Kilimanjaro Stars yaaga rasmi CECAFA baada ya kufungwa na Rwanda goli 2-1. Hii Timu Inakera kuliko Kawaida

Kilimanjaro Stars yaaga rasmi CECAFA baada ya kufungwa na Rwanda goli 2-1. Hii Timu Inakera kuliko Kawaida

Kocha mwenyewe mbwembwe kibao ufundi sifuri, anulizwa kiswahili anajibu kiingereza anajifanya ufundi wa mpira upo kwenye maneno kumbe hata kina Mbwiga wanajua kupiga porojo kuliko yeye.
Hapa katumia udhaifu wa TFF kutojua wafanye nini timu yetu ifanye vizur, amewapigia story za mpira wakadhani naye huyu ni kocha. Ndio maana kuna watu walikuwa wanamtaka mwanamichezo mwenzao aiongoze TFF na sio hawa wazee wa majaribio.
 
Ama kweli leo nimeamini Tanzania ni kichwa cha mwandawazimu, ni lini tutajivunia timu yetu ya taifa?. Cecafa senior challenge cup tumepigwa tena huko 2-1 na Rwanda ni aibu sana kwakweli.
Andika Tanzania bara ama Tanganyika. Ukisema Tanzania unawajumuisha na Zanzibar
 
Ama kweli leo nimeamini Tanzania ni kichwa cha mwandawazimu, ni lini tutajivunia timu yetu ya taifa?. Cecafa senior challenge cup tumepigwa tena huko 2-1 na Rwanda ni aibu sana kwakweli.
Ni Tanganyika ama Tanzania Bara
 
Kilimanjaro Stars ni kichefuchefu tu kwakweli

......akina Ajibu na wenzake ujanja wao ni kwa timu za kibongobongo tu Njombe Mji, Mbeya City na Stand United tu.
 
Mimi nashauri Taifa kama Taifa liwekeze miongoni mwa hivi vitu riadha ngumi muziki basi waachane na hawa vichwa maji, mbona India wanatambulika kwa Hollywood kwanini sisi tusiwekeze kwenye mziki ama riadha.
 
Nakubaliana wewe kwa asilimia zote.
 
Timu ya Tanzania bara, Kilimanjaro Stars imeaga rasmi mashindano ya CECAFA baada ya kufungwa na Rwanda goli 2-1.

Magoli ya Rwanda yalifungwa dakika ya 17 na 66, wafungaji wakiwa ni Innocent Nshuti na Biramahire Abeddy, Kilimanjaro stars ilipata goli dakika ya 29 kupitia Danny Lyanga

Kabla ya Rwanda, Kilimanjaro Stars walitoa suluhu ya 0-0 na Libya na kisha kufungwa na Zanzibar Heroes goli 2-1



======================================================

Kila siku liko vile vile michuano yote iko vile vile ni kupigwa na kudroo tu haina mabadiliko ya kuwapa furaha mashabiki, Kocha wao Kiswahili kirefu sana na Kiingereza chake anatuona sisi mazuzu.

Walah uzalendo wangu kwa taifa unaanza kushuka kwa sababu ya upuuzi wa hii timu.
si mlishangilia sana malinzi kufungwa mkadai ndo ameharibu soka, mkasema raisu was sasa ndo jembe. sasa mnalalamika nini kwa unafiki watz hamtakaa mwendelee
 
Kilimanjaro stars ndo ya taifa au ? Ndo maana malinzi alikuwa anayapiga ela hayana faida
 
HATUTAKIWI KUILAUMU STARS....sema ilitakiwa washiriki michezo ya reds na kukanda ngano..uko wangefanya vizuri...au ingekua kosi la waganga wa kienyeji
 
Hawa wachezaji sidhani Kama niwatanzania tunafungwaje siku ya uhuru? Kweli majeshi ya kukodi hayawezi kukomboa nchi.
 
Back
Top Bottom