Matanzia kizebazeba
JF-Expert Member
- Feb 12, 2013
- 654
- 630
Unataka kuwekeza mkoa gani? Kwa ufahamu wangu mimi alizeti ni zao bora sana ukiachana na swala la soko hata wewe mwenyewe unaweza ukazalisha mafuta kama kwa Dsm bei ya sasa dumu la lita tano ni elfu kumi na saba wewe wekeza kwa speed zote zao la alizeti ni zuri sana
Ahsante mkuu wangu, je zao hilo lahitaji pembejeo pia kama vile mbolea, madawa kupulizia ama nawezaje kulimudu?
ukitumia ile mbegu ya miezi mitatu, waweza kuweka mbolea aina ya DAP (nilitumia mimi kule isanza-mbozi-mbeya) na dawa za kupulizia wadudu ni muhimu sana.
Unaweza kutufafanulia hii mbegu? Nataka kulima Handeni vipi itamea?
Samahani,Mashine zinapatikana sido na kwa wahindi. Nimemnunulia mjombangu mashine moja kwa milioni nane pamoja na filter ina mabomba kumi na mbili. Igembe Nsabo nisaidie, Unauza lita ishirini za mafuta kwa bei gani. Nadhani bei ya shilingi 2,500 kwa lita itakupa shilingi elfu hamsini kwa lita 20. Naogopa kidogo, Kuhusu kulima wengi wanalima kwa njia za asili. Ukilima kitaalam, utapata tani nne za alizeti kwa ekari moja. Huende ukishirikisha wataalaam utalima kwa faida. Mimi nimefanya utafiti wa kilimo cha mpungu cha umwagiliaji. Ekari moja gharama yote ni shs 300,000. Mavuno ni magunia 40 minimum. Una uhakika wa kuuza shs 2,500,000 kwa ekari moja. Kilimo ni ukombozi ni vizuri tunaopenda kilimo tulime sehemu moja ili kupunguza gharama. Tuchangie gharama za mtaalam, gharama za kusafirisha pembejeo na hata usafiri wetu wa kwenda na kurudi shamba.
Samahani,
Umesema kilimo cha mpungu ama mpunga?
Pia umesema kwa heka ni laki ama?..hii ni pamoja na kukodi shamba?..Kama sio pamoja na shamba Ukijumlisha na cost za kukodi itafika shiling ngap??
Pia haya maeneo yanapatikana wp??
Lclfkiiiiiii7uc7ukx8iickkkkjjjfjfjfjfjjjjjjjjjjjdckkñmñ9iupuo