Alex Xavery
JF-Expert Member
- Apr 19, 2015
- 230
- 196
Jamani bado hatujapata ufafanuzi mzuri wa kilimo cha mihogo.hatujajua kwa heka Moja unaweza kupanda kwa kiasi gani na mavuno yake yanakuaje.anayejua basi atusaidie ili tuanze maandalizi
nahitaji mbegu za mpapai nitapata wapi zinakouzwa?Wakuu,
Kutokana na uhitaji wa kuwepo mjadala endelevu na wa tija kwa wajasiriamali, tumeona ni vema tukaweka hii thread kwa maslahi ya wengi.
Tunashauri Mjadala huu ujikitae kwenye maeneo yafuatayo:
1. Aina za mihogo na maeneo inakostawi vizuri
2. Misimu ambayo mihogo inapandwa ni miezi ipi? Inaweza kupandwa misimu yote ya mwaka?
3. Mihogo inashambuliwa na magonjwa yapi? Zipi mbinu za kukabiliana na maradhi hayo?
4. Mihogo inachukua muda gani tangu kupandwa hadi kuvunwa?
5. Hekari moja inaweza kutoa magunia mangapi ya mihogo?
6. Masoko ya mihogo na bidhaa zake ndani na nje ya nchi yapoje?
Asante
Ni Dodoma, ukifika Veyula na Makutupora unaingia kulia. Mimi nimewahi kufika hukoMkuu hawa ARI Hombolo wanapatikana Hombolo kwenyewe au sehemu gani?
Maana mimi nipo maeneo ya Dodoma
Utangulizi
Mihogo hulimwa kwa wingi katika mikoa ya Mara, Mwanza, Kigoma, Mtwara, Lindi, Pwani, Ruvuna, Tanga, Morogoro, Mbeya, na Shinyanga. Muhogo una kiwango kikubwa cha wanga ukilinganisha na nafaka (zaidi ya asilimia 40 kuliko mchele, na zaidi ya asilimia 25 kuliko mahindi). Majani yake hutumika kama mboga na yana virutubishi muhimu hususan vitamini B na protini.
Uzalishaji wake ni wastani wa tani 1,292,000 kwa mwaka. Ili kupata mazao mengi na bora ni muhimu kuzingatia kanuni za kilimo bora cha mihogo hasa zifuatazo:
Mambo Muhimu ya Kuzingatia Katika Uzalishaji
Kuchagua aina ya mbegu
Palizi
- Chagua mbegu kufuatana na mahitaji ya soko, zilizo safi zinazostahimili magonjwa, wadudu waharibifu na zenye uwezo wa kutoa mazao mengi na bora.
Kudhibiti magonjwa na wadudu
- Palilia ili kupunguza ushindani wa virutubishi kati ya mmea na magugu.
- Palilia na kupandishia udongo kwenye mashina.
- Palizi ifanyike mara kwa mara mpaka mihogo inapokomaa.
Muhogo hushambuliwa na wadudu waharibifu kama vidung’ata, vidugamba, mchwa na magonjwa kama batobato na ugonjwa wa michirizi ya kikahawia. Visumbufu hawa wanaweza kusababisha upotevu wa mazao kwa zaidi ya asilimia 90. Hivyo ni muhimu kukagua shamba mara kwa mara ili kuona kama kuna mashambulizi na kuchukua tahadhari mapema.
Maandalizi kabla ya kuvuna
Kukagua shamba
Dalili za muhogo uliokomaa
- Kagua shamba ili kuhakikisha kama muhogo umekomaa. Kwa kawaida muhogo hukomaa katika kipindi cha miezi 9 hadi 24 tangu kupanda kutegemea aina na hali ya hewa. Wakati huo muhogo huwa na unyevu wa asilimia 60 na wanga asilimia 35.
Kuandaa vifaa vya kuvunia, kubeba, vyombo vya usafiri, na vifungashio
- Udongo unaozunguka shina hupasuka.
- Mti wa muhogo huonekana kupevuka.
- Muhogo uliokomaa ni mnene na ukiutafuna utahisi wanga mwingi na maji kidogo.
Vifaa vya kuvunia na kubeba
Vifaa vya kufungashia
- Jembe, Panga, Vikapu, Matenga, na Magunia
Vyombo vya usafiri
- Maboksi ya mbao/plastiki, viroba, Matenga
Kuvuna
- Baiskeli, Matoroli, Mikokoteni, Magari na matela ya matrekta.
Ni muhimu kuvuna mapema ili kupunguza uharibifu unaoweza kusababishwa na mashambulizi ya magonjwa na wadudu waharibifu. Kabla ya kuvuna matawi yote yakatwe ili kurahisisha uvunaji.
Njia ya kuvuna muhogo
Chimbua shina la muhogo kwa kutumia jembe na ng’oa muhogo wote kutoka ardhini. Tenganisha muhogo na shina kwa kutumia panga kali.
Utayarishaji, Hifadhi na Usindikaji wa Mazao ya Mizizi baada ya Kuvuna
Tahadhari
Epuka kukata muhogo wakati wa kuvuna kwani mihogo iliyokatwa au kuwa na majeraha huharibika mapema, kutokana na kuingiwa kwa urahisi na vimelea vya magonjwa.
Kuchambua Na Kusafisha
Kuchambua
Lengo la kuchambua ni kuondoa mihogo isiyofaa, iliyooza na iliyokatwa vibaya na kuharibika.
Kusafisha na kuimarisha maganda
- Mihogo iliyooza isitumike kwa chakula bali ifukiwe.
- Mihogo iliyokatwa au yenye michubuko itumike kwa chakula mapema iwezekanavyo au ioshwe vizuri na isindikwe mara moja.
