Kilimanjaro: Wanawake wakimbia makazi yao kukwepa wabakaji

Kilimanjaro: Wanawake wakimbia makazi yao kukwepa wabakaji

Hilo kundi la TELEZA kuna wakati lilisikika kuendesha oparesheni zake Kigoma.

Watakuwa wamefungua tawi lao Kilimanjaro!
Arusha pia niilisikia kama mwanzoni mwa mwaka huu.
Sema huku watu walikuwa wanasema ni mtu mmoja eti anateleza anapita ndani hata kama mlango umefungwa anakubaka then anaondoka.
Mimi nilijua ni story za kusadikika kumbe kuna ka ukweli sema tu labda watu waliongezea chumvi.
 
Baadhi ya Wanawake wa Kijiji cha Shirimatunda, Kata ya Mnadani, Wilaya ya Hai wamekazimika kukimbia makazi yao kutokana na kuibuka kwa wimbi la Wanaume wanaofanya vitendo vya ubakaji.

Matukio hayo yanadaiwa kutokea katika maeneo ya mtoni wakati Wanawake wakifuata maji, ambapo wanaofanya tukio hilo wanajulikana kwa majina ya ‘Teleza’

Wanawake wa Kijiji hicho wametoa malalamiko yao hayo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Stephen Kagaigai wakati alipofanya ziara wilayani humo kukagua miradi ya maendeleo. Baada ya kupata malalamiko hayo, Kagaigai amemuagiza RPC wa Kilimanjaro, Simon Maigwa kushughulikia tatizo hilo.

Mtendaji wa Kata ya Mnadani ajili ya ziara ya Sembuli Mkilaha amelikiri kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi na kuyafikisha kwenye mamlaka husika ya wilaya hiyo.

Naye, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amesema ataunda kamati kuhakikisha wanaofanya vitendo hivyo dhidi ya Wanawake wanakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Kilimanjaro zamani ilikuwa ni walevi wa mbege tuu ila kwa sasa imekuwa kambi ya mavijana majinga majinga yanayovuta mibange na kunjwa gongo na kufanya uhalifu wa hovyo. Hasa maeneo ya vijijini wilaya zote Kilimanjaro
 
Back
Top Bottom