Kilimo cha matikiti maji (watermelon): Ushauri na Masoko

Kilimo cha matikiti maji (watermelon): Ushauri na Masoko

Haya yalulimwa peramiho B kama unakwenda maposeni.


Yalivunwa vizuri tu mwezi huu na pale sokoni yanakwenda kwa bei ya 2500 kwa tikiti
IMG-20160322-WA0031.jpg
 
Mkuu kilimo kinautajili wa hali ya juu sema kama huja Fanya kilimo utaona makida makida tuu lkn kaa ukijua kwamba hakuna siku itapita hujala zao la mkulima so kwa hapa Tanzania watu zaidi ya million 45 lazima kila siku wale mazao ya mkulima so hakuna siku kilimo kitapiteza utajiri.

Kilimo kinalipa mkuu wala usibeze na kusema ukishawahi kuona mtu ametajirika kwa kilimo.
 
For a detailed Business plan yenye maelezo yote kuhusu kilimo hiki na gharama zake just PM Tuongee biashara.
 
mkuu

haupo sahihi kabisa .... rekebisha hesabu zako tena

1 acre = 4046 sqm (square meters)

one acre ni sawa na approximate 70x70 yards na siyo meters

asante kwa sahihisho lakini bahati mbaya wengi wetu hatujazoea hiki kipimo cha yards, tukiileta kwenye meters natakiwa nipate vipimo vipi?
 
mie nimelima tikitiki ekari moja mwaka huu nataka kuuza, ila mimi ningependa kuuzia shamba. Mwenye taarifa ya hali ya soko kwa Dar es salaam wiki hii. Shamba lipo Kigamboni.
Mkuu umeshauza matikiti yako
 
Kilimo Cha Tikiti.

Je unataka kujitunza kuhusu kilimo cha matikiti? wasiliana nasi kwenye Whatsapp namba 0683556677 Kwa ada ya shilingi elfu mbili tu uweze kuunganishwa kwenye group.

Kumbuka ada hii ni kwa ajili ya somo hili tu. Kila wiki kutakua na masomo tofauti tofauti kuhusiana na Kilimo. Mada ya wiki itapatikana kupitia Instagram KilimoJoint au Facebook. Unaruhusiwa kupendekeza Mada ya wiki. Somo litaanza Kesho tarehe 10-04-2016 saa nane mchana
 
Loohh hii kweli bongo daslam kuungwa wasapu ya tikitiki maji 2000 hii jamii forum umelipia sh ngapi au hio wasap ulionayo

Watanzania tunashindwa kujiongeza hapo hivi (samahani kwa mfano huu koz ni slightly relevant)

Unafikiri hawa jamaa wenye hii wasap wangesema inalipiwa je ni wangapi wangekuwa nayo mpaka sasa ila kwakuwa wanacheza na akili zEtu waafrika ndio maana wanapata data zetu kirahici ila wanatumia indirect method kupata hela ila wewe na tikitiki hutaki kushea na wengine mpka ulipwe 2000
 
Najaribu kilimo cha vitunguu, nasubiri mvua zipungue. Pia naweka pilipili hoho na biliganya
Sawa sawa ni idea nzuri, ila take caution na pilipili hoho zoo delicate lakini zikitoka umekula bingo. Kitunguu pia ni idea nzuri, unalimia wapi Mkuu
 
Sawa sawa ni idea nzuri, ila take caution na pilipili hoho zoo delicate lakini zikitoka umekula bingo. Kitunguu pia ni idea nzuri, unalimia wapi Mkuu
vitunguu nafanya majaribio robo ekari Kigamboni. Kuna watu 2 wamelima na vimekubali walishavuna, ndio maana nataka kuingia huko. Pia kuna eneo dogo nitapanda migomba.

Nitakuwa nawapa mrejesho hapa kila changamoto na mafanikio nitakayo yapata.
 
vitunguu nafanya majaribio robo ekari Kigamboni. Kuna watu 2 wamelima na vimekubali walishavuna, ndio maana nataka kuingia huko. Pia kuna eneo dogo nitapanda migomba. Nitakuwa nawapa mrejesho hapa kila changamoto na mafanikio nitakayo yapata.
Poa chief, kitunguu tafuta mbegu ya red Bombay ndio iko juu sokoni.
 
wana JF kwanza poleni na shughuli za kimaisha za kila siku, bila kupoteza muda mimi ni kijana sasa nataka nijikite katika kilimo na kwa kuanzia nataka nilime MATIKITI MAJI kibada nimepata shamba la kukidi ekari 1.

