ushasikia mtu kafanikiwa kwa kukatisha watu tamaaa?Ushasikia mtu ametajirika kwa ukulima?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
ushasikia mtu kafanikiwa kwa kukatisha watu tamaaa?Ushasikia mtu ametajirika kwa ukulima?
msamehe bure yy ana waza utajiri watu wana waza Mafanikioushasikia mtu kafanikiwa kwa kukatisha watu tamaaa?
Tikiti ni zao la bustani(horticultural crop) hivyo uangalizi wa karibu ni muhimu linastawi maeneo mengi ya nchi laki i linastwi vizuri udongo wa kichanga. linakomaa baada ya 56Days. Kwa Shy Bukombe na Kahama kuna soko kubwa sana maana wanachukua tikiti kutoka Ruanda na burundi kwa maelezo ya kina na Business Plan kama utahitaji unakaribishwa kunipm
Braza naomba tuongee iboxKwanza hongera kwa kuamua kuingia shambani, mimi nalima matikiti na nimeshajilipua kulima ktk kipindi hiki cha masika, kubwa zaidi tafuta mbegu bora kwenye maduka ya kilimo mfano pitia kariakoo, mimi nalima Hybrid F1 sugar queen, na kiwango cha ekari moja utatakiwa kuwa na gram 300 na kila shimo panda mbegu 2 japo wapo wanaopanda mpaka 3, na hapa utatakiwa kuwa na mshimo kama 2000.
Andaa shamba vizuri japo wiki tatu kabla ya kupanda na hakikisha eneo lako lina maji ya kutosha kwani tikiti linahitaji maji mengi katika uhai wake, Panda kwa mbolea, ni vema zaidi kama utapata samadi na kama utatumia ya viwandani zipo kama vile winner(hapa kuna kiambato chake, utamuuliza muuzaji), kwa kukuzia utatumia CAN, andaa dawa za wadudu wanaokata majani pindi matikiti yanapoanza kuota tu na pindi unapoona dalili za matikiti kushambuliwa majani (karate itakufaa).
Unahitaji uangalizi wa karibu sana kuanzia mwanzo mpaka mwisho na hakikisha unakuwa na dawa za kutosha kwa ajili ya kuzuia wadudu waharibifu, ukungu hasa kipindi hiki na magonjwa yanayoshambulia majani, maua na matunda.
Gharama kubwa utakayoingia kwenye kilimo hiki ni kwenye mbegu( ekari moja ni gram 300= 250,000 kwa Dar), dawa( hapa inategemea na hali ya eneo na jinsi magonjwa na wadudu wanavyoshambulia), nguvu zako mwenyewe kwenye kumwagilia( hapa kama unatumia ndoo, ila kama unatumia mashine ya kuvutia maji basi utahitaji wastani wa lita 5 kwa ekari moja kila unapomwagilia) na kutunza shamba, kama unatumia kijana basi hapo ni makubaliano yenu, bomba la kupigia dawa ni muhimu sana.
Mavuno ni kuanzia siku 65 mpaka 75 inategemea na eneo lenyewe na aina ya mbegu, na kiasi cha mavuno kwa ekari moja ni kiasi cha matikiti kama 7000( kila mche mmoja utoe matikiti 2 tu yenye afya nzuri) na soko likiwa nuri basi utauza kwa wastani wa Tsh 1500 au zaidi shambani, na ukiMU kwenda mwenyewe sokoni mfano Buguruni unaweza kuuza bei nzuri kama ni kipindi mmea huo haupatikani.
Ushauri: usiende shambani na matarajio makubwa zaidi ya kupata hela nyingi ukasahau changamoto zake( mavuno kidogo, hasara na muda), shambani kunahitaji uangalizi wa karibu sana na usijaribu kulima kwa simu hasa kama una watu wasio waaminifu watakuua kwa ugonjwa wa moyo. Pia hizo faida zinazopatiakana ni pale tu utakapo fata ushauri wa kitaalamu na ukaamua kwa dhati kufanya kilimo. Nimejaribu kueleza kile ninachofahamu japo sio kwa utaalamu zaid, mengine wajuzi watakuja kujazia.
Karibu sana shambani
Mbona mail yako inatema, au umekosea mahali?
Heck inbox yako mkuuNina mchanganuo wa kilimo cha tikiti kwa anayehitaji pm me ur email.bureeee
nichek kwa ymagina5@yahoo.comNina mchanganuo wa kilimo cha tikiti kwa anayehitaji pm me ur email.bureeee
Tayari cheki emailnichek kwa ymagina5@yahoo.com
Tafadhali
Asante sana kiongozi.Tayari cheki email
Mkuu ile attachment haikufka naomba utume tena.Tayari cheki email
Nimetuma nyingine bila shaka imefika.Mkuu ile attachment haikufka naomba utume tena.
Asante
AsanteNimetuma nyingine bila shaka imefika.
email yangu ni xuma144@gmail.comAnayetaka mchanganuo na maelezo ya kilimo cha tikiti ni pm email nakutumia