Kilimo cha maembe ya kisasa

Kilimo cha maembe ya kisasa

0719527062
0757056472
Karibu mkuu ninapatikana 24/7
Lakini pia ipo Uzi hapa Jf ambao nimeelezea kwa kirefu kidogo kuhusu miche mbalimbali ya matunda.
Ukipata nafasi unaweza kuupitia pia Kwa maelezo zaidi
Embe nzuri za juice wanazotumia Azam au Sayona ni zipi? Asante
 
Mkuu karibu sana SUA tukuhudumie,tuna miche ya maembe aina Saba tofauti tofauti Kwa bei sh 2000 kila mche.
Tuna Aina zifuatazo
1.Dodo
2.Bolibo
3.Tommy
4.Kent
5.Alphonso
6.embe Tanga
7.red Indian
Ume graft ya hapa hapa TZ ?
 
Kwangu nilipanda kokwa la embe dodo miaka 6 iliyopita ndiyo mwaka huu umeanza kutoa matunda.
Mkuu kama mtu anapanda maembe akiwa late 20-30s hata akipanda kokwa itamlipa.
Mmea wa kuota kokwa unakuwa imara sana na lifespan itakuwa ndefu mpaka vitukuu.
Tujifunze kwa babu zetu mbona walipanda miti ya aina mbali mbali na tumekuta wakivuna, sisi tunashindwa wapi ? Tumeshikwa akili na wazungu kila kitu cha short cut.
Binafsi nimebadili mtazamo nataka nianze kupanda vitu vya asili. Nikipata eneo na uwezo hata mninga, mtundu , mvule nitapanda. Mungu katujalia ardhi inastawi kila kitu ila tumewekeza kwenye uharaka na ubinafsi. Mbona watu wa Iringa Njombe , Mbeya wanapanda miti na wanasubi6i miaka 15 ili wavune, kumbe inawezekana kuwa na subira.
I think nimekuwa enlighten kuhusu nature.
Tukishindwa sana basi tuchanganye ya grafting na ya kokwa au kienyeji. Watoto wetu watatuona watu wa maana sana kwakweli
 
Vp kuhusu umwagiliaji umejipangaje
Sitamwagilia,kwani napanada mvua za mwazo ambapo itapata maji kwa miezi zaidi ya 7,then ubichi utakaa miezi mingine 2 hivyo jumla itakuwa 9..hapo hakuna haja tena
 
Miembe ya kisasa inahitaji sana dawa ili update embe nzuri. Nakushauri panda ya kienyeji. Nina miembe ya kienyeji ya Maembe dodo ni matamu na makubwa balaa. Situmii dawa yoyote na ninavuna Maembe kila mwaka pia yana soko kubwa ukienda sokoni
Unapolima ki bisahara usiogope kuhudumia.Hata hiyo ya kienyeji kama utapanda kwa scale ya biashara lazima kupiga dawa.
 
Kila la kheri mkuu!
Kama sikosei,Tabora ni moja ya maeneo yenye maembe mengi kulinganisha na maeneo mengine Tanzania.
Very true..ndio maana wakati nafanya analsis nipande zao gani nikaona ni miembe tu
 
..wakati unasubiri miembe izae na kurudisha mtaji utapanda zao gani la muda mfupi ili kukupa nafuu ya gharama za kutunza na kuhudumia miembe yako?
Bado sijafatilia..ila namewaruhusu ndugu zangu na majirani walime humo ili wasaidie palizi
 
Unapoteza muda ndugu, ungetuuliza tuliozaliwa na kukulia Tabora kabla ya kuingia gharama zote hizi ikitarajia mapato hewa hewa (ya kwenye makaratasi).

Msimu wa maembe huko Tabora huwa yanagawiwa bure, yaani inafika muda Kenta zima linuzwa elfu 30. Ili unielewe vizuri uliza watu wa Iringa, msimu wa nyanya baei inakuwaje. Na kwanini kilimo cha nyanya hakiwatoi.

Pia waulize watu wa huko Mbeya na Njombe kwanini kilimo cha parachichi hakiwatoi?

Wakati wewe ukihangaika kupanda miembe, Kuna maeneo huko Tabora wamezaliwa na kukuta msitu wa miembe.
Mimi pia nimezaliwa na kukulia Tabora ingawa kwa sasa nipo Dar.Tabora ya miaka hiyo sio ya leo,usafiri wa uhakika na SGR inakuja kwa kasi.Bei unayosema ilikuwa miaka hiyo tunatumia siku 2 kwa treni kufika Dar.Soko la nje lipo wazi kabisa ni kufunguka akili tu.Jambo Juice na kina Azam wapo huko wanayatafuta tena mabichi.
 
Miembe ya kisasa inahitaji sana dawa ili update embe nzuri. Nakushauri panda ya kienyeji. Nina miembe ya kienyeji ya Maembe dodo ni matamu na makubwa balaa. Situmii dawa yoyote na ninavuna Maembe kila mwaka pia yana soko kubwa ukienda sokoni

Nimepanda heka sita, ni mwaka wa nane sasa miembe mikubwa sana lakini haizai!!

Mwaka huu imepigwa madawa na mbolea za kila aina naona angalau kuna embe sasa!! Sikutaka habari za madawa
 
Kwa Tabora uko upande gani ambako hakuna samadi mkuu? Hujafanya research ya kutosha. Pia aliyekushauri kutumia miche ya kienyeji naomba uzingatie huo ushauri. Unasema unataka kuwahi kurudisha capital. Sasa hapo inakuwa hivi haupandi kokwa bali unatumia vikonyo vilivyofanyiwa budding au grafting, maanake hapo mti unaanza kuzaa kama hiyo tunayoita ya kisasa.
Bahati mbaya nilichelewa kukusanya samadi kutoka kwa wafugaji ambao na wao kipindi hiki wanahitaji sana kwani mbolea ya viwandani imekuwa ghali sana kwao.Hiyo ya kienyeji iliyofanyiwa grafting nitapanda pia (bolibo na dodo).
 
Tafuta mashine ya kukamua juice baadae badala ya kuwa supplier wa Bakhressa
Au utakaa nayo mbele ya nyumba kama wanaouza matikiti?
Ubunifu muhimu ila mawazo sio mabaya
Swali kwanini ujikite kwenye maembe tu kama ardhi unayo?
Panda matunda aina hata 5
Sawa..pia tapanda minazi,chikichi na michungwa
 
Mimi pia nimezaliwa na kukulia Tabora ingawa kwa sasa nipo Dar.Tabora ya miaka hiyo sio ya leo,usafiri wa uhakika na SGR inakuja kwa kasi.Bei unayosema ilikuwa miaka hiyo tunatumia siku 2 kwa treni kufika Dar.Soko la nje lipo wazi kabisa ni kufunguka akili tu.Jambo Juice na kina Azam wapo huko wanayatafuta tena mabichi.
Viwanda vya juice huwa wanataka embe aina gani?
 
Hayo maembe laki 2 utamuuzia nani? Na unajipangia bei kabisa
 
Hayo maembe laki 2 utamuuzia nani? Na unajipangia bei kabisa
Kama nikiyapata hayo nitahangaika hata soko la nje...TanTrade wanakuongoza hadi unalifikia soko lake huko duniani.Cha msingi zingatia ubora tu
 
Back
Top Bottom