Kilimo cha Alizeti (Sunflower): Masoko, Mbinu na Ushauri toka kwa wadau

Kilimo cha Alizeti (Sunflower): Masoko, Mbinu na Ushauri toka kwa wadau

Wakuu naamini mko poa naomba kama kuna mtaalamu unajua kilimo cha vanilla anipige shule nataka nijaribu kuna mahali nimepata soko
 
Alizeti ni zao zuri sana la biashara linalimwa sehemu nyingi nchini kwetu ila mimi najua Iringa inaongoza,pia Dodoma na Singida nako wanalima sana tu.

Ukipata shamba zuri ekari moja ya alizeti huweza kukupatia kati ya magunia5-10 kutegemeana na aina ya mbegu uliyotumia na pia namna shamba lako ulivyolihudumia.

Gunia moja la alizeti yaani madebe sita huweza kutoa lita 20 za mafuta baada ya kusafishwa,mafuta haya unaweza kuuza kati ya shilingi 28,000-36000 kwa ndoo ya lita 20,pia utaweza kuuza mashudu yako ya alizeti kwa wafugaji.

Ukiwa wewe ni mfanyabiashara mzuri na una mtaji mkubwa fuata ushauri wa ama kwa kununua mashine ya kukamua alizeti kwani ukiwa na mashine hii itakulipa zaidi kwani utauza product yako mwenyewe yenye label ya kiwanda chako,this is very common in Singida,Iringa and in Mpwapwa-Dodoma.

Kama mnataka mali mtayapata shambani, braza umesahau shairi hili la darasa la nne enzi zile?
5*20=100*28-36000=280-360000
Zao hili halina bela msililime kama ni hivi
 
5*20=100*28-36000=280-360000
Zao hili halina bela msililime kama ni hivi
Umeangalia hizo data ni za mwaka gani kiongozi??


Dumu la Lita 20 mafuta ya alizeti Dodoma bei ni elfu 48 wakati huu wa mavuno. Huko mbeleni tegemea bei kupanda marudufu mpaka elfu 60 kuendelea.


Jamaa uliyem quote ni wa 2010, this is 2017
 
Wakuu kama kichwa cha habari apo juu.
Naomba kujulishwa ama kuelekezwa jinsi ya kulima kwa ufanisi na ubora zao la alizeti na kupata mavuno makubwa. Na ningeomba nijue soko lake pia. Tuanze kwa mfano wa shamba la ekari mbili. Karibuni wajuzi
 
Wakuu kama kichwa cha habari apo juu.
Naomba kujulishwa ama kuelekezwa jinsi ya kulima kwa ufanisi na ubora zao la alizeti na kupata mavuno makubwa. Na ningeomba nijue soko lake pia. Tuanze kwa mfano wa shamba la ekari mbili. Karibuni wajuzi
Kama uko kagera,shinyanga,singida dodoma tuwasiliane nikwambie soko lilipo
 
Ni kweli kabisa masaki, kulima kwa kutegemea kudra za Mungu mvua inyeshe, wadudu wasishambulie, wezi wasiingie kuanza kuvuna kabla wewe huvuna n.k n.k.

Kwa kweli ukulima kwa ujuma ni adha, na si adha tu lakini ni risk kubwa sana kwa mtaji wako. kwa uzoefu mdogo nilionao kupitia watu wa karibu wanaofanya biahsara hizi wanasema ni bora wakusanye pesa za kutosha, kununua alizeti msimu wa mavuno kwa wingi na bei huwa rahisi, then ukamue mwenyewe mafuta na pia unaweza ukauza akiba uliyokusanya msimu ambao zinahitajika kwa bei nzuri inalipa kuliko kulima mwenyewe.

The same applies to mpunga/mchele hasa maeneo ya ifakara ambako wachuuzi hupata faida kubwa kuliko wakulima.
Sasa t
1. Tafuta shamba
2. Lima
3. Mavuno hifadhi ghalani i.e usieze kwa walanguzi
4. Nunua mashine ya kukamua alizeti
5. Kamua alizeti zako
5. Uza mafuta nje ya nchi.
6. Pata faida

Mashine za kukamulia alizet huuzwa shilingi ngapi kama unajua naomba niambie.
 
kiboka ya Alizeti mvua.....na yenyewe inasubiri mazao yakishapendeza inashuka ya kufa mtu walah
 
Naomba msaada kwa wataalam waliokwisha kulima na zao la Alizeti wanapambana vipi na ndege, maana naona watamaliza juhudi zote nilizoweka mwaka huu.

Wako wengi na wanashambulia mazao kweli kweli.
 
Naomba msaada kwa wataalam waliokwisha kulima na zao la Alizeti.

wanapambana vipi na ndege maana naona watamaliza juhudi zote nilizoweka mwaka huu maana wako wengi na wanashambulia mazao kweli kweli.
 
Back
Top Bottom