Kilimo cha Mitiki: Utaalamu na biashara yenyewe


Nataka kujua juu ya aina ya udongo mzuri ambao unastawisha mitiki
 
mikaratus inavumwa baada ya muda gani?
 

daah! umemshushua jamaa hadi naogopa kuuliza swali.
 
Naomba msaada kwa mwenye kujua utaalamu wa upandaji miti aina ya mitiki na jinsi ya kuifanya ikue haraka haraka.

Tafadhali naomba anielekeza kuna project naifanya.
 
Acha hatua tano kila baada ya shimo unapopanda, matawi yake ni lazima kuyakata kila yanapoota ili mti ukue kuelekea juu kwa haraka na vile vile kunyooka, usiache tawi hata moja zaidi kuchwa cha mti(sina jina lingine la kuita)
 

Utangulizi
Mbegu za mitiki zinapatikana Tanzania Tree Seed Agency wako Msamvu Morogoro.Kilo moja ya mbegu za mitiki inatosha kuotesha kwenye shamba la hekta moja, ambayo ni wastani wa miti 1000 mpaka 1500 kama itaoteshwa na kutunzwa vizuri

Matayarisho:
  1. Loweka mbegu kwa muda wa siku 3 mpaka 7 ukiwa unabdili maji kila baada ya masaa 12. Hii ni kwasababu ganda la nje la mbengu ya mtiki ni gumu sana na lina sumu mbaya.
  2. Baada ya masaa 72 anika mbegu zako juani kwa masaa 12.
  3. Tengeneza kitalu, weka mbolea ya wanyama au mboji, kisha panda mbegu zako kwenye kitalu.
  4. Mwangilia maji kila siku asubuhi na jioni, mbegu zitaanza kuota baada ya siku 10 hadi 20.
  5. Miche ikifikia urefu wa futi moja, unaweza sasa kuiotesha kwenye shamba lako ulilotayarisha kwa ajili ya kuotesha miti.
  6. Kabla ya kung’'oa miche hakikisha unamwaga maji mengi, ili mizizi isikatike sana, kisha chukua kisu chenye makali ya kutosha na kata ncha ya juu ya mti na ondoa majani, hii inasaidia mti kuchipuka upya hasa eneo ambalo halina maji mengi.
  7. Otesha miti futi 6x6 mitiki inaposongamana, hurefuka haraka ikikimbilia jua angani, hivyo kwa vipimo hivyo miti yako itakuwa mirefu sana na iliyonyooka, baadaye unaweza kuipunguza na kuuza fito za kujengea.
  8. Ili upate mbao bora hakikisha unaondoa matawi yanayochipuka pembeni hadi mti ufike zaidi ya futi 10 kwani ndiyo yanafanya mbao kuwa na mabaka (vidonda)
Bei ya Kilogram Moja (Kg 1) ya mbegu za Mitiki ni TZS 12,500

Tanzania Tree Seed Agency wapo Dodoma Rd, mkoa wa Morogoro kama unaenda Kihonda. Kituo kinaitwa "Misitu" au "Vybes"
 
Kaka Mack vipi baada ya mda gani nitaweza vuna iyo miti ya mitiki? Na je majani yake mbuzi wanakulaaana maeneo nayifikiria panda yana mifugo mingi sana
 
Hivi wanayosema miti inayovunwa baada ya miaka 50 ni miti gani wanasema ina fedha nyingi sana.
 
Hivi wanayosema miti inayovunwa baada ya miaka 50 ni miti gani wanasema ina fedha nyingi sana.

Miaka 50 ni mingi sana, miti ipo aina nyingi na kwa ajili ya matumizi mbalimbali km mbao, nguzo, mkaa, kutengenezea mapambo n.k. Mara nyingi miti kwa ajili ya nguzo ndio huwa na bei sana.
 
Mitiki inastawi vizuri katika udongo wa asili ipi, na hali ipi ya hewa?
 
Mitiki inastawi vizuri katika udongo wa asili ipi, na hali ipi ya hewa?
Hali ya hewa ya mikoa ya pwani, pia uzuri wake hustawi ktk aina nyingi za udongo hata km ni kichanga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…