Kilimo cha maembe ya kisasa

Pole sana lakini shida yenu watu hamfanyi utafiti wa mda gani nilime zao hili au lile. Kwa bongo kanuni ni Moja tu Lima kitu kipindi bei ikiwa ndogo usilime kipindi zao flani Lina bei kubwa kwanini? Nikupe mfano kipindi unalima kitunguu nafaham kabisa kuipata mbegu tu ilikuwa mtihani kwani ilikuwa haipoi ikifika dukani imeisha swali, wapi inaenda ni shambani kwani mbegu hailiwi. Sasa kwanini upande msimu ambao bei ni ndogo, mfano msimu huu baada ya watu wengi kulima kitunguu na kuwakata kwenye bei basi asilimia 80 hukata tamaa kutokana na kupata hasara au kutofika matarajio hivyo ukilima sasa ndio soko litakuwa zuri
 
Na the best Kilimo ni Permanent Crops....yanazaa kila mwaka utakunata tu na soko zuri kipindi fulani...TULIME embe ndugu zangu
 
Hivi hakuna njia ya kitaalam yakufanya maembe yaive katka msimu tofaut na huu wa kawaida ili mtu apge pesa kivyake vyake
Zipo unafanya induction ya enzyme kwa kupulizia hivyo miti inaanza kuzaa na unafanya intensive irrigation,fertilization ili mambo yawe mazuri
 
Ili ufanikiwe katika jambo lolote unatakiwa ulifanye tofauti
 
Sasa si bora aliseme tumbaku kwa heka 10 anakuwa amezidi
 
Tango wengine wanaita tanga ni moja ya embe zinazohitajika zaidi viwandani
embe tango ni zile embe za tabora(wengine huziita boribo za tabora), embe tanga ni hizi embe zinatoka tanga(kule tanga wanaziita viringi(kwa umbo lake la mviringo))
 
Mkuu Bara Bara ya 5, unaendeleaje...umefanikiwa kuanza?

Nakushauri pia ujiunge na chama cha wakulima wa embe AMAGRO-Association of Mango Growers.

Kule utapata network ya kujuana na wakulima wenzio kama mimi na pia kupata utaalamu wa kilimo cha maembe kutoka kwa wakulima wazoefu.

Karibu sana kundini-mtafute katibu wa chama Mzee Mkopi @ 0715-312 036(nami nilipata habari zake humu JF zamani kidogo).

Kila la kheri-ni safari yenye matumaini ingawa kuna changamoto nyingi ndani yake!
 
Asante sana Mkuu...Nimeshapanda miche 450 kwa spacing ya 10x10m. Mzee Mkopi nimeongea nae na kanipa madini mazuri sana na AMAGRO nitajiunga very soon. Niko mbioni kuongeza miche mingine 300 ya Keit ili msimu huu niwe nayo 750.Nashukuru niliyopanda Nov.24 imeshakamata na nataraji nitoe nylon na kuondoa matawi chini yake
 
Unajua nashangaa watu wanacha kupanda mikaribea wakati Haina gharama yoyote ya uendeshaji
 
Juzi tu nimeng'oa Miche ya nyanya nusu heka😄 nimenunua 🐓 hata week hajafikisha ameanza kutaga
 
Nimetoka shamba wiki hii,..nashukuru miche yangu 500 inaendelea vizuri ingawa kama 50 hivi imekufa. Nimeiwekea mbolea ya samadi na kuipalilia.
Wasi wasi wangu ni kama itavuka kiangazi hiki maana nimepanda kwenye ardhi ya kidongo ingawa imeshika na
inatoa majani mapya. Kama tafanikiwa kuivusha na kiangazi hiki,basi mwezi wa 11 mwaka 2025 taongeza mingine 500 ili niwe na 1000.
 
Reactions: Lax
Mkuu ingia gharama ya kumwagilia, mwaka huu mvua chache hata njombe ya mvua. Tafuta makopo ya maji kila mche makopo 4. Jaza maji toboa tundu yadondoke walau wiki moja. Tumia boda kubeba maji.
Huo mradi ushaenda kilichobaki ni kuboresha.
Tafuta mbolea ya HAKIKA ita bust haraka inauzwa 45elf kwa mfuko . Ina composite 25% hivyo ni kama samadi ilioboreshwa.
Uja piga picha miche? Tunafuatlia kwa karibu, waliokukatisha tamaa wataaibika soon.
Watoto wako hawata andamana kudai serikeli iwa ajili, umeisha waandalia ajira ya kudumu.Hayo mambo watanzania tunatakiwa kuyafanya,big up.
 
Hii mvua na mimi kuna miti imeteketea.
Hili wazo la makopo nalibeba. Maana nimetoka site leo tumeliongelea na hapa jukwaani napo nimelikuta
 
Asante sana Mkuu...hayo makopo yana ujazo upi??lita 1 au 0.5.??Vp na hiyo mbolea kwa Dar nitaipata wapi?
 
Nafikiri zoezi hili tulianza mwezi wa 8 maana kwa mujibu wa TMA mvua zitakata Mei.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…