- Mihogo iliyodumaa itumike kwa chakula cha mifugo.
Kusafisha
Mihogo iliyovunwa huoshwa mara tu baada ya kuvuna ili kuondoa udongo na uchafu mwingine. Mihogo ambayo haikuoshwa vizuri hupunguza ubora wakati wa kukausha na kusindika. Mihogo huoshwa kwa maji na kurudiwa hadi maji yanapokuwa safi na kuona kuwa mihogo imetakata.
Kwa maelezo au mazao mengine unaweza tembelea
nahitaji mbegu za mpapai nitapata wapi zinakouzwa?
asante mkuu kwa ushauriUnataka mipapai iliyooteshwa (miche) au mbegu upande mwenyewe? chagua kwa uangalifu sasa hivi kuna tatizo la magonywa ya fangus na virus.
Japo mimi sio Chacha, tuna mradi pale Rufiji kwenye zao la Muhogo uko chini ofisi ya waziri mkuu, tunawajengea wakulima uwezo katika uzalishaji, usindikaji na upatikanaji wa masoko jina la mradi kwa kizungu wanaita Marketing Infrastructure Value Addition and Rural Finance Program (MIVARF).Chacha nami naomba kujuzwa zaidi na sanasana ni utafiti uliofanywa Italy na pia kama kunamtu anajua matumizi ya Starch itokanayo na mihogo.
Mkuu naomba uchungulie PM yakoJapo mimi sio Chacha, tuna mradi pale Rufiji kwenye zao la Muhogo uko chini ofisi ya waziri mkuu, tunawajengea wakulima uwezo katika uzalishaji, usindikaji na upatikanaji wa masoko jina la mradi kwa kizungu wanaita Marketing Infrastructure Value Addition and Rural Finance Program (MIVARF).
Kuna kata tatu tunafanya nazo kazi ambazo ni Bungu, Dimani na Ruaruke. Pale Bungu kuna viwanda viwili. Kikubwa kinajihusisha na utengenezaji wa starch kwa matumizi ya hospitali kwa ubia na watu wa Marekani na kidogo ni kuandaa bidhaa za chakula hasa unga. Katika tani 60 za muhogo mbichi mchakataji anaweza kupata wastani wa tani 16 za starch. Matumizi ya Muhogo kwasasa ni Kuzalisha kachori, unga, chips, kuni, mboga, maandazi na mikate. Kwa upande wa kiwanda wanatengeneza starch pia maganda ya muhogo unaochakatwa yanatarajiwa kutengeneza umeme kwa matumizi ya kiwanda na mwingine kuuza Tanesco.
Masoko moja ni Bungu na Kibiti kwa wakulima wadogo maarufu chini ya muembe pia kwenye viwanda tajwa. Lakini kuna masoko ya Dar es Salaam viwandani kwa Mama Mwaipopo food products na Power Food kawe. Mahitaji ya muhogo mbichi pia yapo masoko ya Kariakoo, Tandika na Kawe ambapo wakulima kwa vikundi wamesaini mikataba na wanunuzi mwaka huu 2016.
Huduma za mikopo kwa wakulima wa muhogo kwa kiasi kidogo hasa za uongezaji thamani zinapatikana benki ya wananchi wa Dar es Salaam (DCB) kwa mikopo ya vikundi. Juhudi zinafanyika wapate mikopo pia kupitia PASS. Usafiri ni rahisi kutoa muhogo ukanda huo kutokana na magari mengi yanayotoka Mtwara na Lindi kupeleka mizigo kutokuwa na mizigo yakupeleka Dar. Nikutakie kila la kheri.
Nimekujibu whatsappMkuu naomba uchungulie PM yako
Nimekujibu whatsapp
Huu mradi uko nchi zima halmashauri zilishindanishwa kwakuandika maandiko tofauti tofauti. Kwa mkoa wa Mtwara zilishinda wilaya mbili za Tandahimba na Nanyumbu kwenye zao la Korosho.Sorry jamaa yangu, huu mradi wa muhogo umebase huko Rufiji tuu au hata mimi nikiamua kulima huko Newala kwa kufuata aina (ya muhogo mnaohitaji) na ulimaji/ubora mnaouhitaji mnanunua??
Ningependa nijifunze kuhusu huu muhogo na soko lake, nitakutafuta PM ndugu. Nashangaa ndugu zangu mihogo wanalima miaka miwili halafu inawadodea hata soko haina.Huu mradi uko nchi zima halmashauri zilishindanishwa kwakuandika maandiko tofauti tofauti. Kwa mkoa wa Mtwara zilishinda wilaya mbili za Tandahimba na Nanyumbu kwenye zao la Korosho. Hivyo mradi unatekelezwa kwa zao hilo. Muhogo ni kwa Mkuranga na Rufiji ambapo sisi tulipewa jukumu lakuwajengea uwezo wakulima wa Rufiji na tunaona mafanikio makubwa. Kimsingi kuna mabadiliko na wakulima sasa wamehamasika tofauti na awali walikuwa wanatugomea kutokana na kuwa na picha mbaya ya miradi ya maendeleo.
Tembelea library SNAL na ofisi za MIVARF Arusha utapata majibu, unless uwe unataka kurudia.Ninaona kuna haja ya kufanya "stakeholders mapping "kwenye zao hili la Muhongo ili kuweza kuboresha value chain ya zao hili na kuwezesha stakeholders kupunguza vikwazo wanavyokabiliana navyo wakati wa utekelezaji wa shughuli zao.
Asante kwa taarifa...! Ila nadhani review ya hii kitu ni muhimu maama wadau wanabadilika kutokana na mazingira na nyakati.Tembelea library SNAL na ofisi za MIVARF Arusha utapata majibu, unless uwe unataka kurudia.