JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imeongeza muda wa kujiandikisha kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa wakazi wa Kijiji cha Kikelelwa Kata ya Tarakea Motamburu wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro hadi Oktoba 28,2024.
Taarifa hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu baada ya kutembelea kituo cha kujiandikisha cha Josho, ambapo watu wasiojulikana wameiba vitabu viwili vya kujiandikishia vikiwa tayari na majina ya watu waliojiandikisha.
Babu amesema tukio hilo limetokea usiku wa Oktoba 18,2024 ambapo ameagiza kutafutwa kwa wahusika ili hatua kali zichukuliwe dhidi yao.
Tayari vitabu hivyo viliishaandikisha wakazi 1,105 wa Kijiji cha Kikelelwa, hivyo kuongezwa kwa muda huo kutawapa nafasi ya kujiandikisha tena.
Mbali na tukio hilo, Babu pia ametembelea kituo cha Lokoro kilichopo katika Kijiji cha Kikelelwa ambapo watu wasiojulikana wamechoma moto ofisi ya Mtendaji wa kijiji ambapo daftari la waliojiandikisha lilikuwemo ndani, hivyo kuunguza nyaraka hizo na nyingine za Serikali.
Chanzo: TBC