Mashine zinapatikana sido na kwa wahindi. Nimemnunulia mjombangu mashine moja kwa milioni nane pamoja na filter ina mabomba kumi na mbili. Igembe Nsabo nisaidie, Unauza lita ishirini za mafuta kwa bei gani. Nadhani bei ya shilingi 2,500 kwa lita itakupa shilingi elfu hamsini kwa lita 20. Naogopa kidogo, Kuhusu kulima wengi wanalima kwa njia za asili. Ukilima kitaalam, utapata tani nne za alizeti kwa ekari moja. Huende ukishirikisha wataalaam utalima kwa faida. Mimi nimefanya utafiti wa kilimo cha mpungu cha umwagiliaji. Ekari moja gharama yote ni shs 300,000. Mavuno ni magunia 40 minimum. Una uhakika wa kuuza shs 2,500,000 kwa ekari moja. Kilimo ni ukombozi ni vizuri tunaopenda kilimo tulime sehemu moja ili kupunguza gharama. Tuchangie gharama za mtaalam, gharama za kusafirisha pembejeo na hata usafiri wetu wa kwenda na kurudi shamba.