Mkuu umenena vyema, kununua miche mara nyingi utapata hadi asilimia 30 madume ambayo Kwa hakika ni hasara kwani unatumia muda wa hadi miezi mitatu kubaini kama ni dume ilihali umepoteza raslimali nyingi.
Acha story za kufunga magunzi ya mahindi au kukata eti itabadilika, haina ukweli.
Mkuu sina hakika kama kuna njia ya kutambua kama ni dume au la. Nakumbuka kituko kimoja Nilipiga picha ya madume Na kumpelekea bwana shamba mmoja ambaye baada ya kuziona alinipa hongera Kwa kupata miti yeye kutoa mapapai( matunda) marefu! Niliondoka bila kujibu.Mkuu,
Miye nimekwisha fanya kosa hili. Nilinunua miche toka kwa wauzaji wa barabarani. Nina miche kama 14 hivi nyumbani na nimeipanda kama 'shamba darasa' kwa ajili ya mradi mkubwa nitakaoufanya baadaye.
Kwa sasa miche inakaribia miezi 2 ila bado sijajua ipi ni jike (itakayoniletea matunda) na ipi ni dume (hasara). Kuna namna rahisi ya kuitambua ikiwa na umri kama huo wa miezi miwili?
Asante.
Njia ya kienyeji huenda ikakusaidia. Chukua Mabunzi (magunzi) ya mahindi, yafunge moja kila mche mmoja wa Mpapai (Kama vile MAMA anavobeba mtoto mgongoni). By default, miche dume yote itageuke jike. Na miche jike itaendelea kubaki jike.Mkuu,
Miye nimekwisha fanya kosa hili. Nilinunua miche toka kwa wauzaji wa barabarani. Nina miche kama 14 hivi nyumbani na nimeipanda kama 'shamba darasa' kwa ajili ya mradi mkubwa nitakaoufanya baadaye.
Kwa sasa miche inakaribia miezi 2 ila bado sijajua ipi ni jike (itakayoniletea matunda) na ipi ni dume (hasara). Kuna namna rahisi ya kuitambua ikiwa na umri kama huo wa miezi miwili?
Asante.
Mbegu za zamani hazita kufaa kwa sababu hazini mazao mengi. Kuna mbegu za kisasa ambazo zinakua haraka na kuzaa mapema. Mbegu hizi huzaa sana na huleta faida kubwa. Hupatikana katika maduka ya pembejeo za kilimo, Wazalishaji wa mbegu bora na Vituo vya utafiti.Wana JF, nataka kufanya kilimo cha mapapai ila nahitaji mbegu za muda mfupi kuzaa ili nianze kuvuna mapema. Naomba msaada wa yafuatayo
1 Wapi nitapata mbegu fupi za muda mfupi kuanza kuzaa?
2. Nikitaka kupanda spacing iwe kiasi gani toka mche hadi mche?
Asanteni sana hii ni katika kuhangaika kuongeza kipato maana hii nchi ukizubaa ukajikuta unanyong'onyea sana kwa wanayojili.
Kweli mkuu watu wamekaa kimya ambacho upande mmoja unaweza kufikiri kuwa zoezi limekuwa gumu Kwa wengi wetu.Nimeona kila mtu anajaribu ila hakuna alieleta mrejesho amefanikiwa ama ku fail
ThanxKwenye bei hapo nakushauri nenda kawaulizie wale wanaouza kwa jumla sokoni ili upate bei ya uhalisia.
Ukipata information zimwage hapa mkuu hata mm napanga kuingia huko
Ingia shambani ukalime utuletee feedback