Kilimanjaro: Wawili wakamatwa wakidaiwa kuzushia ugonjwa viongozi wa Serikali

Kilimanjaro: Wawili wakamatwa wakidaiwa kuzushia ugonjwa viongozi wa Serikali

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro linawashikilia watu wawili wakituhumiwa kwa kosa la kusambaza taarifa za uzushi kwenye mitandao ya kijamii kuwa viongozi wakuu wa serikali ni wagonjwa, kinyume na Sheria ya Makosa ya Mitandao.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Ronald Makona leo Jumatatu Machi 15,2021,watu hao walikamatwa kwa nyakati tofauti.

Amewataja watu hao kuwa ni Peter Pius Silayo (30) Mkazi wa Tegeta Dar es Salaam, ambaye alikamatiwa eneo la Kibaoni Tarakea Wilaya ya Rombo na Melchiory Prosper Shayo (36) mkazi wa Keni Wilaya ya Rombo.

"Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro limemkamata na kumshikilia Peter Pius Silayo na Melchiory Prosper Shayo kwa kosa la kusambaza taarifa za uzushi kwenye mitandao ya kijamii kinyume na Sheria ya makosa ya Mitandao kuwa viongozi wakuu wa Serikali ni wagonjwa," amesema

Kamanda amesema watuhumiwa watafikishwa mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika.

Aidha, Jeshi la Polisi mkoani hapa limetoa wito kwa jamii na wananchi kwa ujumla kuacha kusambaza taarifa ambazo hazina ukweli, na kwamba hatua kali zitachukuliwa kwa wale watakaobainika.

"Hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa mtu yeyote atakaebainika ametoa au amesambaza taarifa za kupotosha umma na kusababisha taharuki kwa jamii"

Chanzo: Mwananchi
 
Kwahiyo wanaokamatwa ni wale waliowazushia viongozi wa serikali tu?
 
Hii kamatakamata itaendelea tu as long as hao viongozi wakuu wataendelea kujichimbia kwa wiki kadhaa. Mwisho wa siku hata hao wakamataji wenyewe wataanza kuhoji.

1615797169437.png
 
kweli nmeamini kuna tofauti kati ya kuwa kiongozi wa serikali na kuwa mwananchi(mnyonge)
 
Basi ma RPC wengine wanaona hawafany kaz nao wataanza kamata kamata hovyo
 
Nakuwa na mashaka pia kwamba wasemayo labda yana ukweli. Kwani tatizo liko wapi mzee akijitokeza?
 
TLS iwe mstari wa mbele kutetea wananchi ambao wanageuzwa adui wa serikali yao wenyewe huku katiba ya nchi ikisiginwa.
 
Back
Top Bottom