hili tunda lilinitoa jasho,
nilipata changamoto nyingi sana wakati naanza kulima,nilikuwa nalima maeneo ya Mwasonga Kigamboni,nilitumia mbegu ya Sukarii F1.ila inabidi ukubaliane na changamoto zitakazo kukabiri,
kwanza kuna panya wanao kula mbengu uliyo panda ile siku ya kwanza, kwa hiyo inabidi ulinde ndani ya siku 3 hadi mbegu ichepue,
kuna ngedere hawa wanakuja baaada ya tunda kuota,kuna fuko hawa wanakuja baada ya tunda kuiva.kuna mvua,kuna magonjwa harafu kuna kuoza kwa matikiti.yani changamoto zipo nyingi,mie nilikata tamaana maana ilikuwa kila siku ni pressure tu. nataka nijaribu kilimo kingine ila siyo tikiti ambalo linataka uache kazi ufanye kazi.