Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Kilimanjaro, imezuia Sh329 milioni zilizopangwa kutumika kununua jenereta mbili kwa ajili ya iliyokuwa Mamlaka ya Uendeshaji na Uendelezaji wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Kilimanjaro (KADCO), baada ya kugundua kuwa hazina ubora unaotakiwa.
Akizungumza kuhusu ripoti ya robo ya kwanza ya mwaka leo Jumatatu, Novemba 11, 2024 Naibu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Kilimanjaro, Sabas Salehe, amesema jenereta hizo zilikuwa na matatizo, ikiwemo injini zenye kutu na sehemu nyingine kupakwa rangi tu, ili kuficha hali yake.
Soma Pia: TAKUKURU Dodoma yakamata Tani 120 za Nondo zisizo na ubora zilizopangwa kujenga Barabraba ya Ihumwa-Bandari Kavu
"Tulipofanya ufuatiliaji, tulibaini kuwa Kadco ilikuwa inakusudia kununua jenereta mbili kutoka Kampuni ya African Power Machinery (APM) kwa gharama ya Sh328.4 milioni," amesema Salehe.
Amefafanua kuwa jenereta hizo zilizowasilishwa zilikuwa na kasoro kama vile nyaya tofauti na injini zilizochakaa.