Hongera ndugu kwa hatua kubwa uliopiga, mambo ya kuzingatia katika kilimo:-
1. Fanya uchunguzi juu ya soko la zao lolote kabla ya kulilima, hii itakusaidia kuangalia matazamio ya faida. Wengi huwa tunakosea tunaanza kulima then tunakuja kutafuta soko usifanye kosa hilo.
2. Andaa pembeje za kilimo unachotaka kukifanya (mbegu, madawa) na pesa ya dharula. Mimi ningekushauri ununue mbegu za kampuni hizi mbili PV Holland na Royal na ulime nusu heka kampuni moja na nusu nyingine kampuni nyingine. Sababu kubwa ya kukwambia hivi hii itakusaidia na kukupa uhakika ni aina gani ni nzuri na bora kuliko nyingine, ninamaana hapa wewe mwenyewe utajua mbegu gani inawahi kuzaa mapema, mbegu gani haishambuliwi na magonjwa na nimbegu gani utaichuma kwa muda mrefu wakati wa kuvuna, hii muhimu sana kuweka kumbukumbu ya kuandika siku ulipopanda.
3. Ingia kwenye kilimo sasa sana uwe unachunguz a mazao yako mara kwa mara maranyingi dawa hupuliziwa kila baada ya wiki 2, inategemea na geographia ya eneo husika.
4. Naamini ukizingatia hayo utafanya vizuri utakapo lima awamu yapili kwasababu utakuwa umepata uzoefu wa kilimo na changamoto ulizopitia. Bamia kupanda hadi kuanza mavuno ni siku 45 mpaka 60.
Nisikuchoshe na maelezo marefu mimi pia najifunza naamini wapo wengine wajuzi zaidi watajazia au kurekebisha pale nilipokosea.
Nakutakia kila lakheri na mafanikio.
Sent from my LG-H635 using
JamiiForums mobile app