SoC01 Kilimo cha Alizeti ni Utajiri

SoC01 Kilimo cha Alizeti ni Utajiri

Stories of Change - 2021 Competition

MTEGULE

Member
Joined
Jul 16, 2021
Posts
15
Reaction score
22
PATA FAIDA KUBWA KUPITIA KILIMO CHA ALIZETI. KWA MTAJI WA LAKI MOJA NA AROBAINI (140,000) KWA HEKALI MOJA NA KUPATA ZAIDI YA MILLION MOJA NA LAKI NNE (1400,000/=) KWA SIKU TISINI (90).

Ndugu Wapendwa hapana shaka ya kuwa mnaendelea vyema na ujenzi wa Taifa letu pendwa la Tanzania.Ikiwa ni tofauti basi Mungu akufanyieni wepesi na mrudi katika hali zenu njema za awali.

Leo ningependa kuwapa mbinu au njia bora ya kuongeza kipato kwa kulima zao la alizeti kwa kutumia kiwango kidogo mnoo cha pesa ambacho ni laki na arobaini tu (140,000/=) na kuweza kupata faida zaidi ya millioni moja na nusu (1500,000/=) kwa siku tisini (90).Natambua kuwa una hamu na shauku ya kutaka kufahamu ni kwa namna gani kilimo hichi kinafanyika.

Alizeti ni miongoni mwa zao muhimu sana ambalo hutoa mafuta mazuri yasiyo na lehemu kwa ajili ya matumizi ya mwanadamu ya kila siku. Alizeti ni zao linalolimwa hasa maeneo ya ukanda wa kati hapa Tanzania kama vile Dodoma, Singida, Manyara na hata Tabora.

Alizeti ina sifa ya kustahimili ukame na ndiyo maana utaona hata mikoa ambapo hulimwa zao hilo haina sifa ya uwepo wa mvua nyingi.

Zao la alizeti limekua na soko kubwa mnoo hapa Ulimwenguni kutokana na uhitaji wake mkubwa, sambamba na hayo mwaka 2017 Tanzania ilitangazwa kuwa ni nchi ya pili katika uzalishaji wa zao la alizeti hapa barani Afrika.

Moja kwa moja nielekee na nieleze ni kwa namna gani unaweza kutumia mtaji kidogo sana na kuongeza faida maradufu ndani ya siku tisini.

Katika jimbo la Kibakwe, wilaya ya Mpwapwa iliyopo mkoani Dodoma..hii fursa adhimu ndipo inapatikana.Kwanza ifahamike kwamba katika vijiji mbalimbali vinavyopatikana jimbo la Kibakwe mfano.Chamtumile,ikuyu,chogola,winza,makose n.k) ardhi kwa ajili ya kilimo cha alizeti inapatikana ya kutosha na ni kwa bei rahisi mnoo.

Mchakato wenyewe uko hivi:

(i)Mbegu nzuri lita 2 ni Tsh 20000/=

(ii) Kukodi shamba hekali moja ni Tsh 20,000/=

(iii) Kusafisha shamba(Kuberega) hekali moja ni Tsh 10,000/=

(iv) Kulima na jembe la plau (Kutifua) hekali moja ni Tsh 20,000/=

(v)Palizi ya kwanza na ya pili..ni Tsh 20,000/= kwa hekali moja.

(vi) Kukata, kuzipiga, usafirishaji mpaka mashineni ni Tsh 50,000/=.

Jumla ya gharama zote ni Tsh 140,000/= .

Kwa kawaida hekali moja ya alizeti hutoa gunia 12 hadi 15 kwa makadirio ya chini. Na katika maeneo ya huko huko zipo mashine maalumu kwa ajili ya kukamua alizeti na bei yake huwa ni chini sana na kama unayaacha mashudu huwa hakuna tozo yoyote.

Lakini pia, ifamike kwamba Gunia moja la alizeti ambazo huwa ni debe 6 tu. Hutoa mafuta kuanzia lita 18 hadi 25(Kwa makadirio ya chini) kutokana na vile alizeti ilivyokomaa.

Hivi sasa lita moja ya alizeti ni Tsh 7000/=kwenye maeneo mengi ya mjini lakini tujaalie wewe utauza kwa Tsh 5000/= kwa lita kwa sababu ni mali yako toka shamba.

Ikiwa umepata gunia 13 kwa hekali moja, kila gunia ukapata lita 22 za mafuta(Kwa makadirio ya chini) utakuwa na lita jumla 286 ukizidisha kwa (5000/=) utapata Milioni moja laki nne na elfu thelathini TSH 1430,000/=

Tsh 140,000/= Hadi Tsh1430,000/=

Faida iliyopatikana ni milioni moja laki mbili na tisini Tsh 1290,000/= kwa siku tisini (90).

