Mkuu somo litatusaidia wengi. Mungu akupe busara ya kuliweka hilo somo hapa jukwaaniNunua mbegu zako nitakuambia jinsi ya kufanya ziote na ni rahisi.
Je utaniruhusu kutoa somo japokuwa si mtaalam kwa faida ya wengine
Mkuu unaweza kunitumia kwa email: teakrondo@gmail.com na ntajaribu kuziweka jukwaaniNimeshindwa jinsi ya kuatach pictures
Kabla mbegu hazijaota unatakiwa uchukue udongo ambao unarutuba unachanganya na Dawa yeyote ambayo inazibiti fungus. Fungicides.
Changanya vizuri na udongo kisha weka ktk vifuko .
Vifuko hivi viandalie sehemu nzuri ambayo kabla ya kuvipanga unanyunyuzia fungicides.
Mbegu zitakapoanza kuota huwa zinaanza na kitawi kimoja, kitakapochomoza kitawi cha pili amisha huo mche kwenda vkwenye vifuko kama picha mkuu atakapo ambatanisha.
Uhamishaji ufanyike alfajili mwisho saa nne asubuhi
Mkuu picha nimeweka tayariTusubili picha zikiwekwa ili nieleweke vizuri
Baada ya hapo inatakiwa miche itunzwe vizuri isimwagiwe Maji Sana.
Sasa la kuzingatia miche inapokuwa ktk kitaru,
Mche wa mtiki ukiwa unakwenda kupandwa sehemu yenye mvua finyu hutakiwa kutayalishwa bado ikiwa ktk kitalu ili kuhimili hali hiyo.
Kwa hiyo kuna virutubisho nilipewa kutoka ktk duka Moja nchini Kenya ambavyo mche hutanuka shina bila ya kuwa mrefu.
Miche hutakiwa kutunzwa sio chini ya miezi saba kabla ya kupelekwa Shambani
Mkuu hiyo miche ya mwezi March ilikuwa imekaa shambani kwa muda gani?Sawa sawa ngoja nitafute majina ya dawa na virutubisho nilivyotumia.