Kilimo cha matikiti maji (watermelon): Ushauri na Masoko

Ninayo business plan ya kilimo cha water melon!.. Ila iko planed zaidi kwa infrastructure za Dodoma cjui kama itakufaa!..

Mkuu mimi nyumbani ni hombolo dodoma je naweza kuwasiliana na wewe kwaajili ya kupata ushauri namna ya kulima kilimo cha matikiti kwa mazingira yetu huko??
 
natangulisha shkurani zangu kwnu.
cku hadi cku zimekua zikipita nikiwaza nn chakufanya ili kufikia malengo.

Mimeamua kufanya mamuzi ya kilimo cha matikiti maji lkn kabla ya kufikia kulima nahitaji kujua vitu vingi, me niko arusha cna shamba km nitapata shaba la kukodi co mbaya.

1)mkoa gn yanakubali vizuri?
2)mbegu bora
3)na mtaji wake kwa shamba la ekari 3 ? pamoja na mabawa ya kuliwa wadudu?

msada wenu jf
 
Hapa JF kuna maelezo ya kutosha kuhusu hili zao

Fungua hiyo link hapo chini soma kilichomo ndani kama hutaelewa basi uliza utajibiwa

kila la kheri

Kilimo cha matikiti maji (watermelon): Ushauri na Masoko
 
Nikimwagilia matikiti kutumia sprinkle inawezekana kupata matunda makubwa na bora?
 
Nikimwagilia matikiti kutumia sprinkle inawezekana kupata matunda makubwa na bora?
Mkuu ingawa sijawahi kulima tikiti lakini najua tikiti lina shina moja tu hata kama limesambaa kiasi gani, kwa hiyo umagiliaji wa namna hii sijui kama utakuwa na tija. nivizuri kumwagilia shina tu.
 
Very educative, asanteni wadau nami naenda kulima sasa!
 
Mkuu nimepata shamba ifakara huko heka 10 ziko karibu na chanzo cha maji, je ntaitaji mbegu mchanganyiko au moja tu na nikiasi gani itanitosha. na soko zuri nasikia ni mmaeneo ya shinyanga na mwanza je hizi taarifa za masoko ni kweli
 
Bei ya sasa kwa matikiti ni 1500 hadi 1000,..soko linazid kua baya kutokana na wingi was matikiti
 
Kuna waliofanikiwa kutokana na huu uzi.? Ushuhuda please.
 
MKUU NAOMBA UNISAIDIE MAELEZO KIDOGO KUHUSU KUPUNGUZA SHINA. KUNA UTAALAMU WOWOTE AMBAO UTASAIDIE KUTOATHIRI UKUAJI WA MMEA AU UNAKATA TU KISHA MMEA UNAENDELEA BILA SHIDA.
 
Bei ya sasa kwa matikiti ni 1500 hadi 1000,..soko linazid kua baya kutokana na wingi was matikiti
Nimepita maeneo ya Ushirombo - Bukombe na Katoro - Geita DC matikiti yanauzwa mpaka Tsh 5,000/ kwa moja kubwa bei ya rejareja.
 
Mwaka huu tupo kwenye sera ya viwanda sasa iv inabid tutengeneze kiwanda cha matikiti
 
Wapendwa hbr zenu! Naomba kuuliza, je Maji ya chumvi hayana madhara kwa matikiti Maji?
 
Hata Mimi nataka kupata elimu Juu ya kupunguza mashina katika mche mmoja.kwani unakuta mche mmoja unatoa mashina 4 au 5 hakafu matunda mpaka 8 je hakuna athari ktk ukuaji?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…