Kilimanjaro: Padri Soka aliyedaiwa kubaka Watoto ashinda kesi 3 za Ubakaji, sasa yupo huru rasmi

Kilimanjaro: Padri Soka aliyedaiwa kubaka Watoto ashinda kesi 3 za Ubakaji, sasa yupo huru rasmi

Kila nikimkumbuka yule mama ambaye mtoto wake aliingiliwa alivyokua akilia napata uchungu sana. Huyo padre aishi kwa tahadhari sana yanaweza kumkuta makubwa watu wakachukua sheria mkononi.
 
Ila sheria hizi, mtu anaweza akacheza na vifungu ukaonekana hujaua ata kama ulionekana na watu
Mkuu inawezekana alibaka au alitengenezewa kesi...
kuna kitu humo ndani parokiani kimejificha...
Hizi kesi za kubaka nimesha shuhudia zaidi ya nne zilizotengenezwa na mtoto amefundishwa kuongea... Bahati Mbaya mbele ya mahakama anajisahau anasema nimeambiwa niseme hivi tofauti na maelezo polisi
 
Yote yanawezekana mkuu
 
Akielezea hukumu hiyo, wakili wa upande wa utetezi, Edwin Silayo alieleza kuwa baada ya mahakama kufuatilia mwenendo wa kesi pamoja na kusikiliza mashahidi wa pande zote upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha tuhuma zilizokuwa zikimkabili padri huyo.
Huyo Padre atafutiwe Kigango kingine, hapo alipo hatakuwa salama
 
Naona watu.wengi humu wanapenda wenzao yawafike mabaya. Yani Padre kushinda kesi watu hawataki kabisa yani tayari wana hukumu zao kuwa padre lazima atakuwa amebakq tu. Jamani !
 
Karma is a bitch.
Kama kweli Ni mbakaji Basi watoto wa hao mahakimu wakae mkao wa kuliwa na Padre.

Ushauri wa bure. Mapadre waoe au wawe na magel friend maana wengi wanatembea na wake za watu.
 
Naona watu.wengi humu wanapenda wenzao yawafike mabaya. Yani Padre kushinda kesi watu hawataki kabisa yani tayari wana hukumu zao kuwa padre lazima atakuwa amebakq tu. Jamani !
Mbakwaji na maandalizi ya hati ya mashitaka iliyomfanya Padri ashinde kesi anausikaje hapo!? Muaandaji wa hati ya mashitaka ni wakili wa serikali (DPP) sasa mapungufu ya DPP yanaamuhusi vipi Muathirika!? Mahakama iaache visingizio,isimamie haki,na isiruhusu kabisa mapungufu madogo ya kisheria kuchukua nafasi ya Haki!!!
 
1. Ni keli hakubaka? au legal technicalities zimemtoa?

UKWELI ANAUJUA MUNGU NA NAFSI YAKE PADRE
Mkuu, umepiga kwenye mshono.

Kila siku huwa nawaambia watu kwamba sio kila aliyefungwa ametenda kosa aliloshtakiwa nalo, na si kila aliyeachiwa huru hakutenda kosa aliloshtakiwa nalo, kuna wakati mtuhumiwa anafungwa kwa kushindwa kujitetea; au mwingine anaachiliwa huru kwa udhaifu wa upande wa mashtaka kuthibitisha kosa linalomkabili mtuhumiwa.

Uko sahihi, ukweli anaujua Mungu na Padre Soka.
 
Uzuri ukitoa mahakama Kanisa pia huchunguza kwa siri mwenendo wa mtuhumiwa ili kudhibitisha kama yapo mazingira yenye viashiria vya ukweli. Askofu wake atachukua hatua kama kuna viashiria vya ukweli.

Askofu akiwa si mtenda haki na Padri akatumia mianya ya kisheria kujinasua atakutana na hukumu ya muumba wake kwa namna ya kutisha maana ni mtumishi wake.

Ila ikiwa ni njama ovu dhidi ya Padre ni laana mbaya.
 
Huu Uzi utakosa wachangiaji , lakini ule wa kwanza wakati anahukumiwa Uzi ulitembea Kama moto nyikani. Ni wazi kwamba binadamu Ni wepesi kuhukumu, lakini hukumu imetoka padri kashinda kesi watu hawana la kuchangia.
 
