inataka.
Katika hukumu hiyo ambayo imetolewa leo Septemba 29 na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Moshi, Erasto Philly aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo, alielezwa kuwa upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha shtaka kwa kiwango ambacho sheria inataka na kwamba kulikuwa na utofauti mkubwa kati ya shahidi na shahidi na hati ya mashtaka.
Mbali na kutofautiana kwa maelezo yaliyotolewa na mashahidi wa upande wa mashitaka ilielezwa sababu nyingine za kuachiwa huru kwa padri huyo ni kuwa kesi hiyo upelelezi wake haukufanywa kwani kulitofautiana kati ya hati ya mashtaka iliyoeleza mtoto alifanyiwa tukio hilo siku moja huku maelezo ya mtoto yakionyesha alifanyiwa tukio hilo zaidi ya mara moja.
Akielezea hukumu hiyo, wakili wa upande wa utetezi, Edwin Silayo alieleza kuwa baada ya mahakama kufuatilia mwenendo wa kesi pamoja na kusikiliza mashahidi wa pande zote upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha tuhuma zilizokuwa zikimkabili padri huyo.
Alidai baada ya upande wa mahakama kupitia maelezo ya pande zote mbili kulikuwa na mashaka mengi upande wa mashtaka na hivyo mahakama ikaweza kuthibitisha kuwa Padri Soka hakuwa na hatia katika kesi hiyo.
"Leo ilikuwa ni hukumu kati ya kesi tatu zilizokuwa zikimkabili Padri Soka, Mahakama baada ya kufuatilia mwenendo wa kesi na yote yaliyojiri na kusikiliza mashahidi wa pande zote wamekuta hana hatia kwa kuwa upande wa mashtaka walishindwa kuthibitisha kesi hii," amesema.
"Leo hii tunashangalia na tunafuraha kubwa kwa kuwa mahakama imeweza kuthibitisha katika kesi zote kwamba Padre Soka hakuhusika kwa namna yoyote katika tuhuma ambazo zilikuwa zikimkabili," amesema.
Sidhani kama atarudHapa kuna jambo.Wizara ya ustawi wa Jamii na Watetezi wa watoto lazima waingilie kati na wakate rufaa . Huyu Padri atahamishwa na kwenda sehemu nyingine mpya na kuboresha mbinu zake za kuhadaa watoto wenye umri mdogo. Kesi hii ni nyeti na ilitakiwa ipewe uzito wake. Hapa kuna heshima ya Kanisa Katoliki ambayo inawezwa kulindwa kwa nguvu yoyote ile na kuwanyima haki waathirika.