Sasa naomba kama kuna mtu amabaye ameshawahi fanya hii kitu anipe mawazo ya kizoefu na hali iliendaje.

Je kuna faida? Au figisu nyingi? natanguliza SHUKRANI!
 
Kwanza hongera kwa kuamua kuingia shambani, mimi nalima matikiti na nimeshajilipua kulima ktk kipindi hiki cha masika, kubwa zaidi tafuta mbegu bora kwenye maduka ya kilimo mfano pitia kariakoo, mimi nalima Hybrid F1 sugar queen, na kiwango cha ekari moja utatakiwa kuwa na gram 300 na kila shimo panda mbegu 2 japo wapo wanaopanda mpaka 3, na hapa utatakiwa kuwa na mshimo kama 2000.

Andaa shamba vizuri japo wiki tatu kabla ya kupanda na hakikisha eneo lako lina maji ya kutosha kwani tikiti linahitaji maji mengi katika uhai wake, Panda kwa mbolea, ni vema zaidi kama utapata samadi na kama utatumia ya viwandani zipo kama vile winner(hapa kuna kiambato chake, utamuuliza muuzaji), kwa kukuzia utatumia CAN, andaa dawa za wadudu wanaokata majani pindi matikiti yanapoanza kuota tu na pindi unapoona dalili za matikiti kushambuliwa majani (karate itakufaa).

Unahitaji uangalizi wa karibu sana kuanzia mwanzo mpaka mwisho na hakikisha unakuwa na dawa za kutosha kwa ajili ya kuzuia wadudu waharibifu, ukungu hasa kipindi hiki na magonjwa yanayoshambulia majani, maua na matunda.

Gharama kubwa utakayoingia kwenye kilimo hiki ni kwenye mbegu( ekari moja ni gram 300= 250,000 kwa Dar), dawa( hapa inategemea na hali ya eneo na jinsi magonjwa na wadudu wanavyoshambulia), nguvu zako mwenyewe kwenye kumwagilia( hapa kama unatumia ndoo, ila kama unatumia mashine ya kuvutia maji basi utahitaji wastani wa lita 5 kwa ekari moja kila unapomwagilia) na kutunza shamba, kama unatumia kijana basi hapo ni makubaliano yenu, bomba la kupigia dawa ni muhimu sana.

Mavuno ni kuanzia siku 65 mpaka 75 inategemea na eneo lenyewe na aina ya mbegu, na kiasi cha mavuno kwa ekari moja ni kiasi cha matikiti kama 7000( kila mche mmoja utoe matikiti 2 tu yenye afya nzuri) na soko likiwa nuri basi utauza kwa wastani wa Tsh 1500 au zaidi shambani, na ukiMU kwenda mwenyewe sokoni mfano Buguruni unaweza kuuza bei nzuri kama ni kipindi mmea huo haupatikani.

Ushauri: usiende shambani na matarajio makubwa zaidi ya kupata hela nyingi ukasahau changamoto zake( mavuno kidogo, hasara na muda), shambani kunahitaji uangalizi wa karibu sana na usijaribu kulima kwa simu hasa kama una watu wasio waaminifu watakuua kwa ugonjwa wa moyo.

Pia hizo faida zinazopatiakana ni pale tu utakapo fata ushauri wa kitaalamu na ukaamua kwa dhati kufanya kilimo. Nimejaribu kueleza kile ninachofahamu japo sio kwa utaalamu zaidi, mengine wajuzi watakuja kujazia.
Karibu sana shambani
 
Naomba ufafanuzi hapo unaposema "unahitaji wastani wa lita 5 kwa ekari moja kila unapomwagilia"...
Namaanisha mafuta ya diesel au petrol( inategemea na aina ya mashine) kumwagilia ekari moja, hasa eneo kavu na linalomeza maji mengi, hizo lita 5 zitategemea na mashine yako, zipo nyingine hazili mafuta mengi sana kwahiyo hata lita 3 zinaweza kutosha kabisa, na unahitaji kumwagilia at least mara 2 kama eneo lako linaweza kutunza maji kidogo na mara 3 kwa maeneo yenye ukame sana, ila kwa kipindi cha mvua kama hiki unaweza kaa hata wiki 2 hujamwagilia
 
Back
Top Bottom