Kilimo cha maembe ya kisasa

Kilimo cha maembe ya kisasa

Miembe ya kisasa inahitaji sana dawa ili update embe nzuri. Nakushauri panda ya kienyeji. Nina miembe ya kienyeji ya Maembe dodo ni matamu na makubwa balaa. Situmii dawa yoyote na ninavuna Maembe kila mwaka pia yana soko kubwa ukienda sokoni
Mkuu hayo ya kienyeji nayo siku hizi yanaharibiwa sana na wadudu
 
Kila la kheri mkuu!
Kama sikosei,Tabora ni moja ya maeneo yenye maembe mengi kulinganisha na maeneo mengine Tanzania.
 
Hii ya kienyeji inachukua muda gani hadi kuanza kuzaa tofauti na ya kisasa inayozaa baada ya miaka 3
Mti wowote wa matunda wa kienyeji bila kubadi ni miaka 5 mpaka 7. Mti wa kienyeji ukiubadi utazaa muda ule ule kama miti ya kisasa ( miaka 3). Kumbuka unapobadi mti unachukua tawi la mti ulioanza kuzaa miaka hata mitatu mfululizo. Hii miti ya kienyeji unatoa tawi kwenye miti ya asili.
 
Katika hekaheka za kujiandaa kustaafu miaka 7 baadae nimeamua nipande miche kama 500 yaani ekari 10 za maembe kisasa.

Shamba lipo Tabora kwa sasa naendelea kuchimba mashimo. Nitapanda bila mbolea ya samadi ila taweka NPK baada ya miezi 3 ikiwa imeshika.

Mpango wangu miche 450 ipone ili nipate wastani wa embe 500 kila mti mwaka wa 6 na hii itanipa embe 225,000 na kama tauza kwa Tzs 400 nipate 90m.Hapo nitaamua kustaafu kazi nikiwa na miaka 55.
Bila picha huu Uzi ni batili..
 
Mti wowote wa matunda wa kienyeji bila kubadi ni miaka 5 mpaka 7. Mti wa kienyeji ukiubadi utazaa muda ule ule kama miti ya kisasa ( miaka 3). Kumbuka unapobadi mti unachukua tawi la mti ulioanza kuzaa miaka hata mitatu mfululizo. Hii miti ya kienyeji unatoa tawi kwenye miti ya asili.
Shukurani mkuu
 
Hivi hakuna njia ya kitaalam yakufanya maembe yaive katka msimu tofaut na huu wa kawaida ili mtu apge pesa kivyake vyake

..kuna miembe inaitwa kent nimesoma wataalamu wanadai inazaa kwa kuchelewa kulinganisha na miembe mengine. kwa hiyo shamba likiwa na mchanganyiko wa miembe inayopishana kuzaa mkulima anakuwa anavuna ndani ya msimu, na nje ya msimu.
 
Katika hekaheka za kujiandaa kustaafu miaka 7 baadae nimeamua nipande miche kama 500 yaani ekari 10 za maembe kisasa.

Shamba lipo Tabora kwa sasa naendelea kuchimba mashimo. Nitapanda bila mbolea ya samadi ila taweka NPK baada ya miezi 3 ikiwa imeshika.

Mpango wangu miche 450 ipone ili nipate wastani wa embe 500 kila mti mwaka wa 6 na hii itanipa embe 225,000 na kama tauza kwa Tzs 400 nipate 90m.Hapo nitaamua kustaafu kazi nikiwa na miaka 55.

..wakati unasubiri miembe izae na kurudisha mtaji utapanda zao gani la muda mfupi ili kukupa nafuu ya gharama za kutunza na kuhudumia miembe yako?
 
Mpango wangu miche 450 ipone ili nipate wastani wa embe 500 kila mti mwaka wa 6 na hii itanipa embe 225,000 na kama tauza kwa Tzs 400 nipate 90m.Hapo nitaamua kustaafu kazi nikiwa na miaka 55.
Unapoteza muda ndugu, ungetuuliza tuliozaliwa na kukulia Tabora kabla ya kuingia gharama zote hizi ikitarajia mapato hewa hewa (ya kwenye makaratasi).

Msimu wa maembe huko Tabora huwa yanagawiwa bure, yaani inafika muda Kenta zima linuzwa elfu 30. Ili unielewe vizuri uliza watu wa Iringa, msimu wa nyanya baei inakuwaje. Na kwanini kilimo cha nyanya hakiwatoi.

Pia waulize watu wa huko Mbeya na Njombe kwanini kilimo cha parachichi hakiwatoi?

Wakati wewe ukihangaika kupanda miembe, Kuna maeneo huko Tabora wamezaliwa na kukuta msitu wa miembe.
 
Katika hekaheka za kujiandaa kustaafu miaka 7 baadae nimeamua nipande miche kama 500 yaani ekari 10 za maembe kisasa.

Shamba lipo Tabora kwa sasa naendelea kuchimba mashimo. Nitapanda bila mbolea ya samadi ila taweka NPK baada ya miezi 3 ikiwa imeshika.

Mpango wangu miche 450 ipone ili nipate wastani wa embe 500 kila mti mwaka wa 6 na hii itanipa embe 225,000 na kama tauza kwa Tzs 400 nipate 90m.Hapo nitaamua kustaafu kazi nikiwa na miaka 55.
Kama sio mtu wa kibla, tupia wanyama wawili, utakuja kunishukuru. Miaka 7 utakuwa unamtukana muajiri wako
 
..kuna miembe inaitwa kent nimesoma wataalamu wanadai inazaa kwa kuchelewa kulinganisha na miembe mengine. kwa hiyo shamba likiwa na mchanganyiko wa miembe inayopishana kuzaa mkulima anakuwa anavuna ndani ya msimu, na nje ya msimu.
Kent inapatikana wapi na ina sifa zipi ?
 
Nimejitahidi kuipata imekuwa ngumu,Taweka NPK kwanza baadae tajitahidi niwke samadi
Kwa Tabora uko upande gani ambako hakuna samadi mkuu? Hujafanya research ya kutosha. Pia aliyekushauri kutumia miche ya kienyeji naomba uzingatie huo ushauri. Unasema unataka kuwahi kurudisha capital. Sasa hapo inakuwa hivi haupandi kokwa bali unatumia vikonyo vilivyofanyiwa budding au grafting, maanake hapo mti unaanza kuzaa kama hiyo tunayoita ya kisasa.
 
Kilimo bana huwa nakiheshimu na huwa nakiogopa sana kuna kipindi ilikuja trend ya kilimo cha vitunguu bas bana

Tuna shamba la mzee hekar 12 mm nikachukua etari 4 nikalima vitunguu kwa mahesabu yangu skutaka magunia mengi nilisema tu nikipata gunia 30/40 za vitunguu zinatosha na kia gunia nikiuza shiling laki 1 bas nimetobao
Nikachukua vijana nikawaweka camp kila wiki naende watembelea napeleka chakula na pembejeo mwisho wa sku kilichokuja nitokea mh mmmmmh
Kwa ushauri wangu ni bora ufugaji kulko kilimo
Shida ya kilimo ni bei hushuka na kupanda mda wwte na mara nying bei ushuka
Ufugaji sku zote bei hupanda ni
Mara chache sana kukuta bei ya mbuzi ng’ombe au kondoo imeshuka
 
Back
Top Bottom