Kilimo cha matikiti maji (watermelon): Ushauri na Masoko

Wadau naomba nijuzwe sukari F1 ipi ni bora kati ya ile ya Africasia na East African Seeds
 
ubora sijaweza kutofautisha ila mwaka jana nitumia east African seeds il a mwaka nataka nijaribu kutoka balton Tanzania
 
Kuna yeyote anayelima kibaha mana nmepata shamba huko msaada plz
 
SAALAMU
HAYA MATIKITI YANAOITWA YA KISASA (F1) HYBRID, HAYA YANAKUWA YAMETENGEZWA YAKIWA NA SIFA ZA ZIADA KULIKO HAYA YA KAWAIDA (lOCAL/OPV). HAYA YA KISASA YAPO AMBAYO YAMEKINGWA KUWEZA KUTOSHAMBULIWA NA MAGONJWA MBAIMBALI KAMA VILE MAGONJWA YA UMBWILI PODA (POWDERY MILDEW), AU KUJIKUNJA KWA MAJANI (LEAF CURLING ). LAKINI PIA YA KISASA YAMETENGENZWA KUWAHI KUKOMAA, MENGI SANA KAMA SUKARI F1 AU JULINA F1 et al... YANAANZA KUKOMAA BADADA YA SIKU 70-75. FAIDA NYINGINE YA KUPANDA HAYA YA KISASA NI KUWA KATIKA SHIMO UNAWEKA MBEGU 1 MAXIMUM SANA NI MBILI, NA ASILIMIA ZA UOTAJI WAKE NI MKUBWA SANA
95%+
KWA MFANO HAYA YA KISASA UNAHITAJI KWA EKA 1 UNAHITAJI MBEGU GRAM 200-250 COZ UNAPANDA MOJA MOJA, LAKINI HAYA YA KIENYEJI (LOCAL/OPV) UNAPANDA MBEGU HADI 3 KWA SHIMO MOJA, HIVYO KWA EKA 1 UNAHITAJI HADI MBEGU GRAM 500-700 NA SI ZOTE ZITAOTA. PIA HAYA YA KISASA NDANI YANASUKARI SANA, NA YANAVUTIA KIUMBO RANGI NA HATA UZITO MENGI UNAKUTA YANAKILO 5 HADI 12. FAIDA NYINGINE YA MUHIMU ZAIDI NI KUWA HIZI ZA KISASA ZINAKUPA MAVUNO MENGI KWA KAMBA MOJA, HIVYO UKILIMA VIZURI NA UKAWEZA KUPAMBANA NA HIZO CHANGAMOTO ZA LISHE, NA WADUDU, NA MADALALI BASI UHAKIKA WA KURUDISHA GHARAMA ZAKO NI MKUBWA SANA.


Hivi haya ya kisasa yana nini zaidi? Maana naona kama wakulima wanaachana na matikiti ya asili
 
SALAAMU
UNAPOZUNGUMZIA UBORA, KUNA MAMBO MENGI HAPO MKUU, JE UNAAMISHA UBORA KWA MAANA YA UTAMU (SUKARI/MAJI), JE UNAANGILIA UBORA KATIKA KUTOSHAMBULIWA NA WADUDU, JE UNAANGALIA UBORA KATIKA KUTOSHAMBULIWA NA MAGONJWA ETC, AU JE UNAANGALIA UBORA KATIKA SHAPE/UMBO KUVUTIA ETC. HAYO MAMBO MARA NYINGI YANAKUWA YAMEANDIKWA KATIKA VILE VIKARATASI/VIFUNGASHO HADI GERMINATION PERCENT WAWEZA IONA, AU ZAIDI KABLA YA KUNUNUA UNAWEZA ULIZA HII MBEGU INAUTOFAUTI GANI NA HII..UTAAMBIWA TU. SUKARI F1 YA EAST WEST INASIFIKA KWA KUWA INAUWEZO WA KUKOMAA HARAKA, INASUKARI SANA, NA INAKUWA KUBWA MNO MAXIMUM NI KILO 12, LAKINI PIA KUNA TAARIFA ZINAONYESHA ZIKO IMPROVED DHIDI YA MAGONJWA MENGI YA FANGASI (KUTU YA MAJANI, NA UBWIRI UNGA/PODA).

KABLA YA KUNUNUA ULIZA KWANZA UPATE ELIMU TOKA KWA MUUZAJI, KAMA NI MWAMINIFU ATAKWAMBIA UTOFAUTI WA MBEGU ALIZONAZO.

Wadau naomba nijuzwe sukari F1 ipi ni bora kati ya ile ya Africasia na East African Seeds
 
Umeeleza vyema sana mkuu. Ubarikiwe.
 

Post yako ina makosa katika vipimo. Acre moja ina surface area of 4046.86 meter squire. Kama unabisha fanya utafiti zaidi, unaweza hata ku google. eg acre to squire meters.
 
Naomba kuuliza, ni mbegu ipi nzuri zinazotoa tikitiki zenye ubora? Msaada
 
Nammimi naomba namba nkuu
 
Hii mada ingenoga kwa kuweka na picha ili iwe rahisi kutambua na kutofautisha hizo aina
 
Habar wana JF!

Nahtaji kuanza kufanya kilimo cha matikiti maji kule Mikese Morogoro mwezi huu wa sita!

Kipi cha kufanya ndugu zangu ili swala hili liende vzuri!
 
Kanunue mbegu inaitwa Juliana F1 inazalishwa na kibo seeds... Ukikosa Hiyo kanunue mbegu inaitwa sugar baby king inazalishwa na African seeds
 
Kanunue mbegu inaitwa Juliana F1 inazalishwa na kibo seeds... Ukikosa Hiyo kanunue mbegu inaitwa sugar baby king inazalishwa na African seeds
alf kibo wana bei nzuri kuliko African seeds
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…