Kilimo cha matikiti maji (watermelon): Ushauri na Masoko

Kilimo cha matikiti maji (watermelon): Ushauri na Masoko

Jamani habarini za wikiendi, naomba kujua mche wa tikiti maji unaweza kuvunwa mara ngapi matunda yake?

Kwa mfano embe zinavunwa kila mwaka, ndizi unavuna mara moja tu na mche unakwisha kazi yake. Vipi kwa matikiti maji, unavunwa mara ngapi na kwa kipindi/interval gani?

Nataka kulima, yanalipa sana nisaidieni tafadhali.[/QUOT
Shamba langu limefikia hatua ya maua ili kuweka matunda,
Tafadhali naomba msaada kwa mambo yafuatayo kwa yeyote mwenye ujuzi
1. mbolea aina gani na ni kiasi gani?
2. madawa aina gani kiasi gani na yanawekwa mara ngapi
3. kuna suala la upogoleaji kukatia matawi na topping, jee inafanyikje
4. suala la uchavushaji nitajuaje kama hali ni nzuri maana nimesikia kuna hand polination
5 idadi ya matunda yanayopaswa kuachwa kwenye mche ni mangapi

TAFADHALI MWENYE UJUZI NAOMBA MSAADA
 
C.K said:
Jamani habarini za wikiendi, naomba kujua mche wa tikiti maji unaweza kuvunwa mara ngapi matunda yake?

Kwa mfano embe zinavunwa kila mwaka, ndizi unavuna mara moja tu na mche unakwisha kazi yake. Vipi kwa matikiti maji, unavunwa mara ngapi na kwa kipindi/interval gani?-TIKITI UNAVUNA MARA MOJA PIA

Nataka kulima, yanalipa sana nisaidieni tafadhali.[/QUOT
Shamba langu limefikia hatua ya maua ili kuweka matunda,UNAHITAJI BOOSTER STARTER (POLYFEED STARTER, SUPER GROW)
Tafadhali naomba msaada kwa mambo yafuatayo kwa yeyote mwenye ujuzi
1. mbolea aina gani na ni kiasi gani?-MBOLEA YA KUPANDIA NI DAP, AU NPK AU YARA MILLER WINNER, MIFUKO 2 INATOSHA KWA KUPANDIA. UTAHITAJI CAN- MIFUKO 2 (100 KGS) YA KUKUZIA
2. madawa aina gani kiasi gani na yanawekwa mara ngapi
-MADAWA UNAHITAJI YA WADUDU LITA 2, YA UKUNGU KILO 2, NA YA KUZUIA MBEGU KUOZA (HIZI UNATUMIA KABLA YA KUPANDA MBEGU UTAHITAJI GRAM 10 KW AMBEGU SIZIZO ZIDI GRAM 500), DAWA UNATUMIA KILA BAADA YA SIKU 14. UTAHITAJI PIA BOOSTER, 1 KG YA STARTER BOOSTER NA 1 KG YA FINISHER BOOSTER
3. kuna suala la upogoleaji kukatia matawi na topping, jee inafanyikje-KWAA TIKITI, TUNA NIMP KLE MBELE/KUKATA KULE MBELE ILI KILA KAMBA /MCHE UBAKI NA ANGALAU MATUNDA 3 YASIZIDI MANNE KWA KAMBA MOJA
4. suala la uchavushaji nitajuaje kama hali ni nzuri maana nimesikia kuna hand polination
-HAND POLLINATION INAFANYIKA KATIKA GREEN HOUSE, SI KATIKA OPEN FIELD
5 idadi ya matunda yanayopaswa kuachwa kwenye mche ni mangapi-3-4

