SoC03 Kilimo cha mabadiliko kitasaidia

SoC03 Kilimo cha mabadiliko kitasaidia

Stories of Change - 2023 Competition
Joined
May 24, 2016
Posts
15
Reaction score
10
Transformational agriculture.png


DUNIA inabadilika pale miaka inaposogea, ya sasa siyo ya jana. Tuanapozungumzia mabadiliko tunazungumzia tabia ya nchi, mambo ya leo siyo yatakayokowepo kesho na siku zijazo baada ya kesho.

Mabadiliko ya nchi si neno geni sana, kila mtu anafahamu na athari zake. Na Dunia imetuletea msamiati katika nyakati hizi unaitwa mabadiliko ya tabianchi. Vipindi na nyakati za hali ya hewa haziendi kama zilivyokuwa mwanzo.

Kuna kuchelewa na kuwahi mvua za vuli na hata za masika. Na imesababisha athari si kwa Wanadamu tu, bali hata kwa viumbe wengine.



Katika makala hii tutaenda kuona jinsi kilimo cha madailiko kikifuatwa na wakulima kinavyoweza kusaidia kuongeza mapato katika mazao na kuboresha hali ya maisha.

Naamini kuna baadhi ya maeneo wameshaanza kunufaika na kilimo hiki. Kama wameweza kuchukua hatua madhubuti hizi tunazokwenda kujadiliana hapa.

Bila kupoteza muda hebu tuingie kwa kina kuangalia, nini wakulima wanatakiwa kufanya kwa msaada wa mtandao nimeweza kupata taarifa hizi.

Kwanza kabisa katika kuendana na mabadiliko ya tabianchi, wakulima wanashauriwa kuelewa matokeo haya ambayo yanatokea sasa;

- Kuanza kwa msimu wa mvua

Hapa kila mtu anafahamu ameshuhudia kwasasa msimu wa mvua unaweza kuwahi au ukaanza kwa kuchelewa kulingana na jinsi mwaka utakavyokuwa. Maana matokeo ya tabianchi yana miaka kadhaa mpaka sasa tangia yalipoanza kwa mara ya kwanza.

Wataalamu wa mambo ya hali ya hewa wanasema baada ya joto la sayari ya Dunia kupanda kwa nyuzi 2 katika kipimo cha Farenihaiti mwishoni mwa karne ya 19. Hiyvo wakulima wanashauriwa kuwa makini kati hili, ili waendane na wakati waweze kufanikiwa katika shughuli zao.

- Kipindi cha msimu wa mvua

Mzingatio katika hili ni kwamba kipindi hiki cha msimu wa mvua, hakitabiriki kinaweza kuwa kirefu au kifupi. Hivyo mkulima awe macho na awe amejiandaa na kukabiliana na lolote kati ya hayo mojawapo.

- Kiasi cha mvua

Mkulima anatakiwa ajue kuwa kiasi cha mvua kinaweza kuwa cha kawaida, cha mvua za kutosha au cha mvua nyingi kuliko kawaida. Au kinaweza kuwa cha mvua chache chini ya kiwango cha kawaida.

Hili litasaidia kama mkulima atakuwa amejua mapema atakuwa amejiandaa na kuchukua hatua itakayomsaidia kufanikiwa katika kilimo chake.

Kipindi cha ukame

Hapa napo inatakiwa ifahamike na wakulima kuwa kipindi cha ukame kinaweza kuwa kirefu au cha muda mfupi. Kama atakuwa amejua mapema hatua za kuchukua pia atakuwa amejiandaa nazo.

Kadhalika, wengi wanaweza kujiuliza taarifa hizi mkulima anaweza kuzipata wapi? Swali zuri na la msingi. Kwa Dunia ya utandawazi kuna vyombo vingi vya habari ambavyo vimekuwepo katika matumizi kuliko ilivyokuwa hapo nyuma.