Naomba kuwasilisha.
 
Upvote 12
Hizo namba hazina uhalisia kabisa
mimi nalima pia lakini hapa umetupiga CHANGA
 
Ukumbuke hayo mapato ni kwa kilimo mseto yaan amechanganya mazao ma5 kama sijakosea kwenye shamba moja
 
Hata kama mtu akalima alzet tu kwa kisasa kupata kupata gunia 12 au 15 ni kaz ngum sana akijtahd san 6 had 8 labda kama ukubwa wa eka unatofautiana lakn eka ya miguu 70 kwa 70 hata gunia 10 haiwezekan
 
Hata kama mtu akalima alzet tu kwa kisasa kupata kupata gunia 12 au 15 ni kaz ngum sana akijtahd san 6 had 8 labda kama ukubwa wa eka unatofautiana lakn eka ya miguu 70 kwa 70 hata gunia 10 haiwezekan
Kwa dodoma msimu wa kuanza kulima alizet uwa ni lin ?
 
Kwa kilimo Cha alizeti ninachokifahamu hekati Moja kutoka magunia ZAIDI ya Kumi...ni maaajabu ya Dunia!
 

MTEGULE

hujarudi tena Mkuu kilio ulichokishadadia cha alizeti kilikuwa ni cha kwenye makaratasi km kile cha matikiti
huko kwenu wametukodisha shamba la eka 50 kumbe wanajua imetukata hasa
waambie kuna siku watatokea na panga ni wizi kumtumainisha mtu kua atapata kunia 10 kwa wka
hebu rudi tuambie umepata gunia ngapi kwa eka? na faida yako maana wenzako wameshavuna
 
Sio mkulima tu bali uwe mkulima wa kutegemea mvua..hakuna rangi utaacha kuiona.

#MaendeleoHayanaChama
Mkuu Tanzania kilimo cha kumwagilia bado sana
Watu wanacheza na hizo hizo mvua na wametoboa

Tatizo ni kwamba asilimia 60 ya watanzania ni wakulima wa kilimo cha kulisha familia zao na ziada ndio wanauza na akilima sana ni eka 5........kama unawazungumzia hawa basi upo sahihi

Wewe amini hivyo lakini wapo watu wapo serous na kilimo na wametoboa
 
Umewahi kulima mkuu ?
Mayu mm nasubiri mavuno yako na udadavue matumizi na mapato
kule post #1 huaweka updates za sasa km palizi ni ngapi kwani km wewe huwezi palilia peke yako wala kuwasimamialazima watakutoroka
naungana na wenzangu hakuna kazi/biashara mbaya kama kilimo cha kutegemea mvua, TAFADHALI UKIVUNA TUWASILIANE
Nina eka zaidi ya 15 huko West Kilimanjaro naziuza mwenye kuzihitaji aniPM
 
Mayu mm nasubiri mavuno yako na udadavue matumizi na mapato
kule post #1 huaweka updates za sasa km palizi ni ngapi kwani km wewe huwezi palilia peke yako wala kuwasimamialazima watakutoroka
naungana na wenzangu hakuna kazi/biashara mbaya kama kilimo cha kutegemea mvua, TAFADHALI UKIVUNA TUWASILIANE
Nina eka zaidi ya 15 huko West Kilimanjaro naziuza mwenye kuzihitaji aniPM
Mkuu sina cha kuficha nimeamua kulima kweli kuwa mfano
Kaangalie kwenye post yangu nimeweka gharama zote nilizotumia so far na bado sijavuna
 
Mkuu sina cha kuficha nimeamua kulima kweli kuwa mfano
Kaangalie kwenye post yangu nimeweka gharama zote nilizotumia so far na bado sijavuna
Sorry Mada zimejichanganya na ya MTEGULE ambaye yeye naye kaandika na sio katenda kwa kupalilia anadai palizi ni sh 20.000 kwa eka ni kweli
Kwenye Mada yako hujatuwekea ulilipa sh ngapi ulipopalilia palizi zako Mrejesho wa mwisho ni 24 March
lkn makadirio umeweka kwenye karatasi ni 50,000 kupalilia kwa eka
Mbegu (ASA)
80 x 5,000 = 400,000
Kupanda
20 x 30,000 = 600,000
Palizi
20 x 50,000 = 1,000,000
Mengineyo
1,000,000
Jumla kuu 4,500,000
ndio maana nikakuomba update ya palizi 2 mwezi April hujaweka hiyo 20x50,000=1,000,000/ x2 = 2M hujaweka bado unalima kwenye karatasi
 
Back
Top Bottom