Kilimo cha Mboga aina ya Asparagus, mboga ghali sana

Kilimo cha Mboga aina ya Asparagus, mboga ghali sana

CHASHA FARMING

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2011
Posts
7,872
Reaction score
9,263
Asparugus ni aina ya mboga iko kama vijitivijiti ila ni mboga ambayo ni very delicious na ni moja ya mboga very Expensive sana.

Kwa Tanzania mara nyingi huwa wana iagiza either South Africa au Dubai, Kwebye Super Ma let zetu huwa inapatikana kwa nadra sana mara mpjamoja na mara nyingi sana haipatikani au haipo.

Hii mboga kwa sisi wabongo ambao hatujatembea sio rahisi kabisa kuijua, Ila kwa walio tembea huko mbele watakuwa walisha kutana nayo.

Kwa Wazungu, Wahindi, wachina na kadhalika wanaijua vyema hii Mboga. Arusha kuna nyakati hiwa inapatikana Supermarket ile ya Shoppers na kilo huwa ni Tsh 20,000 na kuendelea.

Unaweza lima hii Mboga kama una shamba lako sio la kukodi, Shamba lako binafisi na liwe na maji ya kumwagilia. Hii mboga unaweza vuna kwa miaka 25, inavunwa vijiti vyake na inaendelea kuchipua.

Kama uko Dar au Arusha jaribu kufanya utafiti nenda kwenye Super Market kubwa kabisa kabisa waambie una Asparagus unauza usikie majibu yake. Nenda Super market kubwa achana na zile za mitaani za kibongo Bongo.

FB_IMG_1594733213322.jpeg
FB_IMG_1594733337271.jpeg
images%20-%202020-07-16T073820.972.jpeg
FB_IMG_1594733216589.jpeg
Asparagus%20(1).jpeg
 
Inapandikizwa vitawi au mbegu mkuu?
 
Kwa Ulaya ilikuwa ghali zamani lakini kwa sasa nchi nyingi zinalima na thamani kushuka kwa kuwa inapatikana kwa wingi Kama tutalima sana lazima bei itashuka tu
 
Mimi nimeshachimba maji (Sambarai Moshi) sasa niko kwenye mchakato wa kununua Pump na Solar system. Kuna kampuni yoyote inayotafuta mkulima (contract farming) ili iwe mnunuzi?
 
Miaka miwili hadi mitatu mkuu ili uanze kuvuna but baada ya hapo utavuna si chini ya miaka 25.

Haina Changamoto sana ujue zina taka kuwa kama mianzi ilivyo sana labda wakati wa kiangazi unazimwagilia maji basi, na hapo ni ili zikuwe hata wakati wa kiangazi ila sio kwamba kiangazi kinaweza ziua
Mkuu chasha, heshima kwako, naomba nijuze kifupi, huu mmea ukiupanda mpaka mavuno ni muda gani lakini pia nafahamu lazima kuna changamoto zake, je ni zipi changamoto za kilimo hiki.
 
Mkuu hii soko lake liko wazi kabisa haihitaji mkataba, na unatakiwa kuwa na aridhi usio itumia kama nusu heka au hata robo make ukipanda baada ya 2 year ndo unaanza kuvuna, nenda Hata soko kuu waambie una Asparagus uone watakavyo kufuata au nenda Shoppers Super Market au Village Super Market au watafute Supplier wa Mahoteli makubwa kama Maount Meru na kadhalika waulize
Mimi nimeshachimba maji (Sambarai Moshi) sasa niko kwenye mchakato wa kununua Pump na Solar system. Kuna kampuni yoyote inayotafuta mkulima (contract farming) ili iwe mnunuzi?
 
Ningependa kujua zina faida gani mwilini, especially isiyopatikana katika vyakula vya aina nyingine?
 
Kwenye kitabu cha dawa za asili nilisoma sifa yake ni tiba ya ugonjwa wa moyo. Au kama nimekosea inaongeza mauumbile ya kiume.. Nimekisoma zamani na nimeshapoteza hicho kitabu. Mwenye nacho kinaitwa( Turudi Adeni.)
Ningependa kujua zina faida gani mwilini, especially isiyopatikana katika vyakula vya aina nyingine?
 
Mbona hii inapatikana solo la kitu, k koo ,mbezi na hata mbagala zakhem kabla hujafika rangi tatu.nje ya super makrket ya kivon Kuna mama anauza
 
Good and productive,Constructive thread ever

Pamoja mkuu @Chasha poultry farm
 
Back
Top Bottom