Twende pamoja, chanzo kikubwa ambacho ni cha muda mrefu zaidi ni redio, lakini pia kwasasa kuna televisheni(Luninga), magazeti, kuna simu za mkononi, kuna kufuatilia mitandao ya kijamii na kuna maafisa ugani katika kila kata hapa Tanzania.

Ili kilimo cha mabadilko kiweze kusaidia wakulima katika uzalishaji, wanatakiwa kuzingatia baadhi ya mambo kama tunavyokwenda kuyaainisha.

Kuna wakati, kabla ya msimu wa mvua mkulima anatakiwa kuwa amefanya maamuzi ya kujiandaa kwa ajili ya msimu, afanye hivyo kabla msimu kilimo haujaanza.

Kuna kipindi, wakati wa msimu wa mvua, wanatakiwa wakulima kufanya maamuzi ya shughuli za kufanya shambani, kama wakati wa kupalilia magugu lazima wawe tayari kufanya. Wakati wa Kuweka mbolea wawe tayari na mbolea ziwepo, wakati wa kutandaza majani.

Kadhalika, wakati wa kuvuna maji ya mvua na hatua za kukabiliana na majanga na kupunguza athari zinazoweza kujitokeza. Mkulima anashauriwa kufuatilia utabiri wa hali ya hewa wa siku kumi kabla na wa kila siku katika shughuli zake zote za ukulima.

Hata hivyo, kuna wakati baada ya msimu wa mvua. Baada ya kufikia mwisho wa msimu wa mvua, mkulima anashauriwa kuangalia mazao na malisho ya mifugo kwa kawaida huwa katika hatua ya ukomavu na ni kipindi kizuri cha kuvuna, kuhifadhi na kusafirishwa kama yanafaa kwenda sokoni.

Katika hatua hii, mkulima anaweza akapatwa na changamoto zinazohusiana na uhifadhi na utunzaji baada ya kuvuna ili kuhakikisha usalama na ubora wa chakula. Kama atakuwa amefanya mambo kwa kuzingatia ataweza kukabiliana na Changamoto hizi mapema na kwa wakati.

Kwa kuongezea kuna maamuzi muhimu mkulima wa kilimo cha mabadiliko anatakiwa kufanya katika kilimo cha mazao kulingana na taarifa za hali ya hewa atakazokuwa anazipata. Maamuzi ya wakati gani na jinsi gani ya kuandaa shamba kwa ajili ya kupanda.

Hapa anashauriwa maamuzi haya yafanyike wiki mbili kabla ya kupanda, kwa wale wanaotegemea kilimo cha mvua. Anatakiwa pia afanye maamuzi ya jinsi ya kuhifadhi maji na udongo, aina za mazao na mbegu za kupanda.

Pia afanye maamuzi ya kiasi cha mbolea cha kutumia. Aende mbali Zaidi kwa kuamua wakati na jinsi gani ya kutumia mbolea hizo.

Vile vile aangalie na kuamua wakati na jinsi gani ya kupanda. Muda pia na jinsi gani ya kudhibiti magugu ni jambo la kuzingatia. Aina za wadudu waharibifu na magonjwa na jinsi ya kudhibiti maamuzi haya yawe ya mapema na kufanyika kwa wakati husika.

Bila kusahau maamuzi ya muda wa kuvuna na jinsi gani ya kuhifadhi mazao. Mwisho kabisa ni kuamua wakati na jinsi ya kuuza hayo mazao kama ni kwa ajili ya kazi hiyo.

Mkulima akizingatia hayo yaliyomo katika Makala hii, kilimo cha mabadiliko kinaweza kuwa cha tija katika familia yake lakini katika kuleta mabadiliko katika sekta ya kilimo na kuweza kuongeza pato la taifa. Na kuifukuza njaa katika mipaka ya nchi yetu kabisa.

Au unasema msomaji na mwana kwetu Mtanzania, mzawa, mzalendo? Kuna cha kuongeza, ushauri, maoni. Nione maoni yako katika sehemu ya maoni hapo chini. Karibuni!
 
Upvote 2
Back
Top Bottom