Kilimanjaro: Polisi yamsaka Mwalimu kwa tuhuma za kumuua Mwanafunzi wa Darasa la Kwanza

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760

Jeshi la Polisi Tanzania limesema kuwa tuhumiwa huyo James Fabian Urasa anatafutwa kwa tuhuma za kutenda kosa hilo dhidi ya aliyekuwa Mwanafunzi katika Shule ya Msingi Samanga ya Wilayani Rombo.

Inadaiwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo Julai 17, 2023 na kutokomea kusikojulikana

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amesema “Mtuhumiwa alimpa adhabu ya viboko Mwanafunzi baada ya kupiga kelele, aliporejea kwenye dawati lake Mwanafunzi akaanza kujisikia vibaya na ndipo wakampeleka hospitali, akiwa huko akafariki Duniani.

“Baada ya Mwalimu kusikia hivyo, akazima simu na kukimbia, tumemtafuta hatujafanikiwa, juhudi zinaendelea kumtafuta ndio maana tumetoa tangazo hilo, ni bora angebaki kwa kuwa inawezekana Mtoto alikuwa na changamoto zake nyingine za kiafya lakini kitendo cha yeye kukimbia inamaanisha kuna kitu kibaya alichomaanisha.
 
Atakuwa Kenya huyu hapo ni karibu Sanaa

USSR
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…