Kilimo cha Alizeti (Sunflower): Masoko, Mbinu na Ushauri toka kwa wadau

Naomba msaada kwa wataalam waliokwisha kulima na zao la Alizeti wanapambana vipi na ndege, maana naona watamaliza juhudi zote nilizoweka mwaka huu.

Wako wengi na wanashambulia mazao kweli kweli.
Sijawahi kulima alizeti lakini nina wazo. Hivi ukinunua waya mrefu sana na kuunganisha spika sehemu zote za shamba halafu ukakaa kwenye kona na mic wakija unafoka ''toka toka, kamata kamata, piga piga'' haitasadia? Au gharama itakuwa kubwa?
Au unanunua drone unabana kwenye kona ya shamba, ukiona wanakuja unawafuatilia na drone na kuwakimbiza kama ndege mkali anavyofukuza wengine..
 
hahahhaha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna njia nyingi sana za kupambana nao. Wengi huwa wanahamia shambani na kufanya kazi ya kufukuza ndege, veta nahisi wana vifaa vinaweza fanya hivyo na njia nyingine hakikisha ukitaka kulima alizeti na wenye mashamba ya eneo hilo wanailima pia ili mgawane hao ndege kwenye mashamba yenu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alizeti huwezi lima peke yako! Ukilima peke yako ndege wote ni wa kwako peke yako. Mkilima wengi ndege walewale mtagawana wengi na wengine hawawezi kufika huko shamba lako lilipo maana watakua wameshashiba

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aiseh pole sana
Mziki wa ndege unazidi ule wa viwavi
Kwenye mpunga au mtama ungekubali
 
Naomba msaada kwa wataalam waliokwisha kulima na zao la Alizeti.

wanapambana vipi na ndege maana naona watamaliza juhudi zote nilizoweka mwaka huu maana wako wengi na wanashambulia mazao kweli kweli.
Hii nilioona nanenane mby.Tafuta net zilizochoka funga kila tunda lililoanza kukomaa.Ubunifu wangu binafsi maana nimepanga kulima ntakapotulia.Nitatafuta vifungashio laaini vyeupe,ntatoboa matundu na kuvifunga.Naomba ujaribu kidogo ila net uhakika imefanyiwa utafiti uyole Ila kuzipata net ndio ishu naomba ujaribu vifungashio.Mi ntajaribu miche michache ya majaribio, ninashamba porini kuna rutuba hatari najionea wivu rasimali imelala tu naogopa ndege.
 
Mkuu bado unaendelea na hii shughuli?
 
Jamani nilikuwa naomba kujua bei ya machine za kukamulia alizeti kupata mafuta mpaka ku purify, nimeona uko juu kua za india ndo ziko vizuri zaidi, ningependa kwa anaejua anipe bei zake, full set na za sido pia full set. natanguliza salam namaliza na shukrani.
 
Alafu pimbi 1 anajitokeza eti kufuta maonesho ya nane nane sijui huwa wanatumia nini kufikiria
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…