Askofu wake ukweli anaujua unaweza ushinde mahakamani lakini bado kanisani ukapigwa ban…ngoja arudi apelekwe roma sabattical leave
Ila kweli inawezekana kosa amelitenda haiwezekani asingiziwe... sema ndo hivo hapo atahamishwa atupwe sabattical roma baada ya miaka 7 arudishwe bongo atupwe huko ruvuma au lindi
 
Padri Sosthenes Soka (42) wa Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi, sasa yuko huru, baada ya kupangua kesi zote tatu za ubakaji zilizokuwa zikimkabili mbele ya mahakimu watatu tofauti katika Mahakama ya Hakimu Mkazi na Wilaya ya Moshi.

Hii ni baada ya kuachiwa huru leo Septemba 29, 2023 katika kesi ya jinai namba 349 ya mwaka 2022 kati ya kesi tatu za ubakaji zilizokuwa zikimkabili ambapo alikuwa akishtakiwa kwa kosa la ubakaji wa mtoto mwenye umri wa miaka 13, katika kanisa alilokuwa akihudumu.

Padri Soka ambaye alikuwa akitoa huduma katika Parokia teule ya Mtakatifu Dionis Aropagita ya Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi, alifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza, Septemba 26, 2022 na kufunguliwa kesi tatu tofauti za kubaka watoto watatu zilizosomwa kwa mahakimu watatu tofauti.

Katika kesi ya kwanza ya jinai namba 44 ya mwaka 2022 iliyokuwa ikisikilizwa na hakimu mkazi Jenipha Edward, Mahakama ilimuachia huru Septemba 22, mwaka huu baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha shtaka la ubakaji na ulawiti wa mtoto wa miaka 12 lililokuwa likimkabili.

Septemba 25, mahakama hiyo pia ilimuachia huru Padri Soka katika kesi ya jinai namba 45 ya mwaka 2022 ya ubakaji wa mtoto mwenye umri wa miaka 12, ambayo ilikuwa ikisikilizwa na Hakimu mkazi mwandamizi wa Mahakama hiyo, Herieth Mhenga.

Kama ilivyokuwa katika kesi namba 44 na 45 za mwaka 2022, ndivyo imekuwa katika kesi namba 349 ambapo Padri Soka ameachiwa huru leo Septemba 29 baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha shtaka kwa viwango ambavyo sheria inataka.

Katika hukumu hiyo ambayo imetolewa leo Septemba 29 na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Moshi, Erasto Philly aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo, alielezwa kuwa upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha shtaka kwa kiwango ambacho sheria inataka na kwamba kulikuwa na utofauti mkubwa kati ya shahidi na shahidi na hati ya mashtaka.

Mbali na kutofautiana kwa maelezo yaliyotolewa na mashahidi wa upande wa mashitaka ilielezwa sababu nyingine za kuachiwa huru kwa padri huyo ni kuwa kesi hiyo upelelezi wake haukufanywa kwani kulitofautiana kati ya hati ya mashtaka iliyoeleza mtoto alifanyiwa tukio hilo siku moja huku maelezo ya mtoto yakionyesha alifanyiwa tukio hilo zaidi ya mara moja.

Akielezea hukumu hiyo, wakili wa upande wa utetezi, Edwin Silayo alieleza kuwa baada ya mahakama kufuatilia mwenendo wa kesi pamoja na kusikiliza mashahidi wa pande zote upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha tuhuma zilizokuwa zikimkabili padri huyo.

Alidai baada ya upande wa mahakama kupitia maelezo ya pande zote mbili kulikuwa na mashaka mengi upande wa mashtaka na hivyo mahakama ikaweza kuthibitisha kuwa Padri Soka hakuwa na hatia katika kesi hiyo.

"Leo ilikuwa ni hukumu kati ya kesi tatu zilizokuwa zikimkabili Padri Soka, Mahakama baada ya kufuatilia mwenendo wa kesi na yote yaliyojiri na kusikiliza mashahidi wa pande zote wamekuta hana hatia kwa kuwa upande wa mashtaka walishindwa kuthibitisha kesi hii," amesema.

"Leo hii tunashangalia na tunafuraha kubwa kwa kuwa mahakama imeweza kuthibitisha katika kesi zote kwamba Padre Soka hakuhusika kwa namna yoyote katika tuhuma ambazo zilikuwa zikimkabili," amesema.
Hapa kuna jambo.Wizara ya ustawi wa Jamii na Watetezi wa watoto lazima waingilie kati na wakate rufaa . Huyu Padri atahamishwa na kwenda sehemu nyingine mpya na kuboresha mbinu zake za kuhadaa watoto wenye umri mdogo. Kesi hii ni nyeti na ilitakiwa ipewe uzito wake. Hapa kuna heshima ya Kanisa Katoliki ambayo inawezwa kulindwa kwa nguvu yoyote ile na kuwanyima haki waathirika.
 
Sidhani kama atarud
 
Back
Top Bottom