TAFADHALI MWENYE UJUZI NAOMBA MSAADA
 
Naombeni msaada kwa watalaam wa kilimo! Nataka kuotesha miche ya tikiti maji 10,000/= mkoani Shinyanga je,
1. Itanigharimu kiasi gani kuitunza hadi ikue na kufikia mauzo??
2. Shamba ninalo ekari 3 je litatosha??
3. Mbegu zake zinapatikana wapi zaidi??
4. Soko la tikiti maji sasa zuri liko mkoa gani?
5. Angalau kwa kiwango cha chini tikiti moja naweza kuiuza kwa shliingi ngapi??
Asanteni wapendwa!
kwa kuwa wewe bado mgeni katika biashara hii ninakushauri anza kwa ekari kidogo kidogo kaka. anza ata na ekari moja tu kwa sasa
 
habari..mimi nilishapanda tikiti lakini nilipata hasara shamba zima ila sasa nataka nianze tena upya..mnanishauri vipi?
 
Samahani mkuu unaweza kunisaidia kupata shamba la kukodi au mahali wanapokodisha mashamba kwaajili YA KILIMO cha tikiti
 
Mkuu sinampango wa kumtag yyte kwanza hiyo kutag mm sijui maana yake nn waulize moderator mm nimeomba msaada tu wa mawazo
Wewe si wa Dar bila shaka,umenichekesha mkuu kusema hujui kumtag [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Mwezi wa 6
Kuna mawili: pengine unayapa maji mengi sana kupita uwiano wa ukuaji/ujengaji wa gamba la juu na kiwango halisi cha maji yanayotakiwa kwenye tunda kwa muda huo.

Ama, angalia sana kwenye huo ufa/mpasuko yawezekana lilidonolewa/tobolewa na wadudu waharibifu angali likiwa changa hivyo kadri tunda linavyozidi kutanuka tobo limesababisha tunda kupasuka.

Angalizo; zingatia sana dawa ya kuu wadudu, weka dawa ya panya shambani(ile ya tambi) pia epuka kumimina maji juu ya tunda kabisa especially wakati wa hili jua kali make mda huo ngozi ya tunda inakua ya moto na imexpand sana so kitendo cha kulilowanisha maana yake ni kwamba unaliforce lipoe ghafla so obviously lita undergo excessive contraction!

Mwisho kabisa nenda duka la pembejeo waombe dawa ya kuzuia matunda yasipasuke, watakupa dawa ambayo ipo ktk hali ya mafuta na ukiipiga kwenye tunda yale mafuta yatasaidia incase maji yakilimwagikia kwa bahati mbaya basi yanateleza.
 
pia CAN au yaraliva nitrabor inasaidia kuimarisha ganda la tunda
 
TANGU UANZE KUYAPANDA MPAKA SASA UMEWEKA MBOLEA GANI MKUU??

KUPASUKA KWA TUNDA-UKIACHA MECHANICAL DAMAGE (yaani kudondokewa na kitu), SABABU ZINGINEZA NI UPUNGUFU WA Calcium (Ca) au wingi wa maji

QUOTE="kalinje, post: 17061479, member: 293826"]Mengine mwezi wa saba tarehe[/QUOTE]
 
1) Mtaji unategemea na jinsi wewe mwenyewe unavyofanya kilimo chako, watu uliowaajiri n.k. Kwa mfano, kama unamwagilia inategemea unamwagilia na nini, pump ya mguu kama MoneyMaker au ya Petrol? Zote mwisho wa siku utapata faida tofauti. To be on the safe size, weka 1M hadi kuvuna. Ila inaweza ikazidi au ikapungua.

2) Matikiti yanachukua miezi miwili hadi kukomaa

3) Kama wewe ni mjasiriamali unapaswa kujua soko kabla ya kuamua kulima. So tafuta soko kwanza, then ndo uamue kulima.

4) Kipindi cha kipupwe ndio kizuri kwa matikiti maji. Matikiti maji hayapendi mvua nyingi. Yakipata maji mengi karibia na mavuno yanaweza kupasuka yakiwa shambani ukapata hasara.

5) Karibu Mkuranga tulime matiki. Ila maeneo mengi ya ukanda wa pwani ni mazuri kwa matikiti maji.

Hope that helps.
Nice comment ndgu wish nikufindi unipe ideas zaidi
 
Back
Top Bottom