MJ Dannie
Member
- Oct 28, 2015
- 61
- 31
Habari yako mkuu, naomba unijuze changamoto ulizokutana nazo mpaka ukapata hasara, nataka na nianze kulima huu mwezi. Thanks in advancenimeshauza mkuu ila nilipata hasara.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Habari yako mkuu, naomba unijuze changamoto ulizokutana nazo mpaka ukapata hasara, nataka na nianze kulima huu mwezi. Thanks in advancenimeshauza mkuu ila nilipata hasara.
Hivi haya ya kisasa yana nini zaidi? Maana naona kama wakulima wanaachana na matikiti ya asili
Wadau naomba nijuzwe sukari F1 ipi ni bora kati ya ile ya Africasia na East African Seeds
Umeeleza vyema sana mkuu. Ubarikiwe.Kwanza hongera kwa kuamua kuingia shambani, mimi nalima matikiti na nimeshajilipua kulima ktk kipindi hiki cha masika, kubwa zaidi tafuta mbegu bora kwenye maduka ya kilimo mfano pitia kariakoo, mimi nalima Hybrid F1 sugar queen, na kiwango cha ekari moja utatakiwa kuwa na gram 300 na kila shimo panda mbegu 2 japo wapo wanaopanda mpaka 3, na hapa utatakiwa kuwa na mshimo kama 2000.
Andaa shamba vizuri japo wiki tatu kabla ya kupanda na hakikisha eneo lako lina maji ya kutosha kwani tikiti linahitaji maji mengi katika uhai wake, Panda kwa mbolea, ni vema zaidi kama utapata samadi na kama utatumia ya viwandani zipo kama vile winner(hapa kuna kiambato chake, utamuuliza muuzaji), kwa kukuzia utatumia CAN, andaa dawa za wadudu wanaokata majani pindi matikiti yanapoanza kuota tu na pindi unapoona dalili za matikiti kushambuliwa majani (karate itakufaa).
Unahitaji uangalizi wa karibu sana kuanzia mwanzo mpaka mwisho na hakikisha unakuwa na dawa za kutosha kwa ajili ya kuzuia wadudu waharibifu, ukungu hasa kipindi hiki na magonjwa yanayoshambulia majani, maua na matunda.
Gharama kubwa utakayoingia kwenye kilimo hiki ni kwenye mbegu( ekari moja ni gram 300= 250,000 kwa Dar), dawa( hapa inategemea na hali ya eneo na jinsi magonjwa na wadudu wanavyoshambulia), nguvu zako mwenyewe kwenye kumwagilia( hapa kama unatumia ndoo, ila kama unatumia mashine ya kuvutia maji basi utahitaji wastani wa lita 5 kwa ekari moja kila unapomwagilia) na kutunza shamba, kama unatumia kijana basi hapo ni makubaliano yenu, bomba la kupigia dawa ni muhimu sana.
Mavuno ni kuanzia siku 65 mpaka 75 inategemea na eneo lenyewe na aina ya mbegu, na kiasi cha mavuno kwa ekari moja ni kiasi cha matikiti kama 7000( kila mche mmoja utoe matikiti 2 tu yenye afya nzuri) na soko likiwa nuri basi utauza kwa wastani wa Tsh 1500 au zaidi shambani, na ukiMU kwenda mwenyewe sokoni mfano Buguruni unaweza kuuza bei nzuri kama ni kipindi mmea huo haupatikani.
Ushauri: usiende shambani na matarajio makubwa zaidi ya kupata hela nyingi ukasahau changamoto zake( mavuno kidogo, hasara na muda), shambani kunahitaji uangalizi wa karibu sana na usijaribu kulima kwa simu hasa kama una watu wasio waaminifu watakuua kwa ugonjwa wa moyo. Pia hizo faida zinazopatiakana ni pale tu utakapo fata ushauri wa kitaalamu na ukaamua kwa dhati kufanya kilimo. Nimejaribu kueleza kile ninachofahamu japo sio kwa utaalamu zaid, mengine wajuzi watakuja kujazia.
Karibu sana shambani
KAKA HII HABARI UMETOA HAIKO SAHIHI husasan unaposema unapanda kwa umbali wa 2 by 3 metres halafu unapata mashimo 1000. hicho kitu hakipo since one acre ina 70 by 70 metres na surface area ya 4900 meter squared. kama unapanda kwa 2 by 3m, utakua na mashimo 575 tu katika acre moja. this means kama unapataga matunda matano kwenye shimo moja basi utapata 575*5*5= 14375 manke utakua na mashimo 575. iyo inamaanisha utapata matunda 14375 kwa acre tano, kulingana na bei yako ya kuuzia shamba sh mia tano ambayo utakua ulipunjwa sana, manake tikiti moja bei shamba ni buku dsm, hata mikoani. revenue yako itakua 14375*500= 7187500 tsh only, or lets say 7200000. kitu kingine u realy have to explain inakuaje unatumia million 25 kulima na kumwagilia kwa mwaka mmoja. wakati sisi tunatumia just 2. mil kulima acre tano izo izo kwa msimu, kwa mwaka roughly 10 million. hebu tuelezee kuhusu garama zako, manake naanza kuhisi untaka kukatisha watu tamaa ya kulima hayo matunda
WANAOJUA, 1 by 1m space kutoka kwenye mmea mmoja mpaka mwingine. that means kunakua na mashimo 4900 kwa acre. kama target ni kupata matunda matatu makubwa kila shimo then tunfanya simple calculations 4900*3= 14700 fruits per one acre. fanya iyo times the market price ya shamba ambayo ni buku revenues inakua 14700000 ( forteen million tsh). iyo forteen milion toa garama ya 250,000 tsh ya kuhudumia iyo acre moja kuanzia unapopanda, palizi, DAWA, ulinzi, mbegu, trekta, harrow, kila kitu mpaka kuvuna.
Nammimi naomba namba nkuuNdiyo zipo zinakua na uwezo Wa kuhimili mikikimikiki ya masika.hizi nyingine zinaoza.mi mwenyewe ninampango Wa kulima tikiti la masika kwsbb linalipa.kuna jamaa ni mzoefu zaidi Wa mambo haya ndiye aliyeniwekea oda kiwandani.km utapenda nitakutumia no.yake
alf kibo wana bei nzuri kuliko African seedsKanunue mbegu inaitwa Juliana F1 inazalishwa na kibo seeds... Ukikosa Hiyo kanunue mbegu inaitwa sugar baby king inazalishwa